Kwa hulka hizi za Magufuli,sipati picha mgogoro wa kisiasa Zanzibar ukilipuka!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,171
103,637
Nchi na dunia nzima imejua matumizi ya nguvu anayotumia Rais Magufuli katika kutatua changamoto za kisiasa na kiuchumi

Ninatafakari ikiwa mgogoro kisiasa wa Zanzibar ukiamka tena leo,sipati majibu itakuweje

Mgogoro wa kisiasa Zanzibar uliopandikizwa makusudi na viongozi wenye uchu wa madaraka wasiojali maamuzi ya watu, wenye tamaa ya kubaki kwenye madaraka pasi na uwezo wala uthubutu wa kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi.

Katika bunge 2005 JK aliwahi kuahidi kuwa ataushughulikia mgogoro wa Zanzibar. Akaitisha vikao Bagamoyo kwa miezi isiopungua 14. Akiwa Mwenyekiti wa CCM kazi yote iliyofanywa na viongozi wa CCM na CUF kwa kutumia fedha za wananchi maskini wa Tanzania, ikadharauliwa. Kikao cha Butiama kikakataa proporsal ya timu ya mazungumzo. Very simple!

Katika miaka yake kumi JK ameondoka mgogoro wa kisiasa Zanzibar ukiwa ni mbaya zaidi ama sawa na mwanzo alipoingia.

Sasa huyu anko yakiibuka atayabebea mbeleko gani.
 
Hayawezi kuibuka, Raisi Magufuli ana high IQ above average, analiona Raisi wa JMTZ wewe na kundi lako mtakuja kuliona labda miaka 10 ijayo, hivyo usihofu kila kitu kiko sawa na kitabakia hivyo!
 
Nchi na dunia nzima imejua matumizi ya nguvu anayotumia Rais Magufuli katika kutatua changamoto za kisiasa na kiuchumi

Ninatafakari ikiwa mgogoro kisiasa wa Zanzibar ukiamka tena leo,sipati majibu itakuweje

Mgogoro wa kisiasa Zanzibar uliopandikizwa makusudi na viongozi wenye uchu wa madaraka wasiojali maamuzi ya watu, wenye tamaa ya kubaki kwenye madaraka pasi na uwezo wala uthubutu wa kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi.

Katika bunge 2005 JK aliwahi kuahidi kuwa ataushughulikia mgogoro wa Zanzibar. Akaitisha vikao Bagamoyo kwa miezi isiopungua 14. Akiwa Mwenyekiti wa CCM kazi yote iliyofanywa na viongozi wa CCM na CUF kwa kutumia fedha za wananchi maskini wa Tanzania, ikadharauliwa. Kikao cha Butiama kikakataa proporsal ya timu ya mazungumzo. Very simple!

Katika miaka yake kumi JK ameondoka mgogoro wa kisiasa Zanzibar ukiwa ni mbaya zaidi ama sawa na mwanzo alipoingia.

Sasa huyu anko yakiibuka atayabebea mbeleko gani.
Atahamisha watu wote aanze upya visiwa na watu wengine
 
Back
Top Bottom