KISUTU, DAR: Maxence Melo akutwa bila hatia shtaka la Kikoa. Apewa 'Conditional Discharge' kwenye shtaka la kutotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Hukumu ya kesi namba 458 ya 2016 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums inatarajiwa kusomwa leo Novemba 17, 2020 katika Mahakama ya Kisutu

Katika shauri hili lenye mashtaka mawili, watuhumiwa wanashtakiwa kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa kwa kikoa cha DO-TZ

Katika shtaka la pili, Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa JamiiForums kutoa taarifa za Wanachama wawili waliodaiwa kuandika kuhusu madai ya uhalifu uliokuwa ukiendelea CRDB, kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari.

Ifahamike kuwa taarifa za Wanachama ambazo zilitakiwa kutolewa ni
  • IP-Address,
  • Barua pepe,
  • Majina Halisi ya Wanachama hao.
  • Pia ilitakiwa zitolewe post zote zinazohusu Uhalifu unaofanyika katika benki ya CRDB
======

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia kwa Masharti ya kutokufanya kosa kama hilo ndani ya Mwaka mmoja, Mkurugenzi wa JamiiForums Maxence Melo, katika Shitaka namba mbili la kuzuia Upelelezi wa Jeshi la Polisi

Aidha, Shitaka la Kwanza la kutosajili JamiiForums kwa kikoa cha Dot-TZ akikutwa hana hatia.

Mshitakiwa namba mbili amekutwa hana hatia makosa yote Mawili. Hakimu Huruma amesema, Mshitakiwa namba mbili Mike Mushi alikuwa kama Msindikizaji kwenye hii kesi namba 458 ya Mwaka 2016.

Katika shtaka la pili, Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa JamiiForums kutoa taarifa za Wanachama wawili waliodaiwa kuandika kuhusu madai ya uhalifu uliokuwa ukiendelea CRDB, kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari.

Akiongea baada ya kutolewa hukumu hiyo, Maxence amesema hajaridhishwa na uamuzi uliotolewa lakini anaheshimu Mahakama na Sheria za Nchi. Amesema anaongea na mawakili wake waipitie hukumu kwanza ndipo waone kama wakate rufaa au la na kuongeza kuwa ni mapema sana kutolea kauli uamuzi huu kwani anaamini hakuvunja sheria yoyote ya nchi.

Hata hivyo, waliotuhumiwa kuikosesha Serikali mapato walikamatwa na kushtakiwa chini ya hakimu Huruma Shaidi (aliyetoa hukumu hii) kama inavyosomeka hapa > Watumishi wa TPA, CRDB wafikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi

 
Mahakama ya Kisutu siyo final. Kuna mahakama kuu na mahakama ya rufaa...
Na wote wanahaki ya kukata rufaa kama hawataridhishwa na hukumu ya Mahakama ya Kisutu. Tofauti hapa ni kwamba kama Jamhuri ikishinda basi wakata rufaa watafanya hivyo huku wakiwa wameanza kutumikia adhabu, iwe ya kulipa faini au kifungo! Tumuombe Mungu Aepushe hilo, Aamin
 
Back
Top Bottom