Kwa huduma za Mafunzo ya udereva wa awali karibu sana Home of Excellence Driving School

Manala An Academician

Senior Member
Oct 10, 2016
118
54
UDEREVA WA KUJIHAMI

KUTOKA HOME OF EXCELLENCE DRIVING SCHOOL

Imeandikwa na Mr. Manala Tabu Mbumba, Mhadhiri Msaidizi na Mshauri wa Magari-Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)

Home of Excellence Driving School inatoa huduma bora kabisa za udereva pamoja na kusaidia upatikanaji wa leseni kwa wanafunzi wake watakaohitaji kwa kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka kwa mda mfupi.

Huduma zetu hutolewa kwa gharama nafuu sana.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0676060228/0743156408 au fika katika ofisi zetu zilizoko Mabibo mkabala na lango kuu-NIT, Mabibo Road, Dar es salaam, Tanzania

Haitoshi kujifikiria kwamba kila wakati unaheshimu sheria za usalama barabarani, bila kutekeleza dhana ya udereva wa kujihami ambao ni udereva wakutumia akili ili kuepusha ajali.

Falsafa ya udereva wa aina hii inamfanya dereva wakati wote aendeshe gari kwa kutambua athari zinazoweza kujitokeza na mbinu mathubuti za uzuiaji wa athari hizo
Kwa maneno mengine, udereva wa kujihami unakamilisha na mambo makuu matano kama yanavyoonekana hapa chini

1. Kuangalia
Hii inamkumbusha dereva kila wakati kabla hajaanza kuendesha lazima aangalie mbele, pembezoni na nyuma ili kumuwezesha kuwa na picha halisi ya hali ya barabara na kuipeleka kwenye akili kwa ajili ya upangaji, uamuzi na utekelezaji, uangaliaji huu pia unahusisha ukaguzi unaokubalika wa gari analoliendesha na vifaa mbalimbali vinavyotakiwa kuwemo kisheria

2. Kutambua
Kipengele hiki kinamtaka dereva kuwa na uwezo wa kuzing'amua hatari zote na jinsi yakuchukua hatua iwapo zitatokea, mfano umetambua mbele kuna watoto wa shule wapo kandokando ya barabara inapashwa utambue silka au tabia ya watoto kutokuwa waangalifu sana ili uweze kuwa na tahadhali

3. Kutabiri
Hapa sana tunamkumbusha dereva kujiuliza kinachoweza kutokea kutokana na hatari ulizoweza kutambua mfano pale ulipotambua kuna watoto wa shule hivyo utatabiri kuwa wanaweza kuvuka barabara bila kuangalia magari vizuri.

Hivyo, unapashwa wakati wote kutabiri maeneo yote ya hatari kwa kutumia macho yako vizuri

4. Kuamua
Dereva anayejihami daima anatakiwa kutoa maamuzi sahihi na ya haraka, kwani kuchelewesha kwa maamuzi yaweza kuleta madhara na pengine kupelekea ajali mbaya. Hivyo, mara baada tu yakutafakari hatua mbalimbali za kuchukua kama vile kupunguza mwendo, kupiga honi, kuongeza mwendo au kusimama n.k inakubidi kuamua haraka juu ya hatua uliyokusudia.

5. Kutekeleza
Dereva yoyote anapofanya maamuzi daima yanatakiwa kwenda sambamba na utekelezaji, mfano ikiwa umeamua kupunguza mwendo, basi hana budi kupunguza mwendo huo kwani kuendelea kwenda kwa kasi ya juu wakati mazingira hayaruhusu uwekezano wa kupata ajali ni mkubwa.

Aidha mambo hayo dereva anapashwa kuwa nayo akilini ili yaweze kumsaidia katika kutekeleza tendo la kujihami na kuweza kuokoa ajali ambayo angeweza kusababisha au kusababishiwa

Hata hivyo, ukamilifu wa tendo hili lakujihami huwa na mbinu mbali mbali zinazoamuriwa na sababu kadhaa ikiwemo mazingira, gari, binadamu n.k.

Cha muhimu dereva anapashwa kujua mazingira yatakayokuwa yanamzunguka kwa wakati husika ili aweze kuja na mbinu sahihi katika kuokoa athari ambazo zingeweza kutokea.

Hapa nitakuonesha mbinu chache tu ambazo naamini zitakuwa msaada kwa kila mmoja wetu

A. Kama kuna gari lingine mbele yako
Uendeshapo gari na mbele lipo jingine ikatokea kwa ghafla dereva aliye mbele yako anasimama, katika kujihami unapaswa kukumbuka kuwa kila mara uendeshapo gari acha nafasi ya kutosha kati yako na aliye mbele yako (tafiti nyingi zinakadiria umbali wa mita 7) na kila wakati unapaswa kufikiria kuwa mwenzako anaweza kusimama ghafla bila kuonesha ishara yeyote kwa hiyo kaa umbali utakaokuwezesha kuona tairi za nyuma za gari lililo mbele yako daima

B. Umbali wa kusimama
unapashwa kuelewa tu kuwa hakuna gari linaloweza kusimama papo hapo kwa hiyo unapashwa kutembea mwendo ambao kwako utakupa urahisi wakuweza kusimama kwa wakati kunapokuwa na dharura yeyote aidha unapotaka kusimama kamwe usishike breki za ghafla kwani zaweza kuyumbisha gari lako nakupelekea athari zingine zisizo tarajiwa badala yake anza kujiandaa katika umbali unaokubalika ili usilete athari kwa watumiaji wengine wa barabara

C. Kwa gari lililo nyuma
Uendeshapo gari lako daima kuwa msaada wa dereva aliye nyuma yako kwa kutoa ishara kwa kila hatua ya kitendo unachofanya.

Zingatia kutoa ishara katika umbali unaokubalika kumfanya aweze kuchukua hatua pia bila kuleta athari zozote.

Mfano unapotaka kusimama au unakaribia kwenye taa na unahisi kabisa muda wa taa ya kukusimamisha inakaribia kuwaka anza kukanyaga breki zako taratibu na uhakikishe taa za nyuma za breki zinawaka na kama haziwaki unashauriwa utumie mkono wako wa kulia kwa gari ya kuendeshea kulia mpe ishara ya kwamba utasimama na uhakikishe amekuelewa ndipo uweze kusimama

D. Dereva mwingine kuendesha upande wako

Inapotokea dereva anayekuja anaendesha upande wako kwasababu anazozijua yeye labda amelewa, uchovu n.k kitu ambacho kinaweza kupelekea ajali ya uso kwa uso unashauriwa kukaa kushoto zaidi na iwapo dereva huyo amevuka msitari wa katikati ya barabara, jaribu kumpa tahadhali kwa kumpigia honi.

Na kutegemea na hali utakayomuona unashauriwa kupunguza sana mwendo na kamwe usiende kulia maana anaweza kushituka na kuleta madhara makubwa cha muhimu ikiwezekana toka nje kabisa ya barabara kama ni salama

E. Magari kwenye njia panda
Hii ni miongoni mwa sehemu hatari sana, aina ya njia hizi huongozwa na mifumo tofauti tofauti ya mawasiliano mfano alama, taa na zingine haziongozwi na chochote.

Daima unapokaribia njia panda ya aina yoyote kati ya hizo tatu nilizokutajia hapo na ukaona gari jingine linakuja upande mwingine kwa kasi na pengine kuna alama ya kusimama lakini hasimami au kuna taa nyekundu inawaka na hasimami inakupasa upunguze mwendo zaidi huku ukiangalia huku na huku na kutoa ishara ya gari iliyoko nyuma na ikiwezekana simama kumpisha uliyeona anaweza kuhatarisha hali ya barabara

Kwa ujumla katika njia za panda yeyote unapopita unashauriwa kuangalia pande zote na kujiridhisha kama ni salama ndo uendelee na safari.

Kamwe usigombee njia utapita tu pale itakapokuwa salama na usijaribu kabsa kushindania njia na dereva mwingine kuwa na subira ktk kila jambo labda kwasababu za kiusalama tu.

F. Gari linalotaka kukupita
Unashauriwa kuangalia magari yajayo mbele yako, punguza mwendo wako na ubane zaidi kushoto kisha toa ishara yakuruhusu gari linalokupita kama ni salama na unaporuhusu lipite basi usije kubadilisha tena maamuzi ukaanza ushindani

G. Kuovertake
kwanza hakikisha uko umbali unaotakiwa kwa maana unaweza kuziona tairi za nyuma za gari unalotaka kulipita.

Ukiwa bado hujaamua kupita angalia pande zote kujiridhisha hakuna gari mbele inayoweza kuzuia wewe kupita lakini pia tumia vioo vyako vizuri kuangalia kama hakuna gari nyuma yako inayoonesha dalili ya kupita kisha toa ishara yakuomba kulipita gari na mbele yako na hakikisha limekuruhusu kisha utafakari mwendo wako na uwezo wa gari lako.

Kama unaweza kulipita gari la mbele yako kisha hakikisha alama za barabarani zinakuruhusu kufanya hivyo baada ya kujiridhisha kama ni salama unaruhusiwa sasa kuhamia upande wa kulia kwa mwendo mkubwa zaidi ya gari unalotaka kulipita na mara baada ya kupita hakikisha unaonesha ishara yakuanza kurudi wakati huo ukitumia kioo cha kushoto kuangalia hilo mpaka uweze kuona tairi zake za mbele ndo unaweza kurudi upande wako.

Ndugu zangu, ziko mbinu mbalimbali za kujifunza katika mada hii muhimu ambazo madereva wengi wameonekana kushindwa kuzitumia mbinu hizi ama kwa kuzipuuza ama kutozijua na matokeo yake ajali za barabarani zimeendelea kuathiri maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine, kitendo kinachorudisha nyumba dhima ya Taifa letu kila siku.

Mimi napenda kutoa rai yangu kwa madereva wa aina zote kuweza kujifunza mbinu mbalimbali katika taasisi zilizotambuliwa na mamlaka katika kutoa huduma hizi ili wote kwa pamoja tuweze kuwa na uelewa na kuweza kutokomeza janga hili kubwa la ajali zinazolikumba taifa letu hasa ikizingatiwa katika vyanzo vikuu vya ajali binadamu ameonekana kuwa chanzo kikubwa sana cha ajali nyingi tunazozishuhudia, hali ambayo tuna uwezo wa kuizuia kwa sisi wenyewe kuamua tu pamoja na mambo mengine ni kufuata taratibu zinazokubalika kisheria zinazoweza kukufanya ukawa dereva na kuepuka njia zisizo rasmi ambazo wengi wamekuwa wakizitumia na kujikuta wakiharibu sifa za madereva nchini.

Inawezekana kufikia lengo la asilimia sifuri za ajali kama hatua madhubuti zitaendelea kuchukuliwa na wadau wote wanaounda mfumo mzima wa usafirishaji na siyo jambo lakuachia serikali kupitia jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani.

Kama una ndugu, jamaa na rafiki ungependa aweze kupata umahiri wakuendesha gari, HOME OF EXCELLENCE DRIVING SCHOOL ipo kwa ajiri yako.

Huduma zetu ni kukuandaa kuwa dereva mahiri na mwenye vigezo kisheria, taaluma iliyokuwa imesahaulika kwa kipindi kirefu, shule itasimamia pia zoezi la upatikanaji wa leseni watakaopenda kwakuzingatia taratibu zilizowekwa na mamlaka kwa mda mfupi zaidi, Piga simu au WhatsApp 0676060228/0743156408 kupata maelezo zaidi.

Huduma zetu zinatolewa kwa gharama nafuu na utahudumiwa wakati wowote na popote ulipo

Fika ofisini kwetu Tunapatikana, Mabibo, Mkabala na lango la NIT, Mabibo Road, Dar es salaam, Tanzania

Thanks

Contact us HOME OF EXCELLENCE DRIVING SCHOOL

FACEBOOK PAGE: Home of Excellence Driving School

Call: 0676060228
WHATSAP:0743156408
WEBSITE: www.excellencedriving.ac.tz
Instagram: homeofexcellencedrivingschool
 
Baadhi ya huduma zetu ni
1. Mafunzo ya kumfuata mwanafunzi na kumfundisha aliko
2. Mafunzo ya Mtu mmoja mmoja na mwalimu wake kwenye gari
3. Mafunzo ya siku za weekend tu kwa wote wasio na mda siku za kawaida
4. Mafunzo kwa wanafunzi walifika umri miaka 18 na kuendelea

NB:
A. Shule pia inasaidia mchakato mzima waupatikanaji wa leseni kwakuzingatia taratibu zilizowekwa na mamlaka husika kwa mda mfupi zaidi.

B. Vipindi huanza saa 12:30 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni, mwanafunzi anaruhusiwa kuchagua mda wowote hapo katikati kutokana na nafasi yake.
IMG-20191126-WA0003.jpg

Kwa maelezo zaidi
Tafadhali tupigie: +255 676 060 228
Au tembelea ofisi zetu zilizopo
Mabibo, mkabala na lango kuu la kuingilia Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji, NIT, Mabibo Road, Dar Es Salaam, Tanzania
Ahsante na karibu
 
UKAGUZI WA GARI

KUTOKA ESSENCE DRIVING SCHOOL

Inaandikwa na Mr. Manala Tabu Mbumba, Mhadhiri Msaidizi na Mshauri wa Magari-Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)

Essence Driving School inatoa huduma bora kabsa za udereva pamoja na kusaidia upatikanaji wa leseni kwa wanafunzi wake watakaohitaji kwakufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka kwa mda mfupi.

Huduma zetu hutolewa kwa gharama nafuu sana. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0676060228/0743156408 au fika katika ofisi zetu zilizoko Mabibo mkabala na lango kuu-NIT na Tegeta, Dar es salaam, Tanzania

Tafsiri nyingi zinasema, gari ni chombo cha moto kinachotembea kwenye nchi kavu na chenye uwezo wa kuzalisha nguvu yake ili kuweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kutokana na tafsiri hii, na mara zote huundwa na sehemu kuu mbili yaani bodi pamoja na 'chasis' bodi ni ile sehemu inayofunika gari ambayo hufanya kazi za kubeba abiria na mizigo kutegemea na kusudi la kuundwa kwake, mara nyingi tunazo bodi za aina mbali mbali katika magari mfano tumezoea kusikia 'saloon' ambayo ni moja ya muundo wa bodi unaotumiwa na moja ya magari madogo, yako mengi yakuzungumza juu ya bodi lakini kwakuwa hii sehemu lengo letu kwa mada hii nitatafuta mda nitaichambua kwa kina ili msomaji uweze kuwa na uelewa mpana zaidi
Sehemu ya pili ya gari yaani 'chasis' ni sehemu kuu inayounda gari na kwa tafsiri rahisi unaweza kuita ni 'gari bila bodi' kwa maana kwamba ukiondoa bodi kwenye gari kinachobaki kiujumla wake huitwa chasis, nitoe angalizo tu kwamba si gari zote hasa gari za toleo la siku hizi nyingi zimeundwa kiasi ambacho huwezi kutenganisha sehemu hizi mbili labda kwakuharibu tu.

Katika chasis tunaomfumo maalum unaolifanya gari liwe tofauti na vyombo vingine vya usafiri kwakuzalisha nguvu yake binafsi, mfumo huu huitwa injini ambao ndo hufanya kazi ya kutengeneza nguvu yake kwa kushirikiana na mifumo mbalimbali iliyotengenezwa katika mfumo huu wa injini mfano mfumo wa uchomaji, mafuta, hewa, ufuaji umeme n.k baada yakuzalishwa nguvu hiyo husafirishwa kutoka kwenye injini kupitia mifumo mbalimbali mpaka kwenye matairi ya kuendeshea yaani 'driving wheels' na hatimae gari huweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Ndugu zangu, gari ni chombo kilichoundwa na mifumo mbalimbali ambayo hufanya kazi tofauti kwa ushirikiano ili kutimiza kusudi lililokusudiwa ktk gari hilo baadhi tu ya mifumo hiyo pamoja na niliyokutajia tunayo mingine kama mfumo wa breki, mneso, taa n.k. Ili gari liweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi ni jambo la muhimu sana kuhakikisha mifumo yote iliyoko kwenye chombo hiki haina hitilafu ya aina yeyote sawasawa na binadamu tu kwamba akitokea hata kidole hakiko sawasawa basi ufanisi wake huathirika kutokana na kiungo hicho kuwa tu hakiko katika hali iliyozoeleka. Kwa maneno mengine, mifumo yote iliyowekwa ktk gari ni lazima kuhakikisha kila mmoja unawajibika sawasawa kutimiza kusudi lake.

Ili kuhakikisha mifumo hii inafanya kazi sawasawa, dereva au mtumiaji yeyote wa chombo hicho anawajibika kufanya ukaguzi katika chombo chake kwakupitia mfumo mmoja baada ya mwingine kwakuzingatia maelekezo ya mtengenezaji wa gari kupitia kitabu cha mwongozo ambao unakuwemo ktk kila gari.

Hata hivyo, ni vizuri kujua kwamba ukaguzi umegawanyika ktk makundi makubwa mawili yaani ukaguzi wa kisheria ambao huu hufanyika kwa mjibu wa sheria zilizoweka, ukaguzi huu huhusisha uangaliaji wa bima, kadi ya gari, leseni ya dereva n.k na mara nyingi tumekuwa tukishuhudia ukifanywa na askari wa kitengo cha usalama barabarani.

Kundi la pili ni ukaguzi wa kiusalama na mara zote huu hufanywa na dereva, mmiliki au mtaalamu aliyeidhinishwa kuwa na sifa zinazokubalika ktk kulikagua gari na hata kufanya matengenezo ingawa kutokana na hali halisi ya ukosefu wa chombo maalumu cha kuratibu wataalam hawa tumekuwa tukishuhudia kazi hizi zinafanyika kiholela na hata kuongeza matatizo hasa ktk magari ya toleo la siku hizi ambayo kimsingi yanatumia teknolojia ya juu mno.

Ukaguzi huu wa kiusalama unalenga kuhakikisha wakati wote mifumo yote iliyopo katika gari inafanya kazi kwa ufanisi unaokubalika kadri ya maelekezo ya mtengezaji wa gari husika na ieleweke kwamba ukaguzi huu umegawanyika katika makundi makubwa mawili yaani ukaguzi wa kila siku na ukaguzi wa mda maalum.

Makundi haya mawili yamewekwa makusudi kabsa kwa kuzingatia aina na tabia ya mifumo iliyopo katika gari kwa mfano iko mifumo ambayo ikitokea hitilafu kidogo tu madhara yake yaweza kuwa makubwa sana hivyo kuweza kuepuka uwezekano wakutokea kwa madhara hayo ikaonekana ni vema kuwe na ukaguzi wa mara kwa mara ktk gari lako ili kujihakikishia usalama wake mfano tu wa sehemu zinazotakiwa kukaguliwa mara kwa mara ni pamoja na mfumo wa breki, matairi, ukaguzi wa jumla wa nje ya gari lako, kuangalia kama kuna majimaji yamedondoka chini mfano maji ya kupozea, oili ya injini, mafuta ya usukani, oili ya gear box, difu n.k
Kundi la pili huhusisha ukaguzi wa mda maalumu kwakuzingatia umbali wa gari liliotembea, ieleweke tu kwamba kila kipuri kilichofungwa ktk gari kina mda maalum wakutumika kikiwa na ubora wake na baada ya hapo inashauriwa ukibadilishe au ufuate ushauri ulioelekezwa na mtengenezaji wa gari husika. Changamoto kubwa iliyopo ktk watumiaji wengi wa magari wamekuwa hawana tabia yakubadilisha vipuri vya magari yao mpaka utokee uharibifu hali ambayo mbali na kuongeza gharama na mda wa matengezo pia imekuwa ikiongeza uwezekano wa kuhatarisha maisha ya watumiaji wengi wa vyombo vya moto. Nisisitize tu kwa uhumimu kwamba kuelewa maeneo ya kukagua kila wakati na kwa wakati maalum haitoshi bali mbinu sahihi na nini chakukagua ktk kila eneo ni jambo la muhimu sana kuelewa kila mmoja wetu.

Ndugu zangu, ziko faida nyingi sana za kuzingatia taratibu za ukaguzi wa gari, ikiwemo kukuepusha na uwezekano wa kupata ajali inayotokana na uharibifu wa gari lako, sababu ambayo bado imeonekana kuwa changamoto katika nchi yetu. Tatizo ambalo linaweza kukomeshwa bila gharama yeyote zaidi ya kuelewa tabia za gari lako na kufuata maelekezo ya mtengenezaji. Mimi kila mmoja wetu achukue hatua kuanzia unapomaliza kusoma makala hii, ili tuweze kuwa na uelewa wa pamoja katika kipengele hiki muhimu cha ukaguzi, kwa wasio na elimu hii usisite kuwasiliana nasi kuweza kupata mafunzo haya ili uwe balozi muhimu wa kulinda usalama wa chombo chako. Uwe na wakati mwema🤝

Kama una ndugu, jamaa na rafiki na ungependa aweze kupata umahiri wakuendesha gari, pikipiki na Bajaj HOME OF ESSENCE DRIVING SCHOOL ipo kwa ajiri yako, Huduma zetu ni kukuwezesha uweze kufikia malengo yako yakuwa dereva mahiri na mwenye vigezo kisheria, taaluma iliyokuwa imesahaulika kwakipindi kirefu, shule itasimamia pia zoezi la upatikanaji wa leseni watakaopenda kwakuzingatia taratibu zilizowekwa na mamlaka kwa mda mfupi zaidi, Piga simu au WhatsApp 0676060228/0743156408 kupata maelezo zaidi.

Huduma zetu zinatolewa kwa gharama nafuu na utahudumiwa wakati wowote na popote ulipo

Fika ofisini kwetu Tunapatikana, Mabibo, Mkabala na lango la NIT na Tegeta, Dar es salaam, Tanzania

Thanks
Contact us ESSENCE DRIVING SCHOOL
FACEBOOK PAGE: Essence Driving School
Call: 0676060228
WHATSAP:0743156408
WEBSITE: www.essencedriving.ac.tz
 
Ada ni Tsh ngapi ili nianze kuandaa kabisa bajeti yangu mwaka mpya wa 2020, maana driving course ndio my new year resolution.
 
Ada zetu ziko tofauti kutokana na aina ya mafunzo unayotaka Mkuu mfano kwa mafunzo ya kutumia gari ya manual gharama ni Tshs. 200,000/-

Kwa mtu anayefahamu kuendesha ila anahitaji ujuzi wa kuendesha kwa kuzingatia kanuni zilizowekwa na kwa kutegemea na aina ya barabara n.k na kupata dozi nzuri ya nadharia ikiwemo sheria za barabarani, alama, michoro ya barabarani, ufundi wa awali katika gari, udereva wa kujihami, huduma ya kwanza n.k gharama itakuwa Tshs. 100,000/-

Kuna wanaopenda kupata ujuzi pia wa kujua namna bora ya kuendesha gari za automatic ili kuepuka mazoea yaliyozoeleka ya kuweka gear rever kwenye D na kuanza kukanyaga mafuta na breki tu ziko mbinu kadhaa za kuzingatia ili kuweza kuendesha kwa umahiri mkubwa gharama yake ni Tshs. 225,000/-

Mafunzo ya darasa la kumfuata mtu aliko na kumfundisha kulekule gharama yake ni Tshs 340,000/-

Mafunzo ya peke yako kwenye gari na mwalimu tu kwa wale wanaotaka kufundishwa peke yao hii inasaidia zaidi mwanafunzi kupata mda mwingi wa kuelekezwa na mwalimu mda wote wawapo barabarani na kumpa mwanafunzi fursa ya kuuliza maswali kadri awezavyo gharama yake ni Tshs. 270,000/-

Hizo ni baadhi tu huduma tunazotowa, kwa maelezo zaidi unaweza kutupigia simu ktk namba tulizoweka hapo juu au kutembelea tovuti yetu www.excellencedriving.ac.tz au kufika makao makuu ya ofisi zetu Mabibo, Dar Es Salaam karibu na Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji
 
UDEREVA WA KUJIHAMI

KUTOKA HOME OF EXCELLENCE DRIVING SCHOOL

Imeandikwa na Mr. Manala Tabu Mbumba, Mhadhiri Msaidizi na Mshauri wa Magari-Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)

Home of Excellence Driving School inatoa huduma bora kabisa za udereva pamoja na kusaidia upatikanaji wa leseni kwa wanafunzi wake watakaohitaji kwa kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka kwa mda mfupi.

Huduma zetu hutolewa kwa gharama nafuu sana.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0676060228/0743156408 au fika katika ofisi zetu zilizoko Mabibo mkabala na lango kuu-NIT, Mabibo Road, Dar es salaam, Tanzania

Haitoshi kujifikiria kwamba kila wakati unaheshimu sheria za usalama barabarani, bila kutekeleza dhana ya udereva wa kujihami ambao ni udereva wakutumia akili ili kuepusha ajali.

Falsafa ya udereva wa aina hii inamfanya dereva wakati wote aendeshe gari kwa kutambua athari zinazoweza kujitokeza na mbinu mathubuti za uzuiaji wa athari hizo
Kwa maneno mengine, udereva wa kujihami unakamilisha na mambo makuu matano kama yanavyoonekana hapa chini

1. Kuangalia
Hii inamkumbusha dereva kila wakati kabla hajaanza kuendesha lazima aangalie mbele, pembezoni na nyuma ili kumuwezesha kuwa na picha halisi ya hali ya barabara na kuipeleka kwenye akili kwa ajili ya upangaji, uamuzi na utekelezaji, uangaliaji huu pia unahusisha ukaguzi unaokubalika wa gari analoliendesha na vifaa mbalimbali vinavyotakiwa kuwemo kisheria

2. Kutambua
Kipengele hiki kinamtaka dereva kuwa na uwezo wa kuzing'amua hatari zote na jinsi yakuchukua hatua iwapo zitatokea, mfano umetambua mbele kuna watoto wa shule wapo kandokando ya barabara inapashwa utambue silka au tabia ya watoto kutokuwa waangalifu sana ili uweze kuwa na tahadhali

3. Kutabiri
Hapa sana tunamkumbusha dereva kujiuliza kinachoweza kutokea kutokana na hatari ulizoweza kutambua mfano pale ulipotambua kuna watoto wa shule hivyo utatabiri kuwa wanaweza kuvuka barabara bila kuangalia magari vizuri.

Hivyo, unapashwa wakati wote kutabiri maeneo yote ya hatari kwa kutumia macho yako vizuri

4. Kuamua
Dereva anayejihami daima anatakiwa kutoa maamuzi sahihi na ya haraka, kwani kuchelewesha kwa maamuzi yaweza kuleta madhara na pengine kupelekea ajali mbaya. Hivyo, mara baada tu yakutafakari hatua mbalimbali za kuchukua kama vile kupunguza mwendo, kupiga honi, kuongeza mwendo au kusimama n.k inakubidi kuamua haraka juu ya hatua uliyokusudia.

5. Kutekeleza
Dereva yoyote anapofanya maamuzi daima yanatakiwa kwenda sambamba na utekelezaji, mfano ikiwa umeamua kupunguza mwendo, basi hana budi kupunguza mwendo huo kwani kuendelea kwenda kwa kasi ya juu wakati mazingira hayaruhusu uwekezano wa kupata ajali ni mkubwa.

Aidha mambo hayo dereva anapashwa kuwa nayo akilini ili yaweze kumsaidia katika kutekeleza tendo la kujihami na kuweza kuokoa ajali ambayo angeweza kusababisha au kusababishiwa

Hata hivyo, ukamilifu wa tendo hili lakujihami huwa na mbinu mbali mbali zinazoamuriwa na sababu kadhaa ikiwemo mazingira, gari, binadamu n.k.

Cha muhimu dereva anapashwa kujua mazingira yatakayokuwa yanamzunguka kwa wakati husika ili aweze kuja na mbinu sahihi katika kuokoa athari ambazo zingeweza kutokea.

Hapa nitakuonesha mbinu chache tu ambazo naamini zitakuwa msaada kwa kila mmoja wetu

A. Kama kuna gari lingine mbele yako
Uendeshapo gari na mbele lipo jingine ikatokea kwa ghafla dereva aliye mbele yako anasimama, katika kujihami unapaswa kukumbuka kuwa kila mara uendeshapo gari acha nafasi ya kutosha kati yako na aliye mbele yako (tafiti nyingi zinakadiria umbali wa mita 7) na kila wakati unapaswa kufikiria kuwa mwenzako anaweza kusimama ghafla bila kuonesha ishara yeyote kwa hiyo kaa umbali utakaokuwezesha kuona tairi za nyuma za gari lililo mbele yako daima

B. Umbali wa kusimama
unapashwa kuelewa tu kuwa hakuna gari linaloweza kusimama papo hapo kwa hiyo unapashwa kutembea mwendo ambao kwako utakupa urahisi wakuweza kusimama kwa wakati kunapokuwa na dharura yeyote aidha unapotaka kusimama kamwe usishike breki za ghafla kwani zaweza kuyumbisha gari lako nakupelekea athari zingine zisizo tarajiwa badala yake anza kujiandaa katika umbali unaokubalika ili usilete athari kwa watumiaji wengine wa barabara

C. Kwa gari lililo nyuma
Uendeshapo gari lako daima kuwa msaada wa dereva aliye nyuma yako kwa kutoa ishara kwa kila hatua ya kitendo unachofanya.

Zingatia kutoa ishara katika umbali unaokubalika kumfanya aweze kuchukua hatua pia bila kuleta athari zozote.

Mfano unapotaka kusimama au unakaribia kwenye taa na unahisi kabisa muda wa taa ya kukusimamisha inakaribia kuwaka anza kukanyaga breki zako taratibu na uhakikishe taa za nyuma za breki zinawaka na kama haziwaki unashauriwa utumie mkono wako wa kulia kwa gari ya kuendeshea kulia mpe ishara ya kwamba utasimama na uhakikishe amekuelewa ndipo uweze kusimama

D. Dereva mwingine kuendesha upande wako

Inapotokea dereva anayekuja anaendesha upande wako kwasababu anazozijua yeye labda amelewa, uchovu n.k kitu ambacho kinaweza kupelekea ajali ya uso kwa uso unashauriwa kukaa kushoto zaidi na iwapo dereva huyo amevuka msitari wa katikati ya barabara, jaribu kumpa tahadhali kwa kumpigia honi.

Na kutegemea na hali utakayomuona unashauriwa kupunguza sana mwendo na kamwe usiende kulia maana anaweza kushituka na kuleta madhara makubwa cha muhimu ikiwezekana toka nje kabisa ya barabara kama ni salama

E. Magari kwenye njia panda
Hii ni miongoni mwa sehemu hatari sana, aina ya njia hizi huongozwa na mifumo tofauti tofauti ya mawasiliano mfano alama, taa na zingine haziongozwi na chochote.

Daima unapokaribia njia panda ya aina yoyote kati ya hizo tatu nilizokutajia hapo na ukaona gari jingine linakuja upande mwingine kwa kasi na pengine kuna alama ya kusimama lakini hasimami au kuna taa nyekundu inawaka na hasimami inakupasa upunguze mwendo zaidi huku ukiangalia huku na huku na kutoa ishara ya gari iliyoko nyuma na ikiwezekana simama kumpisha uliyeona anaweza kuhatarisha hali ya barabara

Kwa ujumla katika njia za panda yeyote unapopita unashauriwa kuangalia pande zote na kujiridhisha kama ni salama ndo uendelee na safari.

Kamwe usigombee njia utapita tu pale itakapokuwa salama na usijaribu kabsa kushindania njia na dereva mwingine kuwa na subira ktk kila jambo labda kwasababu za kiusalama tu.

F. Gari linalotaka kukupita
Unashauriwa kuangalia magari yajayo mbele yako, punguza mwendo wako na ubane zaidi kushoto kisha toa ishara yakuruhusu gari linalokupita kama ni salama na unaporuhusu lipite basi usije kubadilisha tena maamuzi ukaanza ushindani

G. Kuovertake
kwanza hakikisha uko umbali unaotakiwa kwa maana unaweza kuziona tairi za nyuma za gari unalotaka kulipita.

Ukiwa bado hujaamua kupita angalia pande zote kujiridhisha hakuna gari mbele inayoweza kuzuia wewe kupita lakini pia tumia vioo vyako vizuri kuangalia kama hakuna gari nyuma yako inayoonesha dalili ya kupita kisha toa ishara yakuomba kulipita gari na mbele yako na hakikisha limekuruhusu kisha utafakari mwendo wako na uwezo wa gari lako.

Kama unaweza kulipita gari la mbele yako kisha hakikisha alama za barabarani zinakuruhusu kufanya hivyo baada ya kujiridhisha kama ni salama unaruhusiwa sasa kuhamia upande wa kulia kwa mwendo mkubwa zaidi ya gari unalotaka kulipita na mara baada ya kupita hakikisha unaonesha ishara yakuanza kurudi wakati huo ukitumia kioo cha kushoto kuangalia hilo mpaka uweze kuona tairi zake za mbele ndo unaweza kurudi upande wako.

Ndugu zangu, ziko mbinu mbalimbali za kujifunza katika mada hii muhimu ambazo madereva wengi wameonekana kushindwa kuzitumia mbinu hizi ama kwa kuzipuuza ama kutozijua na matokeo yake ajali za barabarani zimeendelea kuathiri maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine, kitendo kinachorudisha nyumba dhima ya Taifa letu kila siku.

Mimi napenda kutoa rai yangu kwa madereva wa aina zote kuweza kujifunza mbinu mbalimbali katika taasisi zilizotambuliwa na mamlaka katika kutoa huduma hizi ili wote kwa pamoja tuweze kuwa na uelewa na kuweza kutokomeza janga hili kubwa la ajali zinazolikumba taifa letu hasa ikizingatiwa katika vyanzo vikuu vya ajali binadamu ameonekana kuwa chanzo kikubwa sana cha ajali nyingi tunazozishuhudia, hali ambayo tuna uwezo wa kuizuia kwa sisi wenyewe kuamua tu pamoja na mambo mengine ni kufuata taratibu zinazokubalika kisheria zinazoweza kukufanya ukawa dereva na kuepuka njia zisizo rasmi ambazo wengi wamekuwa wakizitumia na kujikuta wakiharibu sifa za madereva nchini.

Inawezekana kufikia lengo la asilimia sifuri za ajali kama hatua madhubuti zitaendelea kuchukuliwa na wadau wote wanaounda mfumo mzima wa usafirishaji na siyo jambo lakuachia serikali kupitia jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani.

Kama una ndugu, jamaa na rafiki ungependa aweze kupata umahiri wakuendesha gari, HOME OF EXCELLENCE DRIVING SCHOOL ipo kwa ajiri yako.

Huduma zetu ni kukuandaa kuwa dereva mahiri na mwenye vigezo kisheria, taaluma iliyokuwa imesahaulika kwa kipindi kirefu, shule itasimamia pia zoezi la upatikanaji wa leseni watakaopenda kwakuzingatia taratibu zilizowekwa na mamlaka kwa mda mfupi zaidi, Piga simu au WhatsApp 0676060228/0743156408 kupata maelezo zaidi.

Huduma zetu zinatolewa kwa gharama nafuu na utahudumiwa wakati wowote na popote ulipo

Fika ofisini kwetu Tunapatikana, Mabibo, Mkabala na lango la NIT, Mabibo Road, Dar es salaam, Tanzania

Thanks

Contact us HOME OF EXCELLENCE DRIVING SCHOOL

FACEBOOK PAGE: Home of Excellence Driving School

Call: 0676060228
WHATSAP:0743156408
WEBSITE: www.excellencedriving.ac.tz
Instagram: homeofexcellencedrivingschool
Tulioko mikoani inakuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamko Serious
Namba zenu hazipatikani hata zikipatikana Hazipokelewi wala kujibiwa.
Nimewatafuta zaidi ya mara TANO kwa namba hii 0764055904
Huenda nyie ni Wababaishaji TU
 
Pole kiongozi, ni bahati mbaya sana unatumia namba ambayo wala hatuitambui. Naomba pitia vizuri uzi wetu au nipigie moja kwa moja kupitia 0765374146
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom