Manala An Academician
Senior Member
- Oct 10, 2016
- 118
- 53
UDEREVA WA KUJIHAMI
KUTOKA HOME OF EXCELLENCE DRIVING SCHOOL
Imeandikwa na Mr. Manala Tabu Mbumba, Mhadhiri Msaidizi na Mshauri wa Magari-Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)
Home of Excellence Driving School inatoa huduma bora kabisa za udereva pamoja na kusaidia upatikanaji wa leseni kwa wanafunzi wake watakaohitaji kwa kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka kwa mda mfupi.
Huduma zetu hutolewa kwa gharama nafuu sana.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0676060228/0743156408 au fika katika ofisi zetu zilizoko Mabibo mkabala na lango kuu-NIT, Mabibo Road, Dar es salaam, Tanzania
Haitoshi kujifikiria kwamba kila wakati unaheshimu sheria za usalama barabarani, bila kutekeleza dhana ya udereva wa kujihami ambao ni udereva wakutumia akili ili kuepusha ajali.
Falsafa ya udereva wa aina hii inamfanya dereva wakati wote aendeshe gari kwa kutambua athari zinazoweza kujitokeza na mbinu mathubuti za uzuiaji wa athari hizo
Kwa maneno mengine, udereva wa kujihami unakamilisha na mambo makuu matano kama yanavyoonekana hapa chini
1. Kuangalia
Hii inamkumbusha dereva kila wakati kabla hajaanza kuendesha lazima aangalie mbele, pembezoni na nyuma ili kumuwezesha kuwa na picha halisi ya hali ya barabara na kuipeleka kwenye akili kwa ajili ya upangaji, uamuzi na utekelezaji, uangaliaji huu pia unahusisha ukaguzi unaokubalika wa gari analoliendesha na vifaa mbalimbali vinavyotakiwa kuwemo kisheria
2. Kutambua
Kipengele hiki kinamtaka dereva kuwa na uwezo wa kuzing'amua hatari zote na jinsi yakuchukua hatua iwapo zitatokea, mfano umetambua mbele kuna watoto wa shule wapo kandokando ya barabara inapashwa utambue silka au tabia ya watoto kutokuwa waangalifu sana ili uweze kuwa na tahadhali
3. Kutabiri
Hapa sana tunamkumbusha dereva kujiuliza kinachoweza kutokea kutokana na hatari ulizoweza kutambua mfano pale ulipotambua kuna watoto wa shule hivyo utatabiri kuwa wanaweza kuvuka barabara bila kuangalia magari vizuri.
Hivyo, unapashwa wakati wote kutabiri maeneo yote ya hatari kwa kutumia macho yako vizuri
4. Kuamua
Dereva anayejihami daima anatakiwa kutoa maamuzi sahihi na ya haraka, kwani kuchelewesha kwa maamuzi yaweza kuleta madhara na pengine kupelekea ajali mbaya. Hivyo, mara baada tu yakutafakari hatua mbalimbali za kuchukua kama vile kupunguza mwendo, kupiga honi, kuongeza mwendo au kusimama n.k inakubidi kuamua haraka juu ya hatua uliyokusudia.
5. Kutekeleza
Dereva yoyote anapofanya maamuzi daima yanatakiwa kwenda sambamba na utekelezaji, mfano ikiwa umeamua kupunguza mwendo, basi hana budi kupunguza mwendo huo kwani kuendelea kwenda kwa kasi ya juu wakati mazingira hayaruhusu uwekezano wa kupata ajali ni mkubwa.
Aidha mambo hayo dereva anapashwa kuwa nayo akilini ili yaweze kumsaidia katika kutekeleza tendo la kujihami na kuweza kuokoa ajali ambayo angeweza kusababisha au kusababishiwa
Hata hivyo, ukamilifu wa tendo hili lakujihami huwa na mbinu mbali mbali zinazoamuriwa na sababu kadhaa ikiwemo mazingira, gari, binadamu n.k.
Cha muhimu dereva anapashwa kujua mazingira yatakayokuwa yanamzunguka kwa wakati husika ili aweze kuja na mbinu sahihi katika kuokoa athari ambazo zingeweza kutokea.
Hapa nitakuonesha mbinu chache tu ambazo naamini zitakuwa msaada kwa kila mmoja wetu
A. Kama kuna gari lingine mbele yako
Uendeshapo gari na mbele lipo jingine ikatokea kwa ghafla dereva aliye mbele yako anasimama, katika kujihami unapaswa kukumbuka kuwa kila mara uendeshapo gari acha nafasi ya kutosha kati yako na aliye mbele yako (tafiti nyingi zinakadiria umbali wa mita 7) na kila wakati unapaswa kufikiria kuwa mwenzako anaweza kusimama ghafla bila kuonesha ishara yeyote kwa hiyo kaa umbali utakaokuwezesha kuona tairi za nyuma za gari lililo mbele yako daima
B. Umbali wa kusimama
unapashwa kuelewa tu kuwa hakuna gari linaloweza kusimama papo hapo kwa hiyo unapashwa kutembea mwendo ambao kwako utakupa urahisi wakuweza kusimama kwa wakati kunapokuwa na dharura yeyote aidha unapotaka kusimama kamwe usishike breki za ghafla kwani zaweza kuyumbisha gari lako nakupelekea athari zingine zisizo tarajiwa badala yake anza kujiandaa katika umbali unaokubalika ili usilete athari kwa watumiaji wengine wa barabara
C. Kwa gari lililo nyuma
Uendeshapo gari lako daima kuwa msaada wa dereva aliye nyuma yako kwa kutoa ishara kwa kila hatua ya kitendo unachofanya.
Zingatia kutoa ishara katika umbali unaokubalika kumfanya aweze kuchukua hatua pia bila kuleta athari zozote.
Mfano unapotaka kusimama au unakaribia kwenye taa na unahisi kabisa muda wa taa ya kukusimamisha inakaribia kuwaka anza kukanyaga breki zako taratibu na uhakikishe taa za nyuma za breki zinawaka na kama haziwaki unashauriwa utumie mkono wako wa kulia kwa gari ya kuendeshea kulia mpe ishara ya kwamba utasimama na uhakikishe amekuelewa ndipo uweze kusimama
D. Dereva mwingine kuendesha upande wako
Inapotokea dereva anayekuja anaendesha upande wako kwasababu anazozijua yeye labda amelewa, uchovu n.k kitu ambacho kinaweza kupelekea ajali ya uso kwa uso unashauriwa kukaa kushoto zaidi na iwapo dereva huyo amevuka msitari wa katikati ya barabara, jaribu kumpa tahadhali kwa kumpigia honi.
Na kutegemea na hali utakayomuona unashauriwa kupunguza sana mwendo na kamwe usiende kulia maana anaweza kushituka na kuleta madhara makubwa cha muhimu ikiwezekana toka nje kabisa ya barabara kama ni salama
E. Magari kwenye njia panda
Hii ni miongoni mwa sehemu hatari sana, aina ya njia hizi huongozwa na mifumo tofauti tofauti ya mawasiliano mfano alama, taa na zingine haziongozwi na chochote.
Daima unapokaribia njia panda ya aina yoyote kati ya hizo tatu nilizokutajia hapo na ukaona gari jingine linakuja upande mwingine kwa kasi na pengine kuna alama ya kusimama lakini hasimami au kuna taa nyekundu inawaka na hasimami inakupasa upunguze mwendo zaidi huku ukiangalia huku na huku na kutoa ishara ya gari iliyoko nyuma na ikiwezekana simama kumpisha uliyeona anaweza kuhatarisha hali ya barabara
Kwa ujumla katika njia za panda yeyote unapopita unashauriwa kuangalia pande zote na kujiridhisha kama ni salama ndo uendelee na safari.
Kamwe usigombee njia utapita tu pale itakapokuwa salama na usijaribu kabsa kushindania njia na dereva mwingine kuwa na subira ktk kila jambo labda kwasababu za kiusalama tu.
F. Gari linalotaka kukupita
Unashauriwa kuangalia magari yajayo mbele yako, punguza mwendo wako na ubane zaidi kushoto kisha toa ishara yakuruhusu gari linalokupita kama ni salama na unaporuhusu lipite basi usije kubadilisha tena maamuzi ukaanza ushindani
G. Kuovertake
kwanza hakikisha uko umbali unaotakiwa kwa maana unaweza kuziona tairi za nyuma za gari unalotaka kulipita.
Ukiwa bado hujaamua kupita angalia pande zote kujiridhisha hakuna gari mbele inayoweza kuzuia wewe kupita lakini pia tumia vioo vyako vizuri kuangalia kama hakuna gari nyuma yako inayoonesha dalili ya kupita kisha toa ishara yakuomba kulipita gari na mbele yako na hakikisha limekuruhusu kisha utafakari mwendo wako na uwezo wa gari lako.
Kama unaweza kulipita gari la mbele yako kisha hakikisha alama za barabarani zinakuruhusu kufanya hivyo baada ya kujiridhisha kama ni salama unaruhusiwa sasa kuhamia upande wa kulia kwa mwendo mkubwa zaidi ya gari unalotaka kulipita na mara baada ya kupita hakikisha unaonesha ishara yakuanza kurudi wakati huo ukitumia kioo cha kushoto kuangalia hilo mpaka uweze kuona tairi zake za mbele ndo unaweza kurudi upande wako.
Ndugu zangu, ziko mbinu mbalimbali za kujifunza katika mada hii muhimu ambazo madereva wengi wameonekana kushindwa kuzitumia mbinu hizi ama kwa kuzipuuza ama kutozijua na matokeo yake ajali za barabarani zimeendelea kuathiri maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine, kitendo kinachorudisha nyumba dhima ya Taifa letu kila siku.
Mimi napenda kutoa rai yangu kwa madereva wa aina zote kuweza kujifunza mbinu mbalimbali katika taasisi zilizotambuliwa na mamlaka katika kutoa huduma hizi ili wote kwa pamoja tuweze kuwa na uelewa na kuweza kutokomeza janga hili kubwa la ajali zinazolikumba taifa letu hasa ikizingatiwa katika vyanzo vikuu vya ajali binadamu ameonekana kuwa chanzo kikubwa sana cha ajali nyingi tunazozishuhudia, hali ambayo tuna uwezo wa kuizuia kwa sisi wenyewe kuamua tu pamoja na mambo mengine ni kufuata taratibu zinazokubalika kisheria zinazoweza kukufanya ukawa dereva na kuepuka njia zisizo rasmi ambazo wengi wamekuwa wakizitumia na kujikuta wakiharibu sifa za madereva nchini.
Inawezekana kufikia lengo la asilimia sifuri za ajali kama hatua madhubuti zitaendelea kuchukuliwa na wadau wote wanaounda mfumo mzima wa usafirishaji na siyo jambo lakuachia serikali kupitia jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani.
Kama una ndugu, jamaa na rafiki ungependa aweze kupata umahiri wakuendesha gari, HOME OF EXCELLENCE DRIVING SCHOOL ipo kwa ajiri yako.
Huduma zetu ni kukuandaa kuwa dereva mahiri na mwenye vigezo kisheria, taaluma iliyokuwa imesahaulika kwa kipindi kirefu, shule itasimamia pia zoezi la upatikanaji wa leseni watakaopenda kwakuzingatia taratibu zilizowekwa na mamlaka kwa mda mfupi zaidi, Piga simu au WhatsApp 0676060228/0743156408 kupata maelezo zaidi.
Huduma zetu zinatolewa kwa gharama nafuu na utahudumiwa wakati wowote na popote ulipo
Fika ofisini kwetu Tunapatikana, Mabibo, Mkabala na lango la NIT, Mabibo Road, Dar es salaam, Tanzania
Thanks
Contact us HOME OF EXCELLENCE DRIVING SCHOOL
FACEBOOK PAGE: Home of Excellence Driving School
Call: 0676060228
WHATSAP:0743156408
WEBSITE: www.excellencedriving.ac.tz
Instagram: homeofexcellencedrivingschool