kwa Hotuba ya Mhe, Membe jioni hii bungeni Anastahiri Kuoteshwa 2015 Magogoni

kimeta cha ufisadi

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
398
70
Muda mfupi ulio pita mhe, Membe amemaliza kutoa mchango wa wizara yake ulio tokana na Taarifa ya kamati ya mhe, Lowasa. Maneno aliyo kuwa akiyatumia mhe, Membe ni ya kidiplomasia ya khali ya juu imewagusa wabunge, wananchi wa kawaida na mataifa ya majirani zetu. Gooooo Membeeeee
 
Muda mfupi ulio pita mhe, Membe amemaliza kutoa mchango wa wizara yake ulio tokana na Taarifa ya kamati ya mhe, Lowasa. Maneno aliyo kuwa akiyatumia mhe, Membe ni ya kidiplomasia ya khali ya juu imewagusa wabunge, wananchi wa kawaida na mataifa ya majirani zetu. Gooooo Membeeeee

Tujulishe alichokisema.
 
Endapo uchaguzi utakuwa ni kati ya Dr Slaa, Lowassa na Membe, basi Membe atakuwa ni chaguo bora zaidi, nitamuunga mkono.
 
hiyo ndio tanzania na watu wake

mleta mada keshajua kwamba hadi majirani wameguswa, hata kabla 80% ya wachangiaji humu hawaijui hiyo hotuba

Bongo = mbayuwayu
 
muda mfupi ulio
pita mhe, membe amemaliza kutoa mchango wa wizara yake ulio tokana na
taarifa ya kamati ya mhe, lowasa. Maneno aliyo kuwa akiyatumia mhe,
membe ni ya kidiplomasia ya khali ya juu imewagusa wabunge, wananchi wa
kawaida na mataifa ya majirani zetu. Gooooo membeeeee

membe hafai kuwa rais mbona kwenye mgogoro wa gesi mtwara hakutumia diplomasia ilihali na yeye ni mbunge wa mikoa ya kusini
 
kimeta cha ufisadi you must be joking. Membe katoa hutuba ambayo imemalizika muda si mrefu kwa maelezo yako. Saa 18:35 (ndani ya dakika 10) umeshafanya tafiti kwa wananchi wa kawaida, wananchi wengine watu wa kimataifa na mataifa ya nje na ukaona kuwa wote wameguswa na kumkubali! Duuh wewe kiboko. Yaani ndani ya huo muda mfupi watu wameshatafakari na kuitolea majibu. Kwa kasi hiyo ya utafiti soon Tanzania tutakuwa level zingine.
Wakati mwingine ni busara zaidi kujipa muda wa kutafakari jambo kwa undani kwanza. Ebu tueleze kasema nini hasa. Sina tatizo na alichokisema ila ninawasiwasi kwa uharaka wa utafiti wako uliochukua si zaidi ya dakika 10 lakini coverage yake babu kubwa. Kwa mtu kama mimi nisiyeendeshwa na ushabiki naweza kukuchukulia kama Pro-Membe kumbe pengine unahoja.
Lakini hatupeleke mtu ikulu kwasababu ya kuwa na hotuba nzuri. Vp vigezo vya mtu kuchaguliwa na kuwekwa Ikulu! Tusimamie hivyo
 
Last edited by a moderator:
Akili ndogo sana ndiyo inayoweza kusema Membe anafaa kuingia magogoni. Ni akili ndogo sana inaweza kusema maneno ya kipumbavu aliyoyazungumza membe bungeni ni ya kidiplomasia
 
Membe mchovu tu.

Aliharibu kuongea kwenye mahojiano na BBC kuhusu wafanyakazi wa serikali ya Tanzania kuhusika kuuzia silaha waasi wa Congo, mpaka balozi Mahiga wakati huo akiwa UN akaokoa jahazi.

Kama mnaanza kampeni semeni tu, lakini msitake kutufanya tuamini kwamba Membe ni boonge la diplomat.
 
membe hafai kuwa rais mbona kwenye mgogoro wa gesi mtwara hakutumia diplomasia ilihali na yeye ni mbunge wa mikoa ya kusini

Ulitaka afanye nini?Membe anaamini katika Tanzania moja,na anajiona Mtanzania kwanza kabla ya Kanda yake,hakurupuki!!

Kwa kuwa Membe ni waziri, maoni yake juu ya gesi ilikuwa ni ndani ya Baraza la Mawaziri,na kutokea huko,uamuzi ulitangazwa na Rais,Waziri Mkuu na Waziri husika(Muhongo).
 
Back
Top Bottom