Kwa Hotuba ya Kagera, ni bora angekaa kimya

Sidhani kama atatokea mwenye KIBURI kama FARAO.

Sidhani kama atatokea DICTATOR kama Adolf Hitler

Sidhani kama atatokea mwenye DHARAU kama Idd Amini

Lakini kwa maajabu ya Mungu yanayoshangaza..
Leo hii wote hao ni MAVUMBI.

Huyu ni Muigizaji walishapita wale Origional.

God's time will tell.

Sasa naanza kuelewa kwa nini Lema aliota ile ndoto
 
Kwa hotuba zake mbili alizozitoa hivi karibuni mkoani Kagera..na kwa jinsi ninavyo wafahamu watu wa mkoa ule jinsi wanavyopenda ku'read between lines' na uwa hawasahau vitu muhimu kirahisi...hasa kwa kauli ya 'mwafa' (kwa lugha ya Kiswahili cha mtaani tunaweza kusema 'imekula kwenu' tusubiri uchaguzi ujao hata kama akiwapa meli nawahakikishieni wadau 'hapati kitu' unless asimame tena jukwaani aombe msamaha jambo ninalofahamu hawezi diriki kulifanya .Waathirika hawakutakiwa kuambiwa maneno ya kejeli yasiyo na uthibitisho wowote kwa mfano'kuna watu wamebomoa nyumba zao kwa kutegemea kufidiwa.... kawaambieni hao wanasiasa wakawajengee mwafa' e.t.c. Wananchi walihitaji maneno ya matumaini.... Wasiowajua wanakagera wamtafute Mbunge Kamala awape mchapo wa yaliyomkuta hata bada ya JK kuingilia kati katika uchaguzi fulani wa ubunge.
uko nyuma...Alileta maneno ya dharua....walichokifanya wananchi waliona bora wampe 'Assumpta' japo wakijua nae hafai kuliko mtu wa kauli mbovu....
Sijapenda Admin ulivyofanya..hii post ilikuwa inajitegemea kumbuka sio watu woote wanapenda kusoma mathread marefuuuuu...mpaka aje kuona huu ujumbe naomba uutendee haki na urudishe post yake ijitegemee kama ilivyokuwa mwanzo
 
Kwa kauli kama hizi za Rais inaweza kuwa ndo maana hata mvua itakuwa chache ili kuepusha majanga, maana mkuu a naangalia kijani. Imagine ikitokea mafuriko yakaharibu mazao lakini aridhi ikabaki kijani, wahanga wanapata misaada? I am totally confused. Hivi hakuna sheria ya kulazimisha aandkiwe hotuba na asome kilichomo. Ni dhahiri mwaka mpya umeanza vibaya huko kagera.
 
Wewe bwana wewe! Tabia za wachache katika jamii zisifanywe kuwa jambo la jumla. Ugumu huu wa maisha huko vijijini watu wavivu wameshapotea kwa vile ile tabia ya kijamaa ilipotea siku nyingi hivyo ili ule lazima ufanye kazi kwa maana lazima ulime. Kama katika kundi la watu elfu ukikuta watano ni wavivu hao hawawezi kuleta njaa katika wilaya nzima.
Unataka kumaanisha wilaya ya Misenyi ndio wavivu kuliko wote Tanzania hii ndio maana wana njaa?
Anyway labda ni mtizamo wenu, ila rais kuwa na mtizamo huo ni mashaka kama viatu hivyo vinamtosha.
Naidahamu Tanzania, naelewa vema mkuu, kama huna mtazamo huo ni wewe, lkn kuna watu hawatambui kuwa niwajibu wao kufanya kazi na msaada ni just a favour. Kuna vitu tumegeuza ni right zetu hata kulalamika serkali haifanyi lakini sio wajibu wa serkali. Nadhani tunahitaji kuwa liberated kifikra maana hata tukeshe tutabishana tu ila tatizo ni jinsi tu tunavyoconceive mambo tu. Ila maadam kawapa live, miaka mitano mingi watu watajiongeza wakati wakisubiri anayeconceive mambo kamwa watakavyo wao, aidha wanaweza kubadilika in a process wakiona umuhimu wa kubadilika
 
Mkuu umeandika maneno meengi yasiyo na mantiki. Hivi unadhani yeye anafahamu hizo theory? Unadhani alivyokua anazungumza, alilenga kufata theory yako hiyo uliyotaja? Lumumba mna mambo sana
.
Naona hata theories zenyewe hujazielewa.
Halafu unataja Lumumba.
Kuna uhusiano gani?
Rubish!
 
Mheshimiwa Rais kweli anafuatilia habari za ulimwengu huu!? .., anasema nini!? Kwamba hajawahi kuona serikali ikiwajengea wananchi wake makazi kisa tetemeko.., OMG..., anatazama habari za kimataifa kweli..,!?

.., amesahau mafuriko ya juzi huko Indonesia..,!? Serikali ya Indonesia ilitoa ahafi ya kuwajengea watu (waathitirika) makazi yao yote bila kubagua!

Wakati sisi tunatafuna rambi rambi za wahanga wa tetemeko kule KGR zilitolewa na wananchi wa kawaida, wadau na wahisani.., wananchi hadi sasa wanalala na kushinda nje.., (tunajenga majengo ya serikali na miundombinu yake) na viongozi wetu wanapiga nyundo za utosi kwenye vidonda vyetu..,

.., nchi ya INDONESIA ilisema wazi, inakwenda kuwajengea makazi ya kuishi wananchi wake wote waliokumbwa na mafuriko ya novemba mwaka huu, yalisemwa na Indonesia's disaster-management agency (BNPD), vijiji 12 katika wilaya 5 vyenye wakazi 60,000 vimeathirika.

Leo kule KGR, (02-01-2017) mheshimiwa Rais anasema hajawahi kuona serikali yoyote ikiwajengea majumba waathitirika wake kutokana na tetemeko (janga la asili).., aisee., nimesikitika sana., najiuliza, mheshimiwa kweli anafuatilia habari za kimataifa!!?

Sasa tujibu maswali yetu.., zile pesa za michango kutoka kwa wahisani, mashirika, taasisi, watanzania kwenda kwenye mfuko wa maafa zilikuwa na lengo la kujenga miundombinu ya serikali tu.., bila kuwasaidia wahanga katika kusimama upya!!?

Tujifunze mazuri kutoka kwa wenzetu hawa.., watu kwanza.., majengo na vitu baadae.., kipaumbele ni watu (kwao) siyo vitu (kwetu)...
SA UTAMJENGEAJE MTU ALIYEVUNJA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE ILI SERIKALI IJE KUMJENGEA NYUMBA NZIMA, NA UTAJUAJE YUPI NYUMBA YAKE KWELI ILIDONDOKA KWA TETEMEKO AU ILIVUNJWA NA MTU MWENYEWE????
 
Yuko sahihi kabisa... he need not deceive the people. Tatizo mnapenda pleasing but empty words...
We! unasema yuko sahihi?

are you crazy?
fedha tulizochanga Sisi wahisani, kutoka ndani na nje ya nchi, mashirika, taasisi watu binafsi hadi mataifa zifanye kazi ambayo haikukusudiwa halafu uje hapa unabana pua eti "yuko sahihi" (?)
huna utu, japo mimi siyo mmoja wao wala siyo mwana kagerela ila watu wa dizaini kama yako siwapendi!
 
Tunajua anachuki na Kagera. Nasema anajisumbu yeye sio Mungu, hata kodi asije kuchukua.
 
rais amesema kuhusu ndugu zetu wa kagera na tumemsikia. tunaomba sasa awaruhusu na wengine wenye uchungu wa kusaidia wananchi wa kagera nao waende kagera nao wafanye mkutano wa hadhara waongee na wana kagera waone namna ya kuwasaidia. tunachoomba rais asiwazuie kufanya hivo.....
 
Wewe nivoj.sued unawadanganya watu. Unafundisha chuo gani? Hiyo Research Philosophy yako maelezo yako ni potofu. Hii ndio tabu ya kuwa na vyuo vinavyookoteza walimu. Hiyo Postitivism Vs Phenomenology / Constructionism iko hivi: Wale wa upande wa Positivism wanaamini kuwa maana au ukweli wa kitu ni mmoja dunia nzima. Yaani ukweli wa ulaya ni ukweli wa Tanzania pia. Hiyo inaitwa 'generalization'. Wale wa upande wa Phenomenology / Constructionism wanaamini kwamba ukweli au maana ya kitu fulani huendana na mazingira husika na maana halisi ya kitu imo kwa watu husika wa mazingira husikana hivyo hakuna maana moja ya kitu kwa dunia nzima na kwa watu wote. Kwamba anayeujua ukweli wa jambo husika ni yule anayekumbana na jambo husika au ni yule anayeishi na jambo husika. Kwa mfano, anayejua maumivu ya tetemeko ni yule aliyekumbwa na tetemeko. Pia upande huu unasema kinachoitwa kijiko Japani chaweza kuwa na maana nyingine maeneo mengine. Yaani kuna uwezekano wa maana ya kitu kulingana na mazingira. Kwa mfano neno au jina linalotumika eneo fulani likiwa na maana nzuri tui laweza kuwa ni tusi likitumika eneo au mazingira ya watu wa eneo fulani. Kwa hiyo kuwa Mwana sayansi hakumaanishi uwe na uhuru wa kutumia misamiati ya kisayansi ambayo ni chukizo au maudhi kwa jamii nyingine. Sasa kama wewe umeipenda Sayansi yako kwa nini uombe uongozi kwa watu ambao si wote ni wana sayansi? kwa nini uombe uongozi wa kijamii ambao unadai kufuata mila, desturi na tamaduni zinazoheshimu utu hata kwa kauli tu? Kama unaona huwezi kuzingatia lugha ya kijamii yenye utu ndani yake kwa nini usibaki kwenye mazingira ya kisayansi ambayo yanakuruhusu kutamta maneno na majina ya kisayansi kama yalivyo? Ukiingia kwenye anga zetu za kijamii tunataka utumie tafsida. Huwezi kuitisha mkutano wa hadhara ambao baba, mama na watoto wanahudhuria halafu unatamka jina la sehemu ya siri ya binadamu kama ilivyo eti tu wewe ni mwana sayansi. Hutufai hata kidogo!
 
Kwa hotuba hiyo tuseme ukweli. Bila kumung'unya maneno kwamba pombe hapo ameteleza
Hayo c maneno ya kuongea Rais alieshika dhamana ya nchi ametumia hasira katika hotuba yake au kwasababu jimbo lile limechukuliwa na upinzani lkn hata hivyo yeye ni rais wa wote hapaswi kuongea hivyo
 
(i) "Waambie hao wanasiasa wawajengee hizo nyumba zenu wenyewe.. "

(ii) "kwa hiyo kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe..,"

(iii) "jukumu la serikali ni kurejesha miundombinu ya serikali, siyo kujenga nyumba za wananchi"

(iv) "asitokee mtu kuwadanganya kwamba serikali itagawa chakula., hauwezi kugawa chakula ardhi ni ya kijani"

(v) "sasa mkuu wa wilaya nataka nikueleze hapa.., sitaleta chakula hapa, hakuna chakula cha serikali, serikali haina shamba "

(vi) " nimekuja kuwapa ujumbe huu, na mwenye kusikia asikie"

>>>> Hayo ni ya maneno ya 'FARAJA' kutoka kwa Rais John Pombe Magufuli akiwa Kagera leo.., una maoni yapi katika kauli hizo za Rais wa watanzania wakiwepo wale wahanga qa tetemeko kule Kagera!!?

Binafsi; sina deni hata chembe.., hii dhambi haiwezi kunitafuna (ya kuichagua CCM).., siyo mmoja kati ya wale ambao walichagua CCM.., siyo mmoja wapo kabisa!
Faraja za raisi ni njema maana hakumumunya maneno wala kuyapamba. Wenye masikio Kagera wamesikia na ujumbe umefika. It was about time the tough in Kagera to tighten their boots and get going.
 
Sidhani kama atatokea mwenye KIBURI kama FARAO.

Sidhani kama atatokea DICTATOR kama Adolf Hitler

Sidhani kama atatokea mwenye DHARAU kama Idd Amini

Lakini kwa maajabu ya Mungu yanayoshangaza..
Leo hii wote hao ni MAVUMBI.

Huyu ni Muigizaji walishapita wale Origional.

God's time will tell.
mwaka huu tumepata SAULI ....wetu wa kutukandamiza .....

siku hizi ongezeko la wanaobadilisha channel wakimuona linaongezeka .....,bora kuangalia muziki kuliko kukereka roho.
 
Faraja za raisi ni njema maana hakumumunya maneno wala kuyapamba. Wenye masikio Kagera wamesikia na ujumbe umefika. It was about time the tough in Kagera to tighten their boots and get going.
huu unjema wa rais uko wapi? hivi lengo kuu la serikali ni nini? kwa nini rambirambi zijenge miundombinu ya umma na sio kuwahudumia wahanga moja kwa moja?
 
Hivi serikali ya Uhuru Kenyata iliyotoa chakula na tents kwa wahanga Kagera ina shamba na kiwanda? Kuna jinsi ya kufikisha ujumbe kwa wananchi bila ya kuwakatisha tamaa. Tunapoenda misibani na kutoa pole ahimaanishi tunaenda kurudisha uhai wa mpenzi wao. Ni kuwafariji tu wafiwa. Kwa hili sioni kama wananchi wamefarijiwa na hotuba hii.
 
Hakuana taifa lolote duniani lililo endelea kwakua na kiongozi mdanganyifu,mzembe,asie na msimamo hakika tulikua tupo ktk shimo, tulitaabika mda mlefu sana na ukweli kua wakagera wameumizwa na hizi kauli, zimewachoma na kupoteza nuru zao juu ya maisha ya hapoa awali lkn lazima watanzania tujue kua huyu jamaa kaja kwaajili ya kulekebisha makosa yanayo onekana na yale tusio yaona,tujiulize kwanini yeye aseme hayo alio yasema nini kaona, kachunguza au hakuchunguza adi atoe kauli hizo je kiongozi wetu hua anatabia ya kukulupuka? je kiongozi wetu ana washauli walio na uzoefu? bila shaka yote aliyaona na aliyafanyia kazi mimi napenda kua na kiongozi alie simama na kuamini kauli zake.
 
Back
Top Bottom