Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 322
- 645
KIGWANGALA alitoa hoja ya namna anavyodhani tunaweza kukabiliana na corona kwa sasa. Kwenye hoja zake alisema haoni hata umuhimu wa tanuru la kujivukiza pale hospitali ya Mhimbili.
Wakati wa uchangiaji wa hoja ya Mhe Kigwangala wengi walimshambulia personal na kusema kuwa kwa nini hakushauri kwenye baraza? Lakini ukweli kuwa mabaraza yetu hoja zinaenda kwa majorities, ukishauri jambo lisipoungwa na wengi linakuwa limejifia na utalazimika kuwaunga wengi.
Sasa tukija kwenye hoja ya Mhe Rais ya leo juu ya Covid 19, kwanza amesema Tanzania siyo kisiwa. Amesema Kama duniani kote ripoti zinatolewa na kila siku Tanzania ni deshi haipendezi, lazima tujulikane tuko wapi. Akasisitiza kwa kusema ataunda timu ya Wataalamu ambao watafanya utafiti juu ya Covid 19 ili Kama Taifa tuangalie njia ya kwenda nayo.
Kwa statement hii ya Mhe Rais inaonyesha sasa ni wakati wa Tanzania kuungana rasimi na mapambano haya Kama ilivyo duniani kote au kuamua rasimi Kama Taifa kutumia njia zetu kukabiliana na janga hili. Matokeo ya tume ndiyo yatatoa dira ya taifa.
Lakini hata hivyo statement inaonyesha sasa rasimi corona ipo.
Kigwangala angesikilizwa badala ya kumshambulia. Kigwangala alitoa mawazo huru ambayo pengine kwenye baraza hayakusikilizwa akaona ayaseme sasa kwa kuwa habanwi na Uwaziri.