Kwa hizi pesa wanataka wafanye maisha

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Nina vijana 5 ambao nimewapata sehemu mbalimbali kama wadogo zangu. Wawili kutoka JF. Elimu ni kuwa, watatu wana Degree, mmoja Diploma na mwingine Certificate.

Hawa tumeongea mambo kadhaa ya msingi na kuafikiana kuwa niwapatie Mtaji wa Tsh 1,000,000 kila mtu akafanye biashara. Warudishe ndani ya miezi 6 kama ilivyo no riba/interest.

Swali, Nahitaji pia kushauriana nao zaidi. Ni biashara gani mtu anaweza fanya kwa mtaji wa milioni 1? Akapata faida kiasi na kurudisha pesa angalau 200,000 ya deni au 1 point something?

Naombeni muweze wasaidia hawa wadau na kunisaidia mimi pia.maana sina lengo la kupoteza hizo pesa. Naamini kuna watu wenye mawazo chanya. Wawili kati ya hao wanatoka mikoani kuja kuishi Dar. But hiyo million 1 inabaki kuwa ndo Initial Capital. Kila mtu afanye nini?

Kama individual.
 
Umewauliza wanataka kufanya biashara gan?

Wanaingia kwenye partnership watu 3 au kila mmoja ana die alone katka biashara?
 
Nina vijana 5 ambao nmewapata sehemu mbalimbali kama wadogo zangu. Wawili toka JF. elimu ni kuwa watatu wana Degree,Mmoja Diploma na Mwingine Certificate.

Hawa tumeongea mambo kadhaa ya msingi na kuafikiana kuwa niwapatie Mtaji wa Tsh 1,000,000 kila mtu akafanye biashara. Warudishe ndani ya miezi 6. Kama ilivyo No Riba/Interest.

Swali. Nahitaji pia kushauriana nao zaidi. Ni biashara gani mtu anaweza fanya KWA MTAJI WA MIL 1? Akapata faida kiasi na kurudisha pesa angalau 200,000 ya deni au 1 point something?

Naombeni muweze wasaidia hawa wadau na kunisaidia mimi pia.maana sina lengo la kupoteza hizo pesa. Naamini kuna watu wenye mawazo chanya. Wawili kati ya hao wanatoka Mikoani kuja ishi Dar. But hiyo Million 1 inabaki kuwa ndo Initial Capital. Wafanye nini?
Naona mwenye certificate ni wewe hapo! Mkuu.
 
Hugo mwenye certificate nadhani ataiweza hiyo biashara ila hizo degree & diploma sidhani kama wataweza kuitendea haki hiyo initial capital ya m1
 
Biashara ya juice ya miwa ukitega sehemu nzuri unaweza kupata hiyo hela kwa mwezi.

Machine = 500000/=.
Pango = 50000/month.
Umeme = 20000/month.
Glass = 30000.
Ndoo 2 = 4000.
Sahani kubwa mbili = 8000.
Miwa ya kuanzia = 100000/=
Ndimu/limao = 2000.
Kabati dogo = 100000/=
Kisu = 10000.
Freezer used dogo = 150000/=

TOTAL HAPO 97400/=
 
Nazi wazitoe shamba walete mjini, wahakikishe wanawateja tayari mkononi.
Iliki kutoka polini kuleta mjini, watafute wateja kwanza.
Usambazaji wa nyama na samaki mahotelini, watafute wateja wakudumu kwanza na wa uhakika.

Uzuri wote ni wasomi hivyo sio suala gumu kufanya marketing kwenye hotel zote za mijini, sina shaka na lugha ya kibiashara kwao na ile lugha iliyokuja na jahazi.
 

Nimeikuta humuhumu, sina uzoefu nayo natumai itasaidia kupanua wazo la biashara watazotarajia kufanya vijana.

Kila la kheri Guddu.
 
Principle ya Biashara haiko ivo kama hao vijana hawajawahi kufanya biashara ni ngumu sana kurudisha ata robo ya mtaji.

USHAURI wangu kwao na kwako kama kuna ambaye amewahi kufanya biashara fulani kwa muda wa zaidi ya miezi 6 mfululizo kisha akaacha kwa sababu zozote na kwa sasa anataka kuendelea akwa .kua anajua faida na mchanganuo wa hasara MPE MTAJI HARAKA SANA.
Hakuna biashara ya kushauriwa iliyo salama zaidi ya iliyo ndani ya medula yako
 
Kwa mtaji huo tafuta vijana (walio serious na maisha) wa darasa la saba wapange chumba tandale kwa tumbo elfu 15 kwa mwezi wanunue ballo la mitumba watembeze vijiweni, kwenye bar, sokoni na hata kwenye stendi kuu za daladala. Wasomi watakuzingua.
 
Wape wapeleke sadaka kwa Buldoza, Mzee wa Upako, Mlima wa Moto, n.k

Kisha zitadabiwadabiwa!
 
Kila mtu ana maisha yake anajitegemea.si kwamba watafanya pamoja.


Kwa mtaji huo tafuta vijana (walio serious na maisha) wa darasa la saba wapange chumba tandale kwa tumbo elfu 15 kwa mwezi wanunue ballo la mitumba watembeze vijiweni, kwenye bar, sokoni na hata kwenye stendi kuu za daladala. Wasomi watakuzingua.
 
Kila mtu anajitegemea hawapo pamoja.


Nazi wazitoe shamba walete mjini, wahakikishe wanawateja tayari mkononi.
Iliki kutoka polini kuleta mjini, watafute wateja kwanza.
Usambazaji wa nyama na samaki mahotelini, watafute wateja wakudumu kwanza na wa uhakika.

Uzuri wote ni wasomi hivyo sio suala gumu kufanya marketing kwenye hotel zote za mijini, sina shaka na lugha ya kibiashara kwao na ile lugha iliyokuja na jahazi.
 
Waje kwenye mgodi wako sister? Unapatikana wapi?


Sina mgodi boss! Sema km wako serious kbs watamake ...!nahakika ndani ya kila siku 7 watakuwa na uhakika wa kumake 700k..! km ni wachakarikaji hela ipo tu ..all the best!
 
unataka uwapige fero zenye chabo ndogo vijana wakose hata hela ya kurudia home..

hhahahahhhha natania tu...


😅😅😅 Muogope Mungu mzee baba!..mm sijafikifiria ht kidg wafanye hizo mambo...! Nyie mmekariri eh😅!mtanyooka mwaka huu👯👯
 
Kama hao vijana wameshindwa kuja kwako walau na wazo la biashara, basi amini tu kwamba hiyo pesa umeamuwa kuitowa sadaka
 
Back
Top Bottom