Kwa hiyo wazungu wamependa falsafa na uongozi mahiri wa Rais Samia, Je, wamemnunua kabisa?

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Tanzania tunatabia ya kupuuza viongozi wetu ila Ulaya wanawahitaji sana viongozi wetu!

Ilikuwa Kwa JPM nchi kadhaa wananchi wake walisikika kumtaka akaongoze nchi zao hadi huko Ulaya na American

Tuna Raisi Samia sasa, Mbunifu na mahili kuongoza na kuelekeza, ni mwanademokorasia haswaa na hiyo Ulaya ndio sifa kuu ya kiongozi anayetakiwa,

Rais wetu Kwa muda mfupi amefanya yasiyotarajiwa, kubwa kabisa ni kumalizana na Mgogoro wa viongozi wa Chadema waliokuwa wameswekwa ndani na kukabiliwa na mashitaka yasiyo na dhamana Kwa kufuta kesi zote, jingine kubwa ni kuiunganisha Tanzania na dunia iliyokuwa ikionekana kutengwa

Lingine kubwa na la ajabu na la kushangaza ni film iitwayo the Royal of Tanzania, hapa tukubaliane sote kuwa, Raisi wetu kaupiga mwingi saana

Mafuta huku bei poa, umeme haukatiki, bidhaa hazina bei kama huko America na Ulaya, na mawaziri wanakula Kwa urefu wa kamba zao na tunaishi nao vizuri kabisa

Mh Rais wetu alisafiri kuelekea huko American sasa ni wiki sasa bado hajarudi, Je, huwenda wa USA wamemkodi ili awapige push kidogo hawa wazungu ukilinganisha na magumu wanayoyapitia huko?

Vita vya Urus na Ukraine, maisha kuwa ya juu zaidi, dollas kuonekana Kwa miaka michache ijayo isiwe tena na solo kama ilivyokuwa Kabla ya vita vinavyoendele huko Ukraine na Urusi?

Au kunatarifa gani bajemeni, Rais wetu tumemisi arudi sasa, na kama ndivyo wa USA wamemkodi watoe tarifa tujue moja
 
Wanamtamani ili na wenyewe wawe maskini kama Afrika?
 
Back
Top Bottom