Kwa hiyo upigaji kura bungeni umeonesha Kipi chama cha Upinzani

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Kuanzia kuchagua spika, waziri mkuu, na naibu spika imekuwa dhahiri kwamba chadema ndicho chama pekee cha upinzani bungeni. Waliobakia wote ni chama tawala na matawi yake. Ndiyo maana pia sioni tija ya serikali ya umoja wa kitaifa. So boring!
 
makubaliana na wewe kwa 100%,
Chama pekee cha upinzani bungeni ni CHADEMA na vilivyobaki ni NG0's za Ccm. Shame on them!
 
Kuanzia kuchagua spika, waziri mkuu, na naibu spika imekuwa dhahiri kwamba chadema ndicho chama pekee cha upinzani bungeni. Waliobakia wote ni chama tawala na matawi yake. Ndiyo maana pia sioni tija ya serikali ya umoja wa kitaifa. So boring!

chadema waliliona hili muda mrefu toka kwenye kampeni ndiyo maana wakavipiga chini kwenye kambi yao...Go chadema tuko nyuma yako:yield::yield::yield::yield::yield::yield:
 
Kama serikali ya umoja wa kitaifa ina maana hii basi inakuza na kuendeleza "amani na utulivu" lakini inaua demokrasia. Nimewasikia wakiahidi pia kujenga "Bunge Moja" nahisi wanamaanisha kusiwepo na chama au mbunge atakayepinga hoja yoyote, kwa mujibu wa maelezo ya Job Ndugai alipokuwa anaomba kura za unaibu spika.
 
huyu ni kama kinyonga, ndio maana ngozi yake nayo imebadilika rangi!

Ngozi kubadilika rangi ni kutokana na ugonjwa wa kisukari alionao. hivyo kwenye swala la afya ya mtu tusifanye masihara. Tumwombee kwa Mungu afya yake iimarike
 
Ndo chama pekee ambacho mpaka sasa viongozi wake hawajanunuliwa na mafisadi, hofu yangu ni walioingia juzi juzi wakitokea CCM!
Maana nasikia wabunge wengine wa chandema, hawajui kama ni wa chadema au ccm, ref. Shibuda!!
 
Oh yeah! CCM Bwana!!! Yaani CUF wametundikwa kwenye ndoano huku waki-smile!!! Afadhali NCCR-Mageuzi waliisambaratisha kwa kuigawa -- Marando group vs Mrema Group na alipoondoka Mrema ikasambaratishwa kwa kuigawa tena -- Mrando Group vs Mbatia group!!

Hawa CUF wamechinjiwa baharini kewupeeeee ambako walijipeleka wenyewe!! For all practical purposes CUF is dead, very dead!!!! Itaendelea kupumua kwa nguvu ya CCM tu. I am very much disappointed with Hamad Rashid Mohamed whom I held in high esteem!! Katekwa na mafisadi!!!

Chadema ni lazima ijifunze hapo. Kwanza ikatae ushirikano wowote na chama chochote cha upinzani Bungeni. I know CCM are behind the present feud -- wanataka kupandikiza watu wao katika safu ya official opposition Bungeni! Msikubali! Waache wapige kelele hadi watokwe machozi -- hakuna kushirikiana na CUF au na utumbo mwingine wowote eti unaojiita opposition!
 
wana jf historia inaandikwa kwa wino mwekundu sasa atajulikana adui no moja wa taifa letu tulieni mtaona wanangu mateso yanapo zidi ukombozi uko karibu kama unavyomuöa ngombe akichinjwa teke la mwisho kali UMA UNAONA NA NDIO NGUVU YETU
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom