Kwa hivi vigezo, je rais wetu ni mzalendo?

Ibra Mo

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
794
250
Wote tunafahamu yakwamba kwa sasa Zanzibar ni Nchi kamili inayojitegemea hii ni baada yakufanya Mabadiliko Makubwa katika Katiba yao.

Pia kuna Wabunge wengi sana wanaotoka Zanzibar ili kuunda Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mie hawa Wabunge kwakweli kazi yao siielewi zaidi yakutufilisi huku Bara na hakuna Mbunge hata M1 anayetoka Bara kuunda Baraza la wawakilishi.

Kitendo cha Rais kuwapa Wanzibar Wizara zote Nyeti kwa Usalama wa Taifa letu ambako ndipo kuna majeshi yetu na Siri zote za Usalama wa Taifa kinakupa picha gani?

Wizara ya Ulinzi:HUSSEIN MWINYI.

Wizara ya Mambo ya ndani(jeshi la polisi,magereza,idara ya uhamiaji):SHAMSI VUAI NAHODHA.
 
sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
397
195
Huu muungano kwanza hauleweki ni wa nini, sasa linapokuja swala la uwiano likawa kama tunavyoliona ndio wanatuzidishia hasira.Kinachoshangaza zaidi waZNZ wanalilia sana kuvunjwa kwa muungano,viongozi fulani fulani bara ndo wanaung'ang'ania sijui kuna siri gani imejificha hapa.
 
jyfranca

JF-Expert Member
Oct 3, 2010
297
0
Mbona hushangai Zanzibar ina Rais mmoja, makamu wa Rais 3. na Jaji mkuu pia Mzanzibar, kwa uwiano Bara inatoa nafasi 3, Rais Waziri mkuu na Spika Zanzibar 5, Rais Wa zanzibar, makamu wa Rais Muungano, Makamu wawili wa Rais Zanzibar na Jaji Mkuu
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,690
2,000
Huu muungano kwa kweli unanichanganya, sijui ni kwa sababu ya nyufa!
 
m_kishuri

JF-Expert Member
Jan 27, 2010
1,485
1,225
Wote tunafahamu yakwamba kwa sasa Zanzibar ni Nchi kamili inayojitegemea hii ni baada yakufanya Mabadiliko Makubwa katika Katiba yao.
Pia kuna Wabunge wengi sana wanaotoka Zanzibar ili kuunda Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mie hawa Wabunge kwakweli kazi yao siielewi zaidi yakutufilisi huku Bara na hakuna Mbunge hata M1 anayetoka Bara kuunda Baraza la wawakilishi.
Kitendo cha Rais kuwapa Wanzibar Wizara zote Nyeti kwa Usalama wa Taifa letu ambako ndipo kuna majeshi yetu na Siri zote za Usalama wa Taifa kinakupa picha gani?
Wizara ya Ulinzi:HUSSEIN MWINYI.
Wizara ya Mambo ya ndani(jeshi la polisi,magereza,idara ya uhamiaji):SHAMSI VUAI NAHODHA.

Duh, Kumbe ukiwa mzanzibari sio mtanzania? Au ni mtanzania wa jina tu, lakini haupaswi kupewa wadhifa wowote nyeti? itanibidi nikasome katiba ya jamhuri ya muungano nione inasemaje kuhusu suala hili.
 
Ibra Mo

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
794
250
Hoja ya msingi kwenye hii thread hainatija.
Weka yako yenye tija.Toa majibu kwa nguvu ya Hoja sio unakurupuka tuuh.Mi nataka unichallange kwa nilichoandika.
Kama Mtu kutoka Bara anahitaji Kibali ili aishi Zanzibar...I stand 2b corrected je M2 kutoka Bara ambaye hana Asili ya Zanzibar anaweza kupewa Madaraka kweli!!So kwanin sisi Tusihoji huu Utumwa tunaofanyiwa.
 
Lenana

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
421
225
Duh, Kumbe ukiwa mzanzibari sio mtanzania? Au ni mtanzania wa jina tu, lakini haupaswi kupewa wadhifa wowote nyeti? itanibidi nikasome katiba ya jamhuri ya muungano nione inasemaje kuhusu suala hili.

ndugu nakushauri ukasoma katiba ya tanganyika! kwanini mzanzibar ni mtanganyika na mtanganyika sio mzanzibar kwa kifupi wazanzibar ni maparasite wanavuna pasipo kupanda! anzia hapa kodi ipi inayotoka zenj inaingia katika fuko la tanganyika! and vice versa of the later is true!
 
m_kishuri

JF-Expert Member
Jan 27, 2010
1,485
1,225
ndugu nakushauri ukasoma katiba ya tanganyika! kwanini mzanzibar ni mtanganyika na mtanganyika sio mzanzibar kwa kifupi wazanzibar ni maparasite wanavuna pasipo kupanda! anzia hapa kodi ipi inayotoka zenj inaingia katika fuko la tanganyika! and vice versa of the later is true!

Kwa hiyo inamaana utawala wa rais A. H. Mwinyi ulikuwa batili? Kwa sababu yeye alikuwa anashikilia our HIGHEST OFFICE IN THE LAND.
 
MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
1,101
1,500
Andaeni maandamano ya kudai uhuru muungano uvunjwe mupewe Tanganyika yenu.Shortly, mie naona hio kupewa hao wazanzibari vyeo na JK ni kama danganya toto.....Msimamo wangu upo pale pale, muungano lazima uletwe kwa wananchi watie baraka zao.

Sio Kibabu kimoja kutoka Butiama kimekurupuka na chupa mbili za udongo wa Tanganyika....Sote tufate kama makondoo!Tunahitaji kuulizwa kama wananchi wanataka muungano ??? Mie mmoja nitakuwa mpiga kampeni ya HAPANA.
 
Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
0
Weka yako yenye tija.Toa majibu kwa nguvu ya Hoja sio unakurupuka tuuh.Mi nataka unichallange kwa nilichoandika.
Kama Mtu kutoka Bara anahitaji Kibali ili aishi Zanzibar...I stand 2b corrected je M2 kutoka Bara ambaye hana Asili ya Zanzibar anaweza kupewa Madaraka kweli!!So kwanin sisi Tusihoji huu Utumwa tunaofanyiwa.

Mtu aliyekurupuka kukujibu usipoteze muda wako wa kumjibu. Achana nae.

Kuhusu thread yako, kuna idea moja ambayo miye siifurahii sana hasa kutokana na hulka ya wazanzibar wengi. Eti watanganyika wakienda visiwani kushika madaraka, wananchi wa visiwani watajisikia wamemezwa ndani ya muungano kuliko sisi tunavyojisia kwa wao kuja kushiriki kwenye uongozi tanzania bara. Hiyo point sioni mantiki. Kama nchi zimeungana sioni sababu kwa nini mtanzania bara kama anakubalika asigomee ujumbe wa baraza la wawakilishi??? Kwa ujumla, hilo eneo mojawapo la kero za muungano zinazopaswa kupatiwa majibu. Sasa hivi maduka mengi tanzania bara ni ya wapemba. Lakini nenda visiwani kama utakutana na maduka ya wachaga.

Mimi nina imani kwamba haya mapungufu yataondolewa endapo watanzania watakubali chama kingine kishike madaraka ya kuongoza nchi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom