Kwa hivi utamtembelea jela tu MTOTO WAKO! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hivi utamtembelea jela tu MTOTO WAKO!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Aug 7, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,627
  Likes Received: 5,790
  Trophy Points: 280
  Kwa hivi utamtembelea jela tu!

  Lily/EmmanuelNI JUKUMU ULILOPEWA NA MUNGU WEWE MZAZI KUHAKIKISHA WATOTO WANAKUWA NA NIDHAMU NA TABIA NJEMA.
  Kujisahau na kufanya mambo yafuatayo unaweza kujikuta mtoto wako anaishia mikononi mwa polisi na anaishi jela baada ya kuachana na kuwa mtoto.
  Na ukifanya yafuatayo ni kweli hutakosa muda wa kwenda kumtembelea jela.
  Hakikisha unampa mtoto wako vitu vyote anavyovitamani.
  Akikua na mtazamo wa aina hii atajua kwamba ni kweli duniani inaweza kumpa chochote anachotaka.

  Ukiona ameanza kujifunza maneno mabaya na machafu, mchekee tu, hii inamfanya ajione yupo smart sana pia itampa nguvu ya kujifunza maneno mengine na sentensi zingine zenye maneno ya aina ileile ambayo siku moja yanaweza kukutikisa kama si kukufanya uzimie.

  Hakikisha humpi nafasi ya kuwa na uhusiano wa kiroho (training). Subiri hadi awe na miaka 21 atakapoamua mwenyewe kujiunga na dini au kuchagua mwenyewe masuala ya kiroho au afuate na aishi vipi kiroho.

  Hakikisha unakwepa wa nguvu zako zote kumtamkia kwamba “umekosea” ili usimsababisha ajisikia hatia. Mwambie ana akili sana kiasi kwamba hawezi kukosea kitu chochote.
  Hii itamsaidia kujua ni kosa au si kosa kuvunja mlango wa gari lililoegeshwa na kukamatwa na polisi.

  Hakikisha unamsaidia kazi zote hadi kuondoa sahani au vyombo wakati amemaliza kula au kumfulia nguo hadi akiwa na miaka 21 pia mwambie asijali sana kwani wenzake watakuwa wanamsaidia kazi mbele ya safari.

  Hakikisha baba na mama mnazipiga mbele ya mtoto siku zote, msithubutu kupigana au kuzozana bila yeye kuwepo kwani kwa njia hii mtoto wenu (watoto) hatashangaa sana au kuumia sana siku mkiachana.

  Mpe mtoto wako pesa zote anazohitaji kwa ajili ya matumizi yake, usimshawishi kutafuta pesa zake, kwa nini apate shida kupata pesa kama unavyofanya wewe? Ni mtoto wako mwache afurahie matunda ya kuwa na mzazi mwenye pesa, jitahidi kufanya hivi hadi afikishe miaka 21 hapo unaweza kuanza kubana au kumpa pocket money pungufu.

  Hakikisha hakuna siku ana njaa, mpe kila aina ya chakula ambacho tumbo lake linaweza kubeba, pia kila kinywaji ambacho yeye anapenda hata kama unaweza kuagiza mbali kwani ni mtoto wako lazima umpe kitu roho na mwili vinapenda au vinatamani.

  Usikubali majirani, walimu au polisi kuingilia maisha ya mtoto wako kwani hawa hawana uchungu na mtoto wako, mwenye uchungu na mtoto ni wewe mzazi, isitoshe mtoto ni wako si wao au jamii au jamhuri.

  Siku ukiona amekasirika hakikisha unamuomba msamaha na mhakikishie kwamba hutarudia tena yeye za zaidi ya yote yeye ndiye yupo sahihi wakati wote.

  Kama hujapata mtoto bado akishazaliwa tu hakikisha unampa jina ambalo hata wanafunzi wenzake wanaweza kumtania majina kama “Shida, Mateso, Chuki, Luleho (wabena mpo?), Fisi, Maskini, Sinahaki nk ilimradi tu likitamkwa jina lake lazima ataniwe.
  NB:

  Mlee mtoto katika njia ipasayo, Naye hataiacha hata atakapokuwa mzee
   
Loading...