Mto_Ngono
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 686
- 589
Nipe nikupe wote tufaidi!!!!
Mara nyingi unapotoa fedha ili kupata huduma unategemea kwamba huduma unayohitaji itakuwa sawa na kiwango cha pesa uliyotoa au pengine ni bora zaidi kuliko kiwango cha pesa uliyotoa. Najua umekutana sana na pengine umetoa kiasi flani cha fedha ukilipia parking slots (wenda nisiite parking slot kwa sababu bado hakuna ubora wa namna hiyo niite egesho ambalo halijarekebishwa wala kuongezewa thamani). Leo ntaongelea kidogo malipo pembezoni mwa ufukwe hasa Coco beach na nimechagua kuongelea hapa kwa sababu malipo yake yako juu tofauti na sehemu nyingine nikimaanisha mwenyegari anatakiwa kulipa shilingi 900.
Swali la kujiuliza ni , Je pesa hiyo ukilipa unafaidika na nini au ni huduma gani nzuri ambayo unapata kwa kulipa? Naamini ela ni ela tu hata ikiwa ndogo bado ina thamani na pia tunaamini ni mipango ya uongezaji wa mapato ya Manispaa ambayo ni mizuri tu na kwa upande wangu nafurahi kutoa ili kuleta maendeleo lakini fedha inayotolewa haioneshi kuongeza thamani yoyote katika eneo husika je ni kweli kwamba hakuna mipango ya uboreshaji wa maeneo hayo ya ufukweni ili mapato yaweze kuongezeka maradufu? mazingira ni mabovu si attractive. Siwezi mlaumu mzabuni aliyepewa hiyo zabuni ya kukusanya kwa sababu yeye naye anaangalia maslahi yake na ya wafanyakazi wake ila suala hili lipo chini ya Halmashauri.
Wenda nishauri tu kwa sababu wote kwa namna moja au nyingine tunashiriki katika ujenzi wa Taifa letu hivyo kushauriana kwa mambo ya msingi yanayolenga kuleta maendeleo ndio uzalendo wenyewe. Nashauri kwamba halmashauri iweze kufanya maboresho ya maeneo hayo kutokana na mapato wanayopata ili iweze kuongeza makusanyo namaanisha mandhari nzuri huongeza wingi wa watu na mali zao. Kama Halmashauri haitaweza kurekebisha yenyewe ni vizuri ikatangazwa zabuni na akapatikana muwekezaji wakaingia katika joint venture ambayo itatoa faida kote kote.
Leo nimeongelea maeneo ya ufukweni lakini zoezi la kuongeza thamani katika maegesho linaweza kufanyika kote kwa sababu sehemu nyingi wenye magari wanapotoa fedha za maegesho ni mbovu na ziko katika kiwango cha chini.
Tufuate mifano hapa chini:-
Naishia hapa kwa leo, wenda nawe unaweza shauri zaidi.