Kwa hili simuelewi JK!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili simuelewi JK!!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Sajenti, Nov 12, 2009.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jana nilipokuwa naangalia taarifa ya habari TBC1 kulikuwa na habari ya ziara ya JK nchini misri na alipata nafasi ya kuonana na watanzania wanaosoma nchini humo.

  Katika mazungumzo yake na hao wenzetu walioko huko alisema anafikiria kushauriana na wizara ya elimu hapa Tz ili waanzishe mtaala wa somo la kifaransa kwa shule za msingi kwa kigezo kuwa lugha ni jambo muhimu na ni vizuri vijana wetu wakaanza nao kujifunza kifaransa pia.

  Sasa nashindwa kuelewa kama hili aliliongea kwa dhamira ya dhati au kutaka kufurahisha wale aliokuwa akiongea nao pale au sisi tulioko huku. Ukizingatia kuwa elimu yenyewe ya msingi hapa Tz ni mshikemshike, kuna sekondari za kata ambazo mpaka leo hazionyeshi dalili ya kutengemaa kwa mahitaji muhimu kama vile walimu, madarasa, madawati, maabara, vitabu etc. Sijui kama ameshafanya utafiti wa mahitaji ya kuanzisha somo la kifaransa katika shule za msingi ikiwemo walimu wa kufundisha somo hilo, vitabu nk...Wadau hebu tulijadili hili....
   
 2. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Punguza munkari ndugu, sio kwamba JK ameshaamua kwamba Kifaransa kifundishwe shule ya msingi, amesema atajadiliana na Wizara husika kuhusu suala hili. Inawezekana kabisa hayo unayoyasema yakaonekana kuwa ni kikwazo baada ya majadiliano kufanyika.
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,829
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Hilo la kiingereza lililoanza kufundishwa tangu tupate uhuru bado halijaeleweka! Politics bana. Thats why I hate politics from the bottom of my heart!
   
 4. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  =======

  Wou! You better hate it from the "heart of your bottom"::)

  With a light touch!
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Mhhhhh....Nna wasiwasi utatakiwa ufute Kauli hiyo!...Ni kama vile ni Nzitonzito Kidogo!
   
 6. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hizi shule zetu za msingi na sekondari za UPE sio zile za school bus mwalimu anaye fundisha somo la kingereza akiongea unaweza kupatwa na mshtuko wa moyo ama ukazimia kabisa, sasa hilo la kusema anataka kuweka kifaransa kifundishwe kwenye shule zetu za UPE si walimu wataacha kazi wote ikiwa kingereza kutamka maneno ina kuwa shida ama atatuletea wawekezaji wa kifaransa waje kutufundisha hicho kifaransa??
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, si vibaya kupromote kifarnsa hata tunapokwenda kwenye utandawazi... nadhani kwa hali inavyoenda itakuwa bora pia kujua kihindi na kichina pia, kwa shule itakayoweza kutoa hiyo elimu!!!

  ...cha kusikitisha zaidi ni kwamba hata yeye hatakuelewa unachosema hapa!
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,829
  Trophy Points: 280
  You are right PJ. Am just counting seconds!
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Baija, una maana gani?
   
 10. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  ======

  OK Mea Culpa please.
  My intention was to show I hate the proposal of imposing French language in a already devastated system of medium of instruction.

  No insult intended to a person. The idea itself is distateful and unpalatable to be compared with a "heart of the bottom" if it ever exist!

  I am sorry for the trouble I might have caused on your part.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu Baija;

  Nakupa tano kwa kuwa muungwana na kutuelewesha, kumbe hukuwa hata na nia mbaya

  Mida yenyewe hii wengne tushachemsha
   
 12. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Badala ya kuangalia uwezekano wa kuendeleza kiswahili kwa kuongea rais/waziri wa elimu wa misri ili kuangalia uwezekano wa Kiswahili kufundishwa huko yeye anataka kifaransa.Hii ni kwa faida ya nani?hata kama ni utandawazi tunaowajibu wa kuwafundisha watu wetu kwa lugha ambayo wanaielewa vizuri ili wawe na uwezo mzuri wa kufikiri na kutenda kwa lugha wanayoijua.
  Tuthamini kilicho chetu japo kidogo.Leo hatuna watu wa kujivunia kwenye fani ya sayansi kwa sababu nyingi lakini moja wapo ni tatizo la lugha.
   
 13. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nani kasema warembo hunuka kikwapa? sema huyo uliye ne ndo haogi! tembea uone!
   
 14. h

  hembe Member

  #14
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nakumbuka Lowasa aliwahi kuwaambia watu wasome Kichina jimboni mwangu,nadhani ni matatizo ya kutokuwa na misimamo ya nini wanafanya,kwa sasa tunatakiwa kuboresha elimu iwe imara na si kuruka ruka na kila tunachoona kinalipa ktk sehemu moja kwan tunahitaji zaidi ya hilo.all the best JK in your wrong path
   
 15. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #15
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Nilikuonya kujiunga na legends hukunisikia rudi kundini u were not meant to be a politician......
   
 16. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2009
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  pole kaka kwa kushindwa kumuelewa raisi wako... ila mi ningependa kukushangaa kwani kuna lipi linalofanywa na serikali yako ambalo halikushangazi... yaani kwa kifupi mtindo wa kuendesha nchi wa serikali yako.. ni ule wa "NA MIMI MAMA" kama uliwahi kusoma hicho kitabu... yaani sisi tupo kutaka kufanya yaliyofanywa na wenzetu bila kuangalia msingi na mipango dhabiti... na ofcoz kingine tunachoweza ni kule kuleta mambo ya msingi yanayobeba maisha na utu wa watu kwa njia ya suprise.. lolote litakaloamuliwa na serikali basi ujue linakuja kwa suprise yaani utekelezaji kwanza halafu elimu jamii baadae tena hiyo elimu jamii unakwenda kusikilizia mahakamani...

  TANZANIA NI MOJA KATI YA NCHI RAHISI SANA KUONGOZA.... kwani kila linalofanyika watu wanaamini limetokea kwa bahati mbaya hakuna anayetakiwa kuwajibika.......ni nchi ya masikhara...

  nafikiria kutafuta mchongo wa kupata direct bora wa filamu kutoka holywood najua nikimleta bongo akae walau wiki tu lazima atapata hadithi za filamu kama 100 hivi.. kuanzia maisha ya mtu mmoja mmoja na serikali kwa ujumla.. kwani nahakika hataamini kama this is how ppl lives...
   
 17. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  mea maxima culpa
   
Loading...