Kwa hili, serikali yetu ndio inayosababisha walimu waonekane wanafanya kazi kwa mazoea.

Nitafurahi ukiandika siku yako huwa inaanzaje na kuishaje.. na unakula kula mara ngapi kwa siku... unapika au unakula nje.
badili maneno na uonyeshe kua utangefurahia kama ungeona serikali imetopa pesa za kujikimu ili tusiishi kama mashetani, hivyo tuwe na moyo mkunjufu wa kulitumikia taifa.
Tuition yako wanafunzi unao, haujawahi kupata au wamekukimbia!? Unatumia fimbo kuhadhibu wanafunzi? Usipo wafundisha unakuwa unafanya nino darasani?
sifundishi twisheni na sina mapango huo. ila natahadharisha wanafunzi, wasikae wakitegemea sana huduma kutoka kwa walimu wenye njaa iliyosababishwa na serikali, bali wawaone wazazi wao na wakatafute elimu kokote. kama ni kufundishwa na wazazi au ndugu zao, au kusoma twisheni za mtaani, au kuhamia private ili kuungana na watoto wa vigogo wakafundishwe na walimu wasioteseka na njaa. ukimwambia mwanafunzi asubiri huduma kutoka kwa mwalimu mwenye njaa inayosababishwa na serikali, unakua na lengo la kumpotezea ndoto zake.
 
Back
Top Bottom