Kwa hili Serikali ya awamu ya tano haipunguzi ila inaongeza tatizo

BLACK_WIDOW

Senior Member
Nov 17, 2018
133
318
Ni wazi kuwa serikali hii tangu iingie madarakani imekuwa ikipinga ukosoaji katika utendaji wake wa kazi, Japokuwa ni jambo la ajabu, sasa usipotaka kukosolewa na wale unaowaongoza endapo wataona baadhi ya mambo hayaendi sawa unataka akukosoe nani?

Nikienda moja kwa moja kwenye hoja, Mjadala mkubwa umeibuka na kuleta sintofahamu juu ya kupanda kwa gharama za vifurushi vya internet

Bila kupepesa macho hawa hawa wasiotaka kukosolewa ndiyo wamefanya haya kwa makusudi ili kuhakikisha matumizi ya mtandao yapungue kwa kupandisha gharama za internet.

Kwakuwa miongoni mwa platforms kubwa za ukosoaji zipo kwenye mitandao, ukianzia na kinara Twitter ambayo ni wazi ndio platform inayowaumiza kichwa ndo maana si ajabu kuona hata uchaguzi ulivyoisha bado ikabanwa wakati pengine paliachiwa.

Wito wangu kwa serikali ya Awamu ya tano. Ipitie upya move hii, kwani ni bora hata hao Watanzania ambao wengi wao wanalalamika na uchumi ulivyo kwa sasa, wakapata namna ya kupoteza mawazo kupitia socialization ya mitandaoni, kuliko kuwawekea ngumu huko, wakakosa namna ya hata ku-divert feelings zao. Kwa huu mpango wenu.

Huo ukosoaji ndo utazidi sasa, utabadilika tu, utakuwa sio ule wa twitter ila utakuwa wa mitaani na vijiweni, kwanza hii mitandao wengine hawaendi huko kwa hao akina kigogo sijui, wengine wao wakienda kwenye page za udaku tu ndo burudani kwao, wapate ubuyu tu

Nyie wenyewe mashahid jinsi sometimes watu mnavyowahamisha kwenye baadhi ya mada nyeti, kutumia kiki za mitandao, wabongo wengi tunapenda hivyo vitu.

Kubana matumizi ya internet hata nyinyi wenyewe haina Afya kwenu.
 
Back
Top Bottom