Kwa hili safu ya uongozi nchini si salama.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili safu ya uongozi nchini si salama....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BJEVI, Jul 3, 2012.

 1. BJEVI

  BJEVI JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama wasaidizi wa rais wamechoka kiasi cha kuongea mambo yasiyoendana na sifa na vyeo vyao ni janga kubwa kwa taifa hili la ulumwengu wa tatu.msaidizi wa rais mathalani stella manyanya-rc -rukwa ni kielelezo tosha kuwa kuna mapungufu makubwa mno katika mfumo wa uongozi hapa nchini,ni aibu kwa serikali na dharau kwa wana rukwa kuwakilishwa na watu wa aina ya stella.ni wazi na nianaamini pia wasaidizi wa rais kwa asilimia 50 hawamsaidii mkuu wa nchi.ndo chanzo cha mkuu kitwa dhaifu.

  Kama kauli za viongozi wetu zimefikia hapa (taarabu,ngonjera,mipasho,uonngo,kupandikiza chuki hadharani,dharau,kebehi) hasa kwa mambo muhimu kuhusu raia ni aibu .je! Kama hali iko hivi kwa wakuu wa mikoa vipi hawa,wapo kama manyanya au kuna unafuu,au ndo kabisa vituko?

  1. Wakurugenzi
  2. Wakuu wa wilaya na
  3. Makatibu tawala
  4.wakuu wa idara mbalimbali za serikali ? Je! Hii inatokana na nini ni kujipendekeza au?.
   
 2. U

  Udaa JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 727
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Liwalo na liwe.
   
 3. E

  EJL Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  Msamehe bure Eng. Manyanya. Huyu alipogundua kuwa "professional" hailipi akakimbilia kwenye siasa akidhani atawini. Kwa hakika Stella alikuwa miongoni mwa wanawake wazalendo wa taifa hili. Lakini ADUAI NJAA na TAMAA akamvaa mwanamama akishindwa kufurukuta. Kutumia fani anataka; lakini akaona kwa hali ya nchi atakufa bila hata kuwa na kakibanda. Akawauliza wenzake; akagundua weeeeengi sana wameacha na kujiunga na "biashara inayolipa sana". Alimtazama Sarungi, Mwandosya, Shein, Msolwa (just to mention few of them) akaona huu ujinga! Kwa nini nisumbue kichwa changu kubuni na kutenda kisayansi wakati naweza kaa mahali; nikisinzia inalipa, nikitukana inalipa? Akajiunga huko kwa politic haraka.
  Lakini akagundua kumbe hata huko si wote wanatembelewa na neema. Akamtazama mama yangu Maua Daftari miaka yoote, elimu yoote, uzoefu wooote; lakini daima anaishia kwa unaibu waziri! Lakini akamuona Ngeleja, Masha, Maige, nk wameingia tu mjengoni wakatwikwa uwaziri! Akaona wako hata walioshindwa udiwani wakapewa ukatibu tarafa baada ya miezi sita wakaramba uDC.
  Stella akajiuliza nitoke vipi?? Jamaa yake Sitta alipompa ulaji kupitia tume ya Mwakyembe, akipiga vigelegele kuwa sasa nimepata mpenyo. Akakomaa mwanamama, akahakikisha waTz wote wanamjua kwa kuonesha uzalendo wa kinafiki. "tulitishiwa sana, wapo waliotaka kutuhonga". Wadanganyika kama kawa tukampigia saluti kuwa ni mzalendo wa kweli. Stella akawini kudanganya umma kuwa wamefanya kazi kamili na ya haki kwa manufaa ya nchi. Kumbe ni kwa manufaa ya tumbo lake/ matumbo yao. Wakafanikiwa sana kuonesha umma kuwa katika waovu wakuu wa nchi ni yule "Mzee wa Monduli". Wakati wakituwini wadanganyika. Stella na kaka yake Mwakyembe wakahakikisha kuwa waanatumia fursa hii kumshika vema mkuu wa kaya. Tangu mwanzo walijua mkuu wa kaya ni kiini cha Richmond/ Dowans; uchunguzi wao wa kimagirini ukawawezesha kuthibitisha hisia hizi. Na kwa kuwa yule "mzee speed and standard" alikuwa anajua afanyacho wakakubaliana kumchinja mzee wa Monduli kama kafara ya wao kupata ulaji zaidi. Wakamwambia mkuu wa kaya, "unajua hawa wadanganyika hawana issue sana mzee, ni wepesi kuamini uongo wa rejareja. Sie hatutasema yote maana hawaulizi hawa. Daima ukisimama pale kwenye maiki ukazungumza huku wao wakikutazama kwenye kideo cha TBC na ukiongea kwa mbwembwe kibao; jamaa hutikia "amina" haraka sana. Muhimu mzee TUKUMBUKE NA SIE.
  Ndivyo ilivyokuwa, wakatoa taarifa nusu na mkuu wa kaya akatimiza ahadi ya kuwakumbuka ktk enzi yake. Stella kweli ni injinia alipiga hesabu zinazolipa; ni wapi angepewa shangingi, nyumba, ulinzi na posho za semina elekezi kiasi hiki? Kuna biashara nzuri kama kuwa mkuu wa kaya anayotokea kiranja mkuu? Bahati mbaya wamegawa mikoa lakini si haba kabla ya kwenda Katavi lazima atapita Rukwa.
  Wana JF msimshangae kabisa Stella, kamwe hawezi "kuukata mkono unaomlisha". Hawezi kunyea kambi!.

  Ukitaka kujua huyu Stella tangu awali aliingia ktk siasa kwa njaa yake; rejea mchango wake bungeni na Bidii forum wakati wa mjadala kuhusu ongezeko la posho za wabunge. Hapo hutashangaa kwa nini anasimama na kuzungumza kama "chemba" au "kibajaji" au yule kwaya master! Afanyeje; aseme ukweli? Afikiri kwa mantiki na kushauri serikali ifanye vema ili akose ulaji! THUBUTU!


  EJL
   
Loading...