Kwa hili Rais Magufuli usije kumtafuta mchawi!!

Haaa unbelievable!!

Eti uhakiki haukuwahusu wanasiasa na wateule wa rais bali watumishi wa umma serious??

Kwanza watumishi wa umma ni akina nani?

Mshahara wa wabunge, mawaziri, RCs, DCs ni mali ya nani??

Kumbe ukifoji vyeti ni jinai tu ukiwa mwl, nesi, afisa ugani nk. lakini ni halali ukiwa mwanasiasa au mteule wa rais.

Yaani mimi nakamshahara kangu ambako hakana hata allowance yoyote bali kodi, bodi ya mikopo nk. kwa elimu niliyoipata kihalali nahangaishwa kutwa kucha eti kujiridhisha vyeti vyangu huku wengine wakila kwa vyeti vyenye utata??

Hoja kubwa si kuwa ama kuto kuwa mwanasiasa hoja ni KUGHUSHI, yaani kutenda kosa la KUGHUSHI, teua tu hata akiwa la saba as long as elimu yake haina utata ana haki ya kuteuliwa.

Leo unaweza ona umetuweza watanzania lakini amini hili halitawaacha salama kisiasa, inaonyesha kuna chuki iliyojificha na watumishi.....ndugu zetu wameachishwa kazi a few months kabla ya kustaafu kwa kosa tu la kutumia vyeti vya wengine japo wamefanya kazi muda mrefu halafu eti wengine waendelee kutembelea magari manene na vyeti hivihivyo, unatupa wakati mgumu kuamini dhamira yako kama ni ya dhati, isiyo na uonevu.

Dr. umeongea kwa hasira sana mna mix vitu viwili

1.qualifications
2.vyeti feki

kosa la makonda kama lipo ni vyeti feki na si qualifications

kwa maana akiteuliwa hawajibiki kuonyesha vyeti wala mwajiri wake hana mpango navyo

kwa hiyo kama ndivyo assume viongozi wote ni darasa la saba.....

kosa la makonda kama lipo na kama kafanya ni kufoji vyeti na sio qualificaton

sasa kuna haja ya wewe na mimi kufungua mashtaka na sio kulia humu
 
Tuna Rais wa ajabu haijawahi kutokea.

Niliwahi kumwambia rafiki yangu wakati wa vuguvugu la kampeni 2015, sitathubutu kuipenda CCM daima hata kama wanifanyie mema mengi kiasi gani.
Sasa kwa haya yanayotokea ndio nazidi kuichukia zaidi.

Watu wenye taaluma zao wanakana na kushindwa kusimamia kauli zao walizozisema tena zingine wamezichapa kwenye majarida yao kisa ni kusaka tonge.
Inahuzunisha sana Kiongozi kujinadi kuwa ni wa wanyonge lakini hapo hapo anawanyonga hao hao wanyonge, sijui wanyonge anaowasema bado hawajazaliwa? Shame on him!!.
Wanyonge wengine wanafikia kusema bora wangezaliwa Faru Fausta katika nchi hii kuliko kuzaliwa binadamu.
Nikikumbuka janga la wana Kagera mwaka jana inaniuma sana, Rais wa wanyonge anawakejeli wanyonge tena wengine wamepoteza ndugu zao huku wakibaki na majonzi ya kupoteza makazi na mali zao halafu anajitokesa huyohuyo aliyesema yeye ni wa wanyonge anawakejeli! Utu uko wapi katika nchi hii!!

Watanzania wenzangu tuamkeni, maamuzi yetu ndio hatima yetu.
 
Usitarajie kuwaondoa madarakani CCM kwa njia ya sanduku la kura

Boss melkiorysaranga ngojea nikukumbushe tu tena. Soma Waebrania 11: 1.

1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Ukweli ni kuwa Wananchi na Watanzania hawajaamua tu. Usichezee kabisa Nguvu ya Umma. Hata Watawala wenyewe wanajua.

Mifano ipo mingi tu.
 
Mtu mwenye sifa ya kusoma na kuandika ana tungaje sheria?
Mbona anajinasibu kuteua maprof, madokt nk?
Hii inaweza kudhihirisha kuwa baadhi ya wateule wake hawana vyeti!
 
ndiyo rais wa wanyonge huyo.
Machafuko na hatimaye Mapinduzi ya nchi fulani Kaskazini mwa Afrika yalanza na kijana mmoja mjasiliamali kunyanyaswa na mgambo. Wananchi wakashika silaha. Walikuwa wanasubiri sababu.

Wananchi wenye silaha za jadi, mawe, nk. wakapata ushindi dhidi ya askari wenye silaha za kisasa.
 
Haaa unbelievable!!

Eti uhakiki haukuwahusu wanasiasa na wateule wa rais bali watumishi wa umma serious??

Kwanza watumishi wa umma ni akina nani?

Mshahara wa wabunge, mawaziri, RCs, DCs ni mali ya nani??

Kumbe ukifoji vyeti ni jinai tu ukiwa mwl, nesi, afisa ugani nk. lakini ni halali ukiwa mwanasiasa au mteule wa rais.

Yaani mimi nakamshahara kangu ambako hakana hata allowance yoyote bali kodi, bodi ya mikopo nk. kwa elimu niliyoipata kihalali nahangaishwa kutwa kucha eti kujiridhisha vyeti vyangu huku wengine wakila kwa vyeti vyenye utata??

Hoja kubwa si kuwa ama kuto kuwa mwanasiasa hoja ni KUGHUSHI, yaani kutenda kosa la KUGHUSHI, teua tu hata akiwa la saba as long as elimu yake haina utata ana haki ya kuteuliwa.

Leo unaweza ona umetuweza watanzania lakini amini hili halitawaacha salama kisiasa, inaonyesha kuna chuki iliyojificha na watumishi.....ndugu zetu wameachishwa kazi a few months kabla ya kustaafu kwa kosa tu la kutumia vyeti vya wengine japo wamefanya kazi muda mrefu halafu eti wengine waendelee kutembelea magari manene na vyeti hivihivyo, unatupa wakati mgumu kuamini dhamira yako kama ni ya dhati, isiyo na uonevu.
Nilwahi kuandika kwenye fbkuwa Bashite atawabeba wahalifu wenzake wa kughushi vyeti. Ndicho kinachotokea! Ulimwengu utatushangaa. What message and impact on our education system has been sent to the public.

It is both unbelieva and unforgettable.
 
Haaa unbelievable!!

Eti uhakiki haukuwahusu wanasiasa na wateule wa rais bali watumishi wa umma serious??

Kwanza watumishi wa umma ni akina nani?

Mshahara wa wabunge, mawaziri, RCs, DCs ni mali ya nani??

Kumbe ukifoji vyeti ni jinai tu ukiwa mwl, nesi, afisa ugani nk. lakini ni halali ukiwa mwanasiasa au mteule wa rais.

Yaani mimi nakamshahara kangu ambako hakana hata allowance yoyote bali kodi, bodi ya mikopo nk. kwa elimu niliyoipata kihalali nahangaishwa kutwa kucha eti kujiridhisha vyeti vyangu huku wengine wakila kwa vyeti vyenye utata??

Hoja kubwa si kuwa ama kuto kuwa mwanasiasa hoja ni KUGHUSHI, yaani kutenda kosa la KUGHUSHI, teua tu hata akiwa la saba as long as elimu yake haina utata ana haki ya kuteuliwa.

Leo unaweza ona umetuweza watanzania lakini amini hili halitawaacha salama kisiasa, inaonyesha kuna chuki iliyojificha na watumishi.....ndugu zetu wameachishwa kazi a few months kabla ya kustaafu kwa kosa tu la kutumia vyeti vya wengine japo wamefanya kazi muda mrefu halafu eti wengine waendelee kutembelea magari manene na vyeti hivihivyo, unatupa wakati mgumu kuamini dhamira yako kama ni ya dhati, isiyo na uonevu.
Utashsngaa wako watu humu jamvini watasifu na kumuona jamaa shujaa....Mkuu aache "double standard"....
 
Hivi nikiwa mojawapo wa waliofoji vyeti nikafukuzwa mh. Akaniteua kuwa RC au Waziri wa Elimu ya Juu inakuwaje hapo?
 
unajua hawa kijani wanadhani huko vijijini watu hawajui kinachoendelea wanajidanganya sana, nimeenda vijijini tabora, mwanza huko aisee, watu mpaka vijijini wana smartphone na wamejiunga kwenye hii mitandao, chochote wanajua na wanabaki kuhuzunika tu, kwani wanajua kijani ndio walioshikilia ni risasi
Kuiamini CCM yataka moyo na kujitoa ufahamu......
 
Mpaka aibu kujiita Mtanzania,
Uzalendo unaisha kabisa.
Hii inasababisha jamii kuzidi kuwa na Chuki dhidi ya Nchi yao.....
Pure double standard..

Hebu vuta picha wale watumishi feki 9000 wanavyokongoroka kwa kuwaza...huku mwenzao Bashiter akitanua kwa fujo zote mjini...

Nawaza tu...'hao wanyonge 9000 si angewafanya kuwa wateule wake ili ngoma iwe droo...tena kiroho safi tu..!

Mwisraeli mmoja huwa anabadilishwa na ma-Palestina zaidi ya 1000 wajameni..
 
unajua hawa kijani wanadhani huko vijijini watu hawajui kinachoendelea wanajidanganya sana, nimeenda vijijini tabora, mwanza huko aisee, watu mpaka vijijini wana smartphone na wamejiunga kwenye hii mitandao, chochote wanajua na wanabaki kuhuzunika tu, kwani wanajua kijani ndio walioshikilia ni risasi
Ingekuwa heri kama upinzani ungeshangilia makosa ya CCM.
 
unajua hawa kijani wanadhani huko vijijini watu hawajui kinachoendelea wanajidanganya sana, nimeenda vijijini tabora, mwanza huko aisee, watu mpaka vijijini wana smartphone na wamejiunga kwenye hii mitandao, chochote wanajua na wanabaki kuhuzunika tu, kwani wanajua kijani ndio walioshikilia ni risasi
Kijani hiyo hiyo ndio imewaletea Smart phone!!
 
Wakati wa kupeana nyumba za dezo serikalini walisema ni kwa ajili ya watumishi wa umma. Wanasiasa wakaja juu na kudai nao pia ni watumishi wa umma na wakapewa nafasi ya kununua nyumba za serikali. Sasa wakati wa kuhakiki vyeti wao sio wafanyakazi wa umma. Warudishe nyumba. Double standard.
Slogan ya Ukawa wakati wa Kampeni sasa nimeielewa....nanukuu...." Lowasaaa, nywele nyeupe, moyo mweupe, Ikulu kweupe, Makufuli tuna vunja, Pombe tunamwaga, Ikulu tunaingia"
Napata shida sana kuelewa mantiki ya kile kinacho imbwa kuwa nina dhamira ya thati ya kuwatumikia Watanzania Maskini!?

Kama kuna wanao adhibiwa na wengine hawaadhibiwi tena kwa makosa yale yale yanayo fanana ni haki kuamini kuna jambo la kheri kweli? Hii kama siyo kukomoa baadhi ya makundi ni nini? Nani yupo juu ya sharia na wengine hawapo?

Binafsi nasononeka sana kwa kweli, tumeimba sheria ni kama msumeno hukata mbele na nyuma (kote kote) ila msemo huu si lolote kwa wakati huu.

Haki iko wapi? Nani mpenzi wa Mungu kama matendo hayaakisi hilo? Uzuri Mwenyezi yeye ndiye anaye jua anaye mtumikia na asiye mtumikia iwe kwa maneno ama kwa vitendo.

Mzee 'Makwaiya' alikuwa na kipindi chake akiuliza Je, Tutafika? Nadhani hapa sasa ndiyo mahali sahihi pa kuuliza swali hili kuliko huko nyuma.

Kama siyo una. sielewi.
 
Kijani hiyo hiyo ndio imewaletea Smart phone!!
Smartphone kwa sasa zipo kila kona ya Dunia, hayo ni matokeo ya utandawazi tu.
Lakini wenzetu wako mbali sana kimaendeleo sio sisi tunajimilikisha simu za kisasa eti nako tuseme tumeendelea!!?
 
Back
Top Bottom