Kwa hili Rais Magufuli usije kumtafuta mchawi!!

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,976
3,127
Haaa unbelievable!!

Eti uhakiki haukuwahusu wanasiasa na wateule wa rais bali watumishi wa umma serious??

Kwanza watumishi wa umma ni akina nani?

Mshahara wa wabunge, mawaziri, RCs, DCs ni mali ya nani??

Kumbe ukifoji vyeti ni jinai tu ukiwa mwl, nesi, afisa ugani nk. lakini ni halali ukiwa mwanasiasa au mteule wa rais.

Yaani mimi nakamshahara kangu ambako hakana hata allowance yoyote bali kodi, bodi ya mikopo nk. kwa elimu niliyoipata kihalali nahangaishwa kutwa kucha eti kujiridhisha vyeti vyangu huku wengine wakila kwa vyeti vyenye utata??

Hoja kubwa si kuwa ama kuto kuwa mwanasiasa hoja ni KUGHUSHI, yaani kutenda kosa la KUGHUSHI, teua tu hata akiwa la saba as long as elimu yake haina utata ana haki ya kuteuliwa.

Leo unaweza ona umetuweza watanzania lakini amini hili halitawaacha salama kisiasa, inaonyesha kuna chuki iliyojificha na watumishi.....ndugu zetu wameachishwa kazi a few months kabla ya kustaafu kwa kosa tu la kutumia vyeti vya wengine japo wamefanya kazi muda mrefu halafu eti wengine waendelee kutembelea magari manene na vyeti hivihivyo, unatupa wakati mgumu kuamini dhamira yako kama ni ya dhati, isiyo na uonevu.
 
Magufuli ni JANGA KUBWA LA TAIFA. Ndani ya mwaka mmoja tu amepindisha sheria mbali mbali za nchi bila kujali athari ya kufanya hivyo. Ndani ya miaka mingine minne sijui nchi yetu itakuwa ina hali gani kwa huu upindishaji wa Sheria za nchi uliokithiri.
 
unajua hawa kijani wanadhani huko vijijini watu hawajui kinachoendelea wanajidanganya sana, nimeenda vijijini tabora, mwanza huko aisee, watu mpaka vijijini wana smartphone na wamejiunga kwenye hii mitandao, chochote wanajua na wanabaki kuhuzunika tu, kwani wanajua kijani ndio walioshikilia ni risasi
 
Hebu vuta picha wale watumishi feki 9000 wanavyokongoroka kwa kuwaza...huku mwenzao Bashiter akitanua kwa fujo zote mjini...

Nawaza tu...'hao wanyonge 9000 si angewafanya kuwa wateule wake ili ngoma iwe droo...tena kiroho safi tu..!

Mwisraeli mmoja huwa anabadilishwa na ma-Palestina zaidi ya 1000 wajameni..
 
Back
Top Bottom