Kwa hili Polisi Watuelimishe; Kuna Sheria ya Diamond na ya Wengine?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,319
72,742
Miezi kadhaa iliyopita vijana watatu mkoani Singida walijirekodi video wakiendesha gari, huku wakicheza wimbo wa Darasa (Muziki). Hali hiyo ilimfanya dereva kuachia usukani na kuserebuka. Baada ya video hiyo kutoka haraka sana walitafutwa na wakashtakiwa kwa reckless driving

Siku kadhaa zilizopita msanii Diamond Platnumz alijirekodi video akiendesha gari, huku akiwa ameachia usukani na bila kufunga mkanda, akicheza. Kosa hili ni mfanano na lile la vijana wa Singida (reckless driving). Lakini Diamond ameitwa makao makuu ya jeshi la Polisi, akakutana na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, akaandika maelezo, akalipa faini, kisha akapiga picha na Kamanda Mpinga. .!

Unaelewa nini??
Ameandika Malisa G..
Hebu na sisi tuliangalie limekaaje?

179b75d630191b8f5d1ac472221c083a.jpg
 
Miezi kadhaa iliyopita vijana watatu mkoani Singida walijirekodi video wakiendesha gari, huku wakicheza wimbo wa Darasa (Muziki). Hali hiyo ilimfanya dereva kuachia usukani na kuserebuka. Baada ya video hiyo kutoka haraka sana walitafutwa na wakashtakiwa kwa reckless driving na kuhukumiwa miezi 6 jela.

Siku kadhaa zilizopita msanii Diamond Platnumz alijirekodi video akiendesha gari, huku akiwa ameachia usukani na bila kufunga mkanda, akicheza. Kosa hili ni mfanano na lile la vijana wa Singida (reckless driving). Lakini Diamond ameitwa makao makuu ya jeshi la Polisi, akakutana na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, akaandika maelezo, akalipa faini, kisha akapiga picha na Kamanda Mpinga. .!

Unaelewa nini??
179b75d630191b8f5d1ac472221c083a.jpg

Ameandika Malisa G..
Hebu na sisi tuliangalie limekaaje?
Animal farm.
All animals are equal, but some animals are more equal than others.
 
mbona wa Tanzania kila kitu hatutaki ukweli,
Wale vijana walishindwa kulipa faini kulingana na makosa waliosomewa.
kuna kanuni na taratibu za kufuata mtu akitenda kosa na kushindwa kulipa faini kulingana na kosa husika

Hawa walikamatwa kwanza kisha wakawekwa mahabusu, wakapelekwa Mahakamani na wakasomewa mashtaka. Hebu niambie, katika hili, utaratibu huu umefuatwa?.
 
mbona wa Tanzania kila kitu hatutaki ukweli,
Wale vijana walishindwa kulipa faini kulingana na makosa waliosomewa.
kuna kanuni na taratibu za kufuata mtu akitenda kosa na kushindwa kulipa faini kulingana na kosa husika

Tujiepushe na uongo. Kweli dereva anaweza kukubali kufungwa miezi sita kwa kushindwa kulipa 30000 au 60000?
Haiwezekani hata utingo kumkopesha 20000?
 
It is a pure double standard. Domond alipaswa kuwekwa rumande na kushtakiwa badala ya kulipishwa faini ya elfu sitini na kupiga picha na Kamanda Mpinga. Akakamatwe!
Sheria inatoa option ya kulipa faini au kutumikia kifungo. Kama huna hela ya kulipa faini unatumikia kifungo. No double standard, ni suala la sheria tu.
 
Nilikuwa najiuliza sana jinsi hawa jamaa wanavyosimamia mambo yao nikafikiri labda ni baadhi, sasa nimepata picha! Sitabishana tena na trafiki, akitaka leseni nampa, akipiga faini nampa labda akitaka nimuachie gari hapo ndio sitakubali.
 
Back
Top Bottom