Kwa hili Obama Kachemsha

akili

Member
May 5, 2008
68
0
Nimekuwa nikimuunga Obama toka siku ya kwanza. Lakini hili la kuanza kushikamana na upande mmoja linanikifu. Na siamini kama litakuwa na mwisho mzuri. Obama kutoa silaha kwa upande wowote katika mgogoro wowote Afrika ni kuanza kile ambacho Afrika inakiogopa kutoka kwenu. Ukifungua njia wewe basi wauza silaha wako wote ndio utakuwa umewaruhusu kumwaga silaha zao barani hapa na kutuachia kama yale mliyoyafanya kule Amerika ya Kati na Kusini, Vietnam na kwingineko Asia. Munge apishilie hilo mbali.

Dawa ya Somalia iko ndani ya Somalia yenyewe na ndugu zao Waislamu. Mkono wa Marekani Somalia nina hakika ni mkoma ambaye hakubaliki hata iwe nini. Unaowasaidia watashindwa na ndio mwanzo wa kuanza kujiaibisha Afrika na kwingineko.

Somalia ni moto wa kuotea mbali ndugu yangu. Hawa ni watu ambao kisasi chao hakiishi milele. Na hakuna adui mbaya kama mtu ambaye hajui kusahau ubaya aliofanyiwa na anataka revenge. Hukumbuki yaliyowapata Wamarekani Somalia mara baada ya kuondoka Siad Barre ndugu yangu. Na wewe hivi hivi unaona na unakubali kushauriwa na wajinga wanaodhani Somalia ni sawa na sehemu nyingine duniani na unakubali. Haya ngoja muanze kutumiwa salamu maana mmeyataka wenyewe wallahi.

Na nyie Waburundi na Waganda hivi mna njaa kali kiasi hicho hadi kukubali kutumika kama canon fodder ???
 
Kiongozi,
Toa overview ya jambo unalotaka kulisema kwanza ili wajumbe wafahamu unarefer to events gani exactly.
 
Unajua mkuu Marekani siyo kama baadhi ya nchi zetu Africa. Raisi wa Marekani hafanyi vitu kutokana na opinion zake tu bali na kufuata washauri wake. Ni vigumu kwa nchi kama Marekani kubaki neutral kwenye mambo mengi. Mfano mzuri ni mambo yanayo tokea Iran. Mkulu Obama akawa kimya na kuja kutoa tamko akatoa tamko ambalo lipo very neutral. Kufanya hivyo viongozi wengine Marekani wakamjia juu. So in many cases if America has to take a side raisi anashauriwa what side is better to take. So I don't think the blame should be entirely on Obama bali unabidi pia uangalia na the forces within American politics itself. Kama Marekani kupitia past administrations walishakuwa na position regarding Somali yeye hawezi kuja ghafla na kubadilisa muelekeo.
 
Last edited by a moderator:
Unajua mkuu Marekani siyo kama baadhi ya nchi zetu Africa. Raisi wa Marekani hafanyi vitu kutokana na opinion zake tu bali na kufuata washauri wake. Ni vigumu kwa nchi kama Marekani kubaki neural kwenye mambo mengi. Mfano mzuri ni mambo yanayo tokea Iran. Mkulu Obama akawa kimya na kuja kutoa tamko akatoa tamko ambalo lipo very neutral. Kufanya hivyo viongozi wengine Marekani wakamjia juu. So in many cases if America has to take a side raisi anashauriwa what side is better to take. So I don't think the blame should be entirely on Obama bali unabidi pia uangalia na the forces within American politics itself. Kama Marekani kupitia past administrations walishakuwa na position regarding Somali yeye hawezi kuja ghafla na kubadilisa muelekeo.

Kiongozi,
unachosema ni kweli kabisa kwa asilimia 100. Hata hivyo kupokea lawama kwa niaba ya umma ni mojawapo ya majukumu ya Rais. Hivyo kama sera inaonekana haifai, ''rafiki yetu'' Obama inabidi abebeshwe tu mzigo wa lawama.
Ukweli ni kwamba Obama anajitahidi sana kuogolea upande tofauti na mkondo.
Marekani ni cnhi ambayo imejengwa katika misingi ya kinyang'anyi na kinyonyaji kwa karne kadhaa. Iwapo Obama ataamua kutoka moja kwa moja kwenye utamaduni huo wa serikali za Marekani, kitakachotokea ni kwamba uchumi wa nchi utaanguka na Marekani itapotea kwenye sura za mataifa makubwa duniani. Sidhani kama Obama au mmarekani yeyote anaweza kukubaliana na matokeo hayo, ndio maana Obama ataendeleza sera za kinyang'anyi za Marekani. Anachoweza kuboresha ni mtindo tu watakaokuwa wakiutumia katika unyang'anyi wao hivi sasa.
Imetia matumaini kuona Obama anafikiri alternative energy sources. Hii in my view itawezesa kwa kiasi kikubwa Marekani kupunguza ulazima wa unyang'anyi ambao ndio unasimamisha uchumi wa Marekani hivi sasa.
 
Absolutely right mkuu. Tatizo ni status quo. Marekani haiwezi kubadilisha na mtu mmoja because ya system yao ya checks & balances. Which means what ever policies he decides to push he can't do so kama the other branches of government hazitaki. Sawa Obama wants change but taizo ni do his fellow leaders belive in his vision? Kama ulivyo sema mkuu historia ya power ya Marekani ni kufanya by any means possible to promote their interests. Tatizo ndiyo hilo mkuu kuwa ukiwa raisi you take the heat for everything. Ila nadhani ni busara kwetu kutokujipa matumaini sana kuwa Obama will change America.
 
Serikali ya Marekani in Sera zake hata kama aje Obama, Bush au nani atafuata hizo hivyo kuhusu Somalia inachukuliwa kama taifa la uovu na kuwekwa katika list ya Nchi Hatari kabisa, Na ndio maana walikimbia huko
 
Nimekuwa nikimuunga Obama toka siku ya kwanza. Lakini hili la kuanza kushikamana na upande mmoja linanikifu. Na siamini kama litakuwa na mwisho mzuri. Obama kutoa silaha kwa upande wowote katika mgogoro wowote Afrika ni kuanza kile ambacho Afrika inakiogopa kutoka kwenu. Ukifungua njia wewe basi wauza silaha wako wote ndio utakuwa umewaruhusu kumwaga silaha zao barani hapa na kutuachia kama yale mliyoyafanya kule Amerika ya Kati na Kusini, Vietnam na kwingineko Asia. Munge apishilie hilo mbali.

Dawa ya Somalia iko ndani ya Somalia yenyewe na ndugu zao Waislamu. Mkono wa Marekani Somalia nina hakika ni mkoma ambaye hakubaliki hata iwe nini. Unaowasaidia watashindwa na ndio mwanzo wa kuanza kujiaibisha Afrika na kwingineko.

Somalia ni moto wa kuotea mbali ndugu yangu. Hawa ni watu ambao kisasi chao hakiishi milele. Na hakuna adui mbaya kama mtu ambaye hajui kusahau ubaya aliofanyiwa na anataka revenge. Hukumbuki yaliyowapata Wamarekani Somalia mara baada ya kuondoka Siad Barre ndugu yangu. Na wewe hivi hivi unaona na unakubali kushauriwa na wajinga wanaodhani Somalia ni sawa na sehemu nyingine duniani na unakubali. Haya ngoja muanze kutumiwa salamu maana mmeyataka wenyewe wallahi.

Na nyie Waburundi na Waganda hivi mna njaa kali kiasi hicho hadi kukubali kutumika kama canon fodder ???

How good is your International Relations?
 
Marekani itaendelea kuwa hivyo kwa Somalia kwa Muda na Hata kufadhili magaidi huko Somalia kwa ajili ya manufaa yake yenyewe. Kumbuka kuwa Marekani ndio imeifanya Somalia kuwa hivi ilivyo.
 
Unaweza kulinganisha Obama na Kikwete ,kuingia kwao kwenye madaraka ilikuwa kwa mbwembwe na hata matarajio ya wengi ni kuweka maisha bora kwa kila mwananchi ,sasa pima mabadiliko ya uongo'zi wao kila siku zinavyozidi.Wenyewe wanajiita watoto wa mjini ,misafara na showing kibao.
 
Sijaelewa ni uamuzi upi wa Obama unaupinga. Labda link ya huo uamuzi ungesaidia.
 
Juzi congress iliambiwa kuwa wameamua kuwasaidia serikali iliopo madarakani ya Somalia na mpaka jana jamaa walikutana na wahusika kule stste dept kulizungumzia hili kwa undani zaidi
 
Somalia hali ilivyo ni mfano wa hell on earth. Hali ni mbaya na wasomali wameshindwa kuutatua. They need help. Jitihada zozote za kuwasaidia wasomali kuutatua ule mgogoro ni jambo zuri.

Wamarekani wanajitahidi kutafuta suluhu kule Somalia. Inawezekana juhudi zao tunafikiria si sahihi. Lakini ni nani anayefanya kingine zaidi? Nchi zingine zote wako happy na wametulia tu na kuangalia kinachoendelea somalia na wanadhani hakiwahusu. Wengine mchango wao ni huu huu wa kulalamika tu na kukosoa pale wengine wanapojaribu.

Nadhani wasomali wanahitaji msaada kutoka kwa yeyote anayejali. Wamarekani wanaisaidia serikali ya sasa iweze kusimama. Wengine wanawasaidia kina nani??
 
Obama itamchukua Muda mrefu sana kubadili Sera ya Mambo ya Nje ya America na hivyo kufanya hivyo ilivyo Leo. America Foreign Policy is Dead man
 
Au hii ni Abstract??? Ila imekaa nusu nusu hii habari. Hebu weka mambo kamili tuelewe.
 
Pia kumbukeni kuwa Al-Qaida wanatumia ombwe la utawala wa kisheria nchini Somalia kufanya mambo yao. Yule Mkomoro anayetafutwa, mfuasi wa Bin Ladin nasikia kajichimbia huko.
 
Obama akifanya hivyo basi jua wamerikani wengi sana wataona wanamwmabia kuwa anataka urafiki na Somalia.
 
Nimepachika vipande vipande vya habari inayohusu US/Somalia

The Obama administration has begun sending arms aid to the beleaguered government of Somalia, officials said Thursday, in an escalation of its commitment to one of the world's most troubled states.

State Department officials said the support was intended to help sustain a transitional government that is steadily losing ground to Islamic militants in fighting that has been catastrophic for civilians. The administration also is stepping up humanitarian aid to the country, said officials, who declined to disclose how much would be spent
U.S. officials and their allies worry that a victory by the hard-line Shabab militant group and other insurgents would further destabilize the region, and make Somalia a haven for international terrorist groups.

In early May, the al-Shabab and Hizbul Islam militias launched a new offensive in Mogadishu in an effort to topple the internationally-backed transitional government of President Sheikh Sharif Sheikh Ahmed. The insurgents reject the government's brand of Islamism as too moderate and want African Union peacekeepers to leave the country

Factors
American Interest
1) The goal is to stem Islamic insurgent advances in the Horn of Africa
2) Somali pirates have intensified their attacks in the Gulf of Aden, carrying out attacks on over 111 commercial ships.

Kwa picha ilivyo Somalia ungekuwa kwenye hiyo nafasi ya Obama, ungefanya nini?
Hivi Somalia kuna shule?
 
Mkuu swala la Obama kutoa silaha Umelitoa wapi hebu tupe link uliyosoma au kusikia habari hiyo.Au umeamua tu kuandika
 
Back
Top Bottom