Kwa hili nina kila sababu ya kulizungumzia

Wilson Gamba

Verified Member
Mar 1, 2013
600
500
Habari za siku wana jamvi? Ni mda mrefu nilikuwa sitoi mchango wangu huku jukwaani hii ni kwa kutingwa na majukumu.Leo naomba niwaletee hili la dada zetu kuwa na viburi,kejeli kwa bwana zao na madhara yake.

Ni juzi tu nilikuwa niko safari na nilipofika Ubungo majira ya saa tano usiku nilianza ona ongezeko la watoto wengi wakipigania mabox ya kulalia,huruma ilinishika sana kwa kuwa nilikuwa nimekaa karibu na mama mmoja kwenye benchi kwenye jumba la wasafiri tulianza kuliongelea la watoto kuwa mtaani ili hali wamezaliwa na wazazi tulienda mbali zaidi akanieleza kuwa ili linachangiwa zaidi na kina dada wengi ambao wanakimbiwa na wanaume mara baada ya kujifungua kutokana kutokuwa makini kataka kuishi na bwana zao na hivyo kupelekea kutomdu malezi ya watoto na hivyo watoto kukimbilia mitaani.

NACHOKIOMBA NINAOMBA DADA ZETU TUWE NA NAMNA NJEMA YA KUISHI KATIKA NDOA NA KUVUMILIA NA PIA SISI AKINA BABA NAOMBA TUWA HURUMA KWA WANETU TUNAOZAA HATA KAMA UNA MATATIZO NA MAMA MWANAO HANA KOSA MTUNZE KTK MALEZI MAZURI NA KUMPA MAHITAJI MUHIMU KMA VILE ELIMU ,MALAZI, CHAKULA NA MAPENDO.

MUNGU AWABARIKI
 
mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
5,815
2,000
tatizo ni wanawake wanabeba mimba bila kutarajia na wanabebeshwa hata na mtu wasiyemjua vizuri ,
 
Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
52,940
2,000
Mmmmh kesho pia useme na wanaume wanaojaza watoto wa watu mimba tena wengine wanafunzi then wanakataa....
Pia useme na wale wanaume wanaojifanya wastaarabu wananing'iniza na tai kabisa then wanaenda kuwajaza mimba wanawake wale wanye ulemavu wa akili/viungo na wale ombaomba....either kwa sababu ya mitamaa yao au ushirikina then wanakaa mbali.....
Usisahau wale wenye michepuko...wakiona imeshika mimba wanaitelekeza kwa kuogopa kugaribu ndoa zao...... Nadhani hawa nao wanachangia hili tatizo kwa asilimia kubwa
 
halati88

JF-Expert Member
Apr 4, 2014
461
195
Mmmh hapana sio kweli kama hiyo ndio sababu basi kwa asilimia ndogo sana.
 
Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,542
1,225
Chukua mtoto mmoja ikiwa uwezo unaruhusu, ni baraka isiyosahaulika zaidi.
^^
 
PesaNdogo

JF-Expert Member
Jun 19, 2013
1,996
2,000
Habari za siku wana jamvi? Ni mda mrefu nilikuwa sitoi mchango wangu huku jukwaani hii ni kwa kutingwa na majukumu.Leo naomba niwaletee hili la dada zetu kuwa na viburi,kejeli kwa bwana zao na madhara yake.

Ni juzi tu nilikuwa niko safari na nilipofika Ubungo majira ya saa tano usiku nilianza ona ongezeko la watoto wengi wakipigania mabox ya kulalia,huruma ilinishika sana kwa kuwa nilikuwa nimekaa karibu na mama mmoja kwenye benchi kwenye jumba la wasafiri tulianza kuliongelea la watoto kuwa mtaani ili hali wamezaliwa na wazazi tulienda mbali zaidi akanieleza kuwa ili linachangiwa zaidi na kina dada wengi ambao wanakimbiwa na wanaume mara baada ya kujifungua kutokana kutokuwa makini kataka kuishi na bwana zao na hivyo kupelekea kutomdu malezi ya watoto na hivyo watoto kukimbilia mitaani.

NACHOKIOMBA NINAOMBA DADA ZETU TUWE NA NAMNA NJEMA YA KUISHI KATIKA NDOA NA KUVUMILIA NA PIA SISI AKINA BABA NAOMBA TUWA HURUMA KWA WANETU TUNAOZAA HATA KAMA UNA MATATIZO NA MAMA MWANAO HANA KOSA MTUNZE KTK MALEZI MAZURI NA KUMPA MAHITAJI MUHIMU KMA VILE ELIMU ,MALAZI, CHAKULA NA MAPENDO.

MUNGU AWABARIKI
Watoto wa mtaani kwa sehemu kubwa ni matokeo ya baba zao, na wataendelea kuongezeka kutokana na tabia ya vijana wengi kutokubali majukumu pale wapenzi wao wanapata mimba na hili wimbi la jamii kupokea tabia ya kuwa na wapenzi wengi kama jambo la kawaida watu wanazaa kila mahali watu tofauti tofauti
 
Diva Beyonce

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
12,927
2,000
Wanaume wa siku hizi majanga kwahyo mtu akitofautiana na mkewe mwanaume unakimbia hafu unakuja kusingizia wanawake really! Does it make sense? Nyie ndo mnakimbia majukumu yenu hapo kila mtu awe responsible kwenye majukumu yake
 
Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
987
1,000
wanawake wana kalenda zao ila hata hawazijui. Mwanamke akiamua asipate mimba (zisizotarajiwa) anaweza ila wengi wapo wapo tu, Hivi kweli jamaa ako ameomba gemu, siku hyo mwanamke atajikagua kote lakini hukagui kalenda unategemea nn?
 
guasa

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
1,867
0
wewe umekataa wangapi? kosa la mzazi unambebesha mtoto? hizi research ubora wake uangaliwe!
 
kamagetac

JF-Expert Member
Jul 25, 2014
2,478
2,000
Mbona lawama umewapa wadada? Hivi jukumu la kulea katika ndoa ni wadada tu? Mmmmmm!!! kama ni hivyo ndoa zitaendelea hivyo
 
sofina

Member
Aug 29, 2014
85
95
Hiyo ni moja ya sababu,lkn sio kwamba sababu hiyo tu ndio inasababisha hivyo hayo majanga
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom