Kwa hili ni Lowassa pekee anayeweza kuleta mabadiliko Tanzania

Mwangaza

Senior Member
Feb 26, 2008
198
64
Wadau,

Wote tunajua katiba ya Wananchi ilivyojaa matakwa ya wananchi, ambayo Mh.Lowassa AMEAHIDI KURUDISHA RASIMU HII YA WANANCHI na tuweze kuapata Katiba bora ya Wananchi itakayotuvusha miaka mingi ijayo kwa HAKI NA USAWA ndipo tutapa AMANI YA KWELI, lakini Magufuli wala chama chake hawajawahi kuahidi hili wala halipo kwenye ilani ya chama.

Hivyo HAWAWEZI KULETA MABADILIKO YA KIKATIBA TUNAYOTAKA, Katiba ndio sheria mama inasimamia kila kitu kwenye nchi kuanzia Elimu, Rasilimali, Utawala,Uadilifu, Haki na Usawa-Amani, nk..kwa maana magfuli hataweza kuleta mabadiliko kwenye Katiba.

Moja kwa moja ni kwamba HAWAWEZI KULETA MABADILIKO TZ.Tumeona nchi mbalimbali ambapo katiba ni mbovu,mabadiliko ya kikatiba lazima yafanyike. mfano Kenya mabadiliko yao yaliendana na kubadilisha Katiba pia.

HAPA TUNA KILA SABABAU YA KUMCHAGUA MH.LOWASSA..

Karudishwa kwa katiba ya Wananchi kutatulelea mengi, ambayo maccm wameyaondoa kwa ubinafis wao, kama haya..

1. Kupunguzwa kwa madaraka ya rais
-Katiba ya CCM imeyafuta haya na imemwongezea Rais madaraka.

2. Kutenganisha mamlaka ya mihimili ya dola

-Katiba ya Wananchi ililipa Bunge mamlaka zaidi kuisimamia Serikali na hata pale ambapo Bunge lingekataa bajeti au muswada mbaya wa Serikali mara kadhaa, rais asingeliweza kulivunja Bunge. Katiba ya maccm imeliondo hili.

3. Mawaziri wasitokane na wabunge,
-Wananchi walipendekeza hili ili wabunge wafanye kazi ya uwakilishi pekee na mawaziri watumie weledi wao kumsaidia rais kazi za Serikali.

Katiba ya CCM imefuta masharti haya.

4. Kumwajibisha mbunge
Katiba ya CCM imefuta hili.hawatakaki tuwawajibihe wabunge wanaposhindwa kutuwakilisha.

5. Vyanzo vya mapato vya kuaminika

6.Muundo wa shirikisho lenye mamlaka kamili

7. Kupunguza ukubwa wa Serikali

-Rasimu ya Warioba ilisema idadi ya mawaziri isizidi 15.
Katiba ya CCM inasema mawaziri wasizidi 40, pendekezo hili halina uhalisia kwa sababu Serikali ya Muungano itashughulika na mambo ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano ya Tanganyika/ Tanzania Bara na kuifanya kuwa KUBWA ZAIDI na hivyo kuhitaji mawaziri zaidi ya 40, NA KUONGEZA GHALAMA bure kabisa.

8.Kupunguza ukubwa wa Bunge

Ya Wananchi ilipendekeza idadi ya wabunge isizidi 75, Ya maccm imekwa wabunge wasipungue 340 na wasizidi 390...HUU NI UPOTEVU WA KODI BURE KABISA.

9. Ukomo wa vipindi vya ubunge
- CCM wamenyofoa kipengele hichi.

10. Kuwapo kwa tunu za Taifa
Tunu hizi ni pamoja na utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya Taifa. Raia wa Tanzania walikuwa na wajibu wa kuheshimu tunu hizi lakini Katiba ya maccm imezifuta tunu hizi.

11. Maadili na miiko ya viongozi
Katiba ya wananchi imesema maadili na miiko kwa viongozi (mathalan kutenganisha biashara na uongozi ili kuepusha mgongano wa masilahi), isiwamo kwenye Katiba bali ikawekwe kwenye sheria.

14. Usawa wa 50:50 kati ya wanawake na wanaume
Katiba ya CCM imefutilia mbali pendekezo hili muhimu

15. Kuanzishwa kwa mgombea huru
Katiba ya CCM imefutilia mbali pendekezo hili muhimu

17. Uhuru wa Mkuu wa Jeshi la Polisi
Rasimu ya Wananchi ilipendekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi atekeleze kazi zake kwa uhuru, bila woga, upendeleo wala chuki na kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria za nchi. Masharti haya yamefutwa na Katiba ya CCM.

18. Ukomo wa vipindi vya ubunge
Rasimu ya Wananchia iliweka ukomo wa vipindi vya ubunge kuwa vitatu na kuwa na ukomo wa miaka 15 kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Maccm wamefuta pendekezo hili.

19. Kuanzishwa kwa mgombea huru

Rasimu ya wananchi ilitoa haki ya mgombea huru bila vikwazo, Katiba ya maccm imeweka masharti magumu ambayo hakuna mtu anayeweza kuyatimiza kirahisi, kitendo hiki siyo sawa.


20. Uhuru wa Mkuu wa Jeshi la Polisi

Rasimu ya Wananchiilipendekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi atekeleze kazi zake kwa uhuru, bila woga, upendeleo wala chuki na kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria za nchi. Masharti haya yamefutwa na kwenye katiba ya CCM.

BILA LOWASSA HAKUNA MABADILIKO..TUSIDANGANYIKE.

CHAGUA LOWASSA ....KWA MABADILIKO YA KWELI.
 
Tusidanganyike -- ni lowassa pekee awezaye kuleta mabailiko

chagua mabadiliko

chagua lowassa
 
kwa kuwa tunaongozwa na chuki binafsi na ujinga people are ready to TRADE ''wananchi`s katiba'' for a ''proclaimed'' ''Mr.Clean''
 
Tusifanye kosa kuiacha CCM madarakani, itakuwa kosa kubwa sana ambalo tutajutia maisha yetu yote
 
ndo maana vipaumbele vyake ni elimu ili hawa jamaa waliopata phd na hawajui sadam alikua rais wa wapi wakasome
 
Back
Top Bottom