Kwa hili naamini kwa dhati Dr. Slaa hakuonyesha ukomavu wa kisiasa

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Katika vita yeyote ile ni kosa la jinai kufanya tendo lolote linalo imarisha mshikamano ndani ya kambi ya adui. Hii inatokana na ukweli kwamba adui wanapoanza kuzozana wao kwa wao wanatoa fursa nzuri kwa upande wa pili kuwatokomeza.

Kosa la aina hiyo ndilo alilofanya Dr. Slaa huko Tabora alipotoa nyongeza kwenye orodha ya mafisadi papa, na vile vile alipomtaja mtoto wa JK ya kuwa anao utajiri mkubwa usioelezeka. Madai hayo yamesababisha uongozi wa juu wa CCM, usitishe hatua uliokusudia kuwachukulia mapacha watatu, kwa lengo la kuepusha upanuaji wa uwanja wa mapambano.

Katika hali hiyo kauli hizo za daktari zimesaidia kuepusha mfarakano mkubwa ndani ya CCM, jambo ambalo lingelisogeza karibu kusambaratika kwa chama hicho.
 
That was a very good strategy,
gamba nimegoma kung'oka,
wananchi watabaki mdomo wazi,
yaani hata presida! kasindwa?
hukumu 2015.
 
Duh,mwisho wa siku ndo tutajua effect zake,..tukiona matokeo
1.yawezekana ni kweli kabisa kwamba amewahi kuwastua na wao wakaahirisha
2.yawezekana nia yake ni wao waendelee kutunza kansa yao ili kifo choa kiwe cha ghafla!

Tusubiri
 
Muungwana si na yeye kaingizwa na magamba bila hivyo alikua awe Salim A Salim
 
Nilisema siku moja humu. Dr Slaa anaisaidia sana CCM kwa "breaking news" zake. Najua anapewa taarifa nyingi tu kwa kuaminiwa na Watanzania sasa. Sidhani kama kuwataja hadharani kumeisaidia Tanzania na Watanzania. Bado watu wanaendelea kuhomola kwa saana tu.
 
inatakiwa zaidi ya kuwataja ...serikali ina jukumu la kuwachulia hatua,baada ya kuwachunguza
 
Moto uendelee tuu, mpaka kieleweke kanga kunyonyolewa manyoya aka magamba!!
 
Katika vita yeyote ile ni kosa la jinai kufanya tendo lolote linalo imarisha mshikamano ndani ya kambi ya adui. Hii inatokana na ukweli kwamba adui wanapoanza kuzozana wao kwa wao wanatoa fursa nzuri kwa upande wa pili kuwatokomeza.

Kosa la aina hiyo ndilo alilofanya Dr. Slaa huko Tabora alipotoa nyongeza kwenye orodha ya mafisadi papa, na vile vile alipomtaja mtoto wa JK ya kuwa anao utajiri mkubwa usioelezeka. Madai hayo yamesababisha uongozi wa juu wa CCM, usitishe hatua uliokusudia kuwachukulia mapacha watatu, kwa lengo la kuepusha upanuaji wa uwanja wa mapambano.

Katika hali hiyo kauli hizo za daktari zimesaidia kuepusha mfarakano mkubwa ndani ya CCM, jambo ambalo lingelisogeza karibu kusambaratika kwa chama hicho.

Yaani unamlaumu Dr. Slaa kwa kushindwa kuongoza kwa viongozi wa CCM..? Lini watawajibika kwa udhaifu na makosa yao wenyewe?
 
A%20S%20cry.gif
Move ya Dr. Slaa naona ilikuwa a very good one, kwanza kwa CCM kukubali kuwa waliotajwa na Slaa ni kweli walikuwa mafisadi ni hatua kubwa sana maana huko nyuma walishakataa mpaka kutishia kumpeleka mahakamani (hapo serikali imedhihirisha kuwa inadanganya wananchi wake). Kwa Dr. Slaa kutaja list ya pili imewachanganya CCM maana imejikuta inatakiwa kujisafisha si kwa watu watatu tu bali ni wengi na hata wale ambao tunawaamini kwa utendaji wao, na kama walikubaliana na listi ya kwanza kwa nini na listi ya pili isiwe kweli? wananchi tutajuaje kama serikali inatudanganya tena? Kikubwa CCM inachotakiwa kufanya ni mabadiliko ya hali ya juu kitu ambacho sikioni kinafanyika zaidi ya propaganda. Propaganda waliyotaka kuileta ni kuwa wamejisafisha na ufisadi na kuwa sasa ni wasafi, lakini wamejikuta hawawezi fanya hivyo na hasa baada ya kushindwa hata kuwachukulia hatua wale ambao walishakiri kuwa ni mafisadi, kwa kweli tukiendelea kukichekea na kukishabikia chama hichi basi sie kweli tutakuwa WaDanganyika kweli. Lets do something for our beloved country, either upo CCM au CDM, lets clean our house(serikali) mafisadi wanatuua na kutufanya masikini pasipo sababu. Lets do something and be a change
A%20S%20cry.gif
 
Title yako ndo sijaielewa "Kwa hili naamini kwa dhati Dr. Slaa hakuonyesha ukomavu wa kisiasa" Hapa unamaanisha kuwa Dr. Slaa si mkomavu kisiasa ndo maana hakuuonyesha au ni mkomavu na hakuuonyesha ukomavu wake????

Dr. Katimiza wajibu wake, kazi ya kusubiri hatua zipi/gani CCM wachukue hili halimuhusu.
 
Baada ya list ya mafisadi ya Dr Slaa:
1. Mramba, Daniel Yona na Mgonja walifikishwa mahakamani (hata kama ni kwa danganya toto)
2. Hatimae CCM wamekiri wana magamba. Walao wamekubali RA, EL na EC ni mafisadi

Haya yoote yasingetokea iwapo Dr. na CDM wasingefanya vitu. Sasa wewe unataka ukomavu gani wa kisiasa? Au na wewe gamba?
 
alichokifanya Dr. Slaa ni mtaji mkubwa wa kesho (2015). Kuongeza orodha ya pili ya mafisadi kumewafanya ccm washindwe kutekeleza walichokuwa wakijigamba nacho, na hivyo, kuwaonesha wananchi ukweli kuwa ccm ni waongo, mafisadi,na watu wapropoganda. Itakuwa vigumu ccm kuwashawishi wananchi kuwa RACHEL sasa ni wasafi wakati walisema hadharani kuwa ni wachafu na "wanajivua gamba". Hii inaongeza credit kwa CDM kuwa ccm siyo watu wa kuamniniwa kutawala tena!!!
 
Katika hili nadiriki kusema kua Dr. Silaa umezidi kuonyesha kua huna DIRA na kamwe hufai kuwa RAISI
 
hivi hizi analysis mnazifanyaje? kwamba kawaimalisha?

1. Inazidi kuprove kuwa CCM hawawezi kuendelea bila Mafisadi, ndio wano-control chama
2. wananchi watazidi kuvunja Imani na CCM, manake na mbwebwe zote za siku 90, wao wenyewe wanapingana
3. tatizo kubwa la umaskin ni ufisadi, Mnyonge gani atakubali kuchagua fisadi kuwa Raisi?
4. that was a very good strategy i think....inaprove kwa CCM wenyewe an wananchi kuwa hawawezi kujivumbua, kujivua mens CCM ife
 
suala la kuwatoa mapacha watatu ccm halitekelezek.....sio kwamba wameshindwa fanya hivo coz of that second list from dr....hiyo imetumika kama kisingizio tu....CCM wanajichimbia kaburi lao wenyewe....The Dr was right............
 
Back
Top Bottom