Kwa Hili Mh Raisi Kuwa Makini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Hili Mh Raisi Kuwa Makini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masanilo, Jan 2, 2011.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nimefatilia kwa makini hotuba ya Mh Kikwete kwenye salaam za mwaka mpya, dhahiri suala la katiba mpya si suala la serikali wala chama anachokiongoza. Nimemuona akitamka bila kuwa na hisia toka moyoni mwake. Nasita kabisa kumpongeza kwa sababu binafsi nina mfahamu Jakaya Kikwete ni mtu wa midhaha hata kwenye mambo ya msingi. Ni tume ngapi Mh Kikwete ameunda tokea ameingia Madarakani? Kipi kimeishafanyiwa kazi? Wale jamaa wa madawa ya kulevya, Majambazi wanaendelea kupeta tu. Suala la EPA amepiga changa la macho kwa kuzungumza watanzania wanachohitaji kukisikia. Kamati ama tume atakayounda sitegemei ije na agenda mpya. Ningependa suala hili lifanyiwe kazi na Kamati ya Bunge.

  Tunahitaji katiba mpya kupunguza madaraka ya uraisi, Bunge litumike kuthibitisha teuzi za raisi, Tuwe na wagombea huru, Muungano wetu na Zanzibar upitiwe upya, mfumo wa sasa serikali ya Muungano inabeba mno Zanzibar, tunataka Tanganyika yetu, Raisi lazima aweze kuwajibishwa pale anapovunja katiba. Tume huru ya Uchaguzi iundwe kwa maridhiano ya vyama vote vya upinzani.

  Ningependa pia kufuta vyeo visivyo na tija kama kuna DED mkuu wa wilaya anakazi gani? Kama kuna RC sasa Kazi ya RAS ni nini? Muundo wa serikali upitiwe upya kupunguza matumizi na kuongeza tija.

  Kuwe na sheria ya kubana Kiongozi anayeletea hasara taifa basi mali zake zitaifishwe
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Well said Mchungaji. Hili sio swala la yey kuunda tume. Tumekuwa na tume ngapi za Rais kuhusu katiba mpya ambazo zote zimekuja na mapendekezo ya kufanya tu "repair" ya vipengele kadhaa kwenye katiba?

  Hapa watapewa jukumu, with tunes and rhythms, za Mkuu wa Kaya na kwa kuwa atatumia advantage ya kuteua watu wenye heshima yao kwenye jamii ambao tunawaita wataalam, mwisho wa siku watatuletea report ya kusema katiba haina haja ya mabadiliko zaidi ya "repair" nyingine na tutapotezewa kwa kuambiwa "WATAALAM WAMESEMA".

  Hizi tume za Raisi ni upuuzi mtupu na ulaji wa fedha za umma huku zikitekeleza pre-determined resolutions za Mkuu.

  Better jambo hili liachwe mikononi mwa bunge na iundwe Tume huru kabisa yenye makundi anuai ya jamii ambayo yatatekeleza wajibu wao kwa mujibu wa mustakabali wa nchi yetu. Otherwise ni usanii mwingine wa Rais wetu


  O.T: Signature yako Mchungaji nimeikubali, nakutakia kila la kheri kwenye four-years term plan yako.
   
 3. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Masanilo umesema vizuri, ila subiri kutoa moni kwenye tume halafu tuone utendaji utakavyo kuwa, ikiwa tofauti hapo ndipo tutakapowasha moto ambao hautazimika
   
 4. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa upande mwingine ukiangalia kuunda tume nikujaribu kupoteza muda, ni sawa na mtuhumiwa anapoisumbua mahakama ili siku zisogee lakini hukumu iko palepale
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sisi wenye akili tunajua janja ya Kikwete! Tume itatoa Mapendekezo ya kijinga mwanzoni mwa 2015
   
 6. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Masanilo hilo halina ubishi ni wazi kuwa tamko lake ni kupunguza kasi la madai ya Katiba Mpya subiri utaona hiyo tume mpaka mwaka 2015 itakuwa Bado kwakuwa sisi Watanzania tulivyowasaulifu ndio tutasahau kabisa na 2015 inafika kesho tu huku Tume hiyo itakuwa haijafanya chochote cha msingi!
  Nina wasiwasi sana na hilo la katiba mpya kuwa tayari 2015.
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,670
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kumkubalia Kikwete azima yake ya kuanzisha mchakato wa kuunda katiba mpya,hili la yeye kuunda Tume tulikatae kwa sauti kubwa maana yeye na Tume yake watatupeleka mpaka 2015 bila majibu ya msingi kisha uchaguzi ufuatao tutaendelea kuufanya kwa katiba hii na NEC hii hii. Tume gani alishawahi kuunda ikaleta ripoti yenye tija? Tume ya Kikwete NO, tunataka tume ya Bunge!
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mchungaji,

  Umeanza lini biashara ya kumpigia mbuzi gitaa? Of all the people, huyu jamaa unaweza kumpa ushauri kweli au na wewe umeanza mwaka na illusions ukasau mtu unayemwongelea ni mtu wa namna gani?

  Hata hivyo naamini unakumbuka ule usemi maarufu sana kwenye mambo ya IT...garbage in.....hebu malizia basi mkuu!!


  DC
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Garbage out....

  Ila mkuu pamoja na udhaifu wake basi aambiwe mara nyingi nyingi ataelewa huenda labda ni slow learner.
   
 10. m

  mzambia JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Jamani hebu tukumbuke tume zilizopita kama ya nyalali, kisanga, bomani maoni na mapendekezo yamefanyiwa nini?
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Labda kwa kuwa wewe ni mchungaji basi inawezekana tuko kwenye levels tofauti.

  Labda tayari mwenzetu una upako wa kuwafanya mabubu wasikie na vipofu waone? Utakuwa na lipya zaidi ya yale aliyosema Mrisho Mpoto na wengine kibao au utatumia utaratibu wa kubabu babu wa kumlabua vibao?
   
 12. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Utashangaa sana kusikia mwananchi wa kawaida kutoka Tanganyika akisema Zanzibar inabebwa.Mshangao wangu unakuja kwani mie nikiwa kama mzanzibari sitaki hata huo muungano.

  Nadhani kilio chako cha kuwa Zanzibar inabebwa ni sawa kile kilio cha mtoto mchanga anaelia kuekwa chini......Na kwa bahati mbaya mzazi wa mtoto ni baba wa kambu anaepata ruzuku kwa kulea mtoto huyo.Hivyo hamshushi mtoto anaendelea kupiga kelele za kushushwa lakini wapi ni bure!

  Usijidanganye kuwa wazanzibari wanataka muungano.Kama kuna mzigo, basi ni wa hiari.Tanganyika ni nchi masikini, so is Zanzibar at the moment.Mkiona mzigo na complexity ni kubwa ya kuresolve muungano.Solution ni kuvunja, which is the best solution to this problem!
   
 13. tunalazimika

  tunalazimika JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  akitutia hasara naye tunamfanyia kichina china tu_mali zake hatugusi kabisa, atakutana nazo kwa sir !
   
 14. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Rais Kikwete hana cha kupoteza kwa hiyo acheni kuropoka hapa.
   
 15. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Siamini kama wateule wakikwete wataweza kuleta hoja zitakazo onyesha mabadiliko tunayoyatazamia, maana kumbuka yeye ndo atakuwa kawapa ulaji,
  La msingi ni Tume kuundwa na Bunge na tume hiyo iwajibike kwa bunge.
   
 16. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,080
  Likes Received: 4,663
  Trophy Points: 280
  2005 Kugombania Urais thru CCM, nilikuwa sijaelewa why Mkapa alikuwa anampinga JK na kum favour Sumaye, sasa nimejua
  at least Sumaye angekuwa rais, i said at least.
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Tulipo sasa si mahala pa kucharibu kuendeleza mizaha kama kweli tupo serious.Kila kitu kina turning point na siasa za leo katiba ni turning point yetu. Imagine, jinsi ambavyo wateule wa rais walio wengi wanavyotuongoza bila kujua wanayofanya na hakuna yoyote anayeweza kuhoji. Ndio maana Dowans, TRL, Air Tanzania na mashirika mengine mengi yako hoi. Mambo lazima yabadilike maana uzoefu unatuonyesha watawala kwa kuitumia katiba hii hawako na nia ya kuona mambo yanakuwa tofauti zaidi ya kupendeleana tu.
   
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280

  - Fair and balanced too!


  William.
   
 19. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona amekuja na long term plan. Wasiwasi wangu kwa nini awe mke kutoka Zenj wakati bara tuna watoto bomba!

  Vinginevyo ana mapendekezo ya busara juu ya katiba tuitakayo. Nafikiri wote tukija na mawazo mazuri katiba inaweza ikaanzia JF na kuwa rubber stamped na watawala
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Unatoa mawazo yako au unalalamika?

  Eti haonyeshi hisia hapa unaonyesha ulivyo hasi...hisia zinapimwa vipi tena? (indicators). umezoea kugomba ndio uonekane baba...

  Mheshimiwa ameunda tume na nyingi kama si zote zimefanyiwa kazi, hadi kufukuzwa PM, Kufunguliwa mashtaka vigogo, kufunguliwa Zombe etc...weka rekodi zote usiwe mchoyo mkuu

  Hakuna changa la macho, Rais wetu ni msikivu, mpole na mzalendo anafanya hata mambo ambayo hata asingefanya hana lawama...kumbuka katiba mpya si sera ya chama...ni personal decision mpe credit mkuu acha uchoyo

  Hayo mengine ni mapendekezo yako peleka kwenye tume itakayoundwa hivi karibuni ok

  Acha kulialia na kulalamika kama yule mzee wenu asiyona jema kwa JK mwambieni utakonda bure..JK ni mzalendo atakayeingia kwenye historia kama rais Msikivu, aliyekubali mabadiliko kwa faida ya nchi yake.
   
Loading...