Kwa hili mb. Lekule Laiza ameiweka uchi serikali yake inayoongozwa na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili mb. Lekule Laiza ameiweka uchi serikali yake inayoongozwa na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HGYTXK, Oct 5, 2012.

 1. HGYTXK

  HGYTXK Senior Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kupitia taarifa ya habari iliyorushwa na kituo cha ITV nimemsikia Mbunge huyo akitoa maneno yafuatayo ktk harakati zake za kuomba kura kwa wanaCCM ktk ngazi ya uenyekiti anayoigombea.Namnukuu.

  "Wananchi wa Longido mnatakiwa mtambue kuwa nafasi hii ninayoigombea haina maslahi kwangu kimaslahi ila ninachokihitaji ni kurudisha hadhi ya chama ambacho ni mimi ndiye niliyekifikisha hapa kilipo,Mnakumbuka kuwa hata hii wilaya ya Longido ni mimi ndiye niliyeipigania mpaka tumepata halmashauri hapa ata kama HAIKUWA NA VIGEZO VYA KUWA HIVYO".

  MY TAKE: Hii ndio serikali yetu,hautaji Degree kuamini kuwa mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo yanayofanyika hayazingatii vigezo bali ni utashi tu wa watawala ktk kuangalia ni jinsi gani watatoa fadhira zao kwa watu fulanifulani ktk chama chao.Kuna sehemu nyingi sana hapa nchini zina kila vigezo zinazostahili kuitwa wilaya,mkoa ama Manispaa lakini hazifanywi hivyo kutokana na kutokuwa na makada ama viongozi maarufu wanaotokea sehemu hizo.Tumekusikia Leiza na asante kwa kuonyesha madudu ya serikali yetu.

  MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TZ.
   
 2. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kwa ccm sishangai
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hili mbona liko wazi ndugu yangu, huoni nasi huku Katavi ndio tunakumbukwa kwa kuwekea barabara ya lami na zaidi tumepata mkoa mpya hii yote ni kwa sababu ya Pinda. Bila yeye haya maendeleo tunayoyashuhudia huku hivi sasa tungekuwa tunayasikia tu.
   
 4. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwa maana hiyo basi, yale majimbo yanayoongozwa na wapinzani wasahau maendeleo hata kama wamefikisha vigezo stahiki.
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Lakini upeo wake wa kuelewa unaweza kuwa chanzo cha kutojua kama Londigo ilikuwa na vigezo vya kuchaguliwa kuwa Wilaya. Nadhani tatizo hapa si Serikali kuifanya Longido kuwa Wilaya bali ni mawazo duni tu ya mwanasiasa huyo kuwa yeye ni chanzo cha wilaya hiyo kupata hiyo hadhi. Suala la eneo fulani kupewa hadhi ya wilaya si la wanasiasa pekee, linapitia mchakato mkubwa, hushirikisha wataalamu wa ardhi, wanasiasa, wachumi na wengine wengi.
   
 6. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sasa kama yeye alifikisha hiyo wilaya hapo,kwan hakuna wakuipeleka zaid ya hapo?
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu ungetaja majimbo ambayo yanaongozwa na wapinzani na siyo wilaya la sivyo mchango wako huu unaweza kukushushia hadhi ya kuwa GT. Hili linaweza kusaidia pia kutazama hali za majimbo hayo kimaendelea ukilinganisha na yale ambayo ni Wilaya.
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Teh teh, Vijana wamewakamata hao wazee, hadi sasa wanaongea vitu ambavyo vinawashushia hadhi. Mimi ninachoamini ni kwamba hoja za kuomba kupata wilaya si za siri na huwa zinawasillishwa kwenye vikao mbalimbali na hata katika vikao vya Bunge, hivyo sijiaminishi kabisa kuwa kuna Wilaya inapitishwa kisiasa hata kama hazina vigezo. Namshangaa sana huyu mzee kama alikuwa anajua kabisa kuwa anaongoza jimbo ambalo halina vigezo vya kuwa wilaya na akakaa kimya. Ni dhahiri kabisa kuwa kwa kauli hiyo yeye ndiye hana vigezo vya kuwa kiongozi wa juu wa CCM.
   
 9. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,322
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Mkuu, inaonekana wewe umesoma vitabu vinavyo onesha taratibu za kupata manispa, halmashauri, mkoa, wilaya n.k, hizo ni theories, practically huwa haiko hivyo kwa magamba, mwana siasa alioko sehemu fulani inategemea anamvuto na ushawishi kiasi gani kwa wakuu wa magamba, rejea yafuatayo, hivi ule uwanja wa ndege wa kimataifa pale Arusha enzi za Sumaye, uliishia wapi? nakumbuka enzi hizo watu walipiga kelele, kwamba huo ni upotezaji wa pesa cause kama kuna KIA, ambao upo jirani sana na Arusha, kuna sababu gani ya kujenga huo mwingine tena, watawala wakakomaa, serikali ipobadirika, kimya, hii ndio Bongo bana!
   
 10. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  usishangae mkuu, ndiyo maana kuna pendekezo la kuiweka Tanzania chini ya CCM kwenye maajabu ya dunia. we fuatilia watakuelekeza namna ya kuipigia kura ili iingie kwenye maajabu ya Dunia.
   
 11. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Vipi sisi ambao hatuna viongozi wa juu serikalini?
   
 12. The Planner

  The Planner JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kama ningekuwa mmoja kati ya wana Longido ningecomment kuwa.,kama anaweza kupigania vitu visivyo na vigezo na kuiingiza nchi katika kugharamia wilaya mpya isiyo na vigezo haoni kwamba hiyo ni sababu tosha ya kumnyima madaraka ayatakayo!
   
 13. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Mh. Lekule Laizer amesema kweli kwani Longido ni kama kijiji vile! Mji hauna hadhi ya kuitwa Makao Makuu ya Wilaya.
   
 14. M

  Mawinyi Yeye Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu bwana yeye kaamua tu kuweka wazi lakini hivi ndivyo vitimbi vilivyo kithiri katika majimbo ya uchaguzi 2010 eg, ILEMELA namengine mengi tu!
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Sijui inakuwaje maana ndio mfumo tuliourithi tangu enzi za mwalimu.....tehe tehe eeh.
   
 16. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tayari ipo uchi tangu zamani
   
 17. Mwamba Usemao Kweli

  Mwamba Usemao Kweli JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 745
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  ndio viongozi wetu hawa kupitia chama magamba sampuli ya Dk. Bana na wengineo wengi wenye kufikiri kwa kutumia sehemu za kupumzikia chini mwilini mwanadamu anapochoka kusimama ama kutembea.
   
 18. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Katavi usicheke mkuu, sisi tunaumia wenzio!
   
 19. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,491
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  mkoa wenye wilaya mbili tena baada ya wilaya ya mpanda kukatwa....katavi ishaongezeka wilaya nyingine kweli...kwa tz hii ni kawida sana
   
 20. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,491
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  ndo sehem gani hiyo...mwamba usemao ukweli apa unaogopa kusema ukweli
   
Loading...