Umeandika mambo ya msingi kodi kubwa inaliwa na wAchache ndo maana kila mwaka ripoti ya C.A.G lazima ibaini madudu.Wakati Rwanda hadi muuza vocha kwenye foleni ya Magari barabarani anamashine ya EFD!
Kodi lazima ikusanywe. Hao tunaowaita machinga na hawalipi kodi kipato chake kwa mwaka ni kikubwa kuliko sekretari katika ofisi ya mkuu wa wilaya lakini huyu kila mwezi analipa kodi kwa lazima kupitia mshahara wake!
Watu walipe kodi. Kigali na Rwanda kwa ujumla mtu anaona ufahari kulipa kodi kwa sababu anaona faida ya kufanya hivyo!
Kwetu kidogo ni tofauti. Wengi wanaolipa wanaona wanalipa kodi kubwa, na hawaoni faida kubwa ya kufanya hivyo kwa sababu ama hawaoni tija ya kutosha kutokana na kodi zao, ama wanaumia kuona wengine ndio wafaidikaji wakubwa wa kodi zao, na wengine wenye vipato zaidi yao hawalipi kodi ipasavyo!