Kwa hili la UKUTA nipo upande wa Rais JPM,inaweza isiwe suluhisho lakini itapunguza upotevu wa madini ya Tanzanite

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg

Supt Burgess akikagua kikosi chake cha kwanza cha askari wa mgodi wa Mwadui mwaka 1951.

image.jpeg

Askari wa Mgodi wa Mwadui wakisimamia uchambuzi wa almasi "Sorting Area"

image.jpeg

Wafanyakazi wa Mgodi wa Mwadui wakikaguliwa kama wamebeba almasi mara baada ya kumaliza kazi katika mgodi.

image.jpeg

Lango la kuingia kwenye eneo linalochimbwa madini ya almasi,lango hili lililindwa masaa 24

image.jpeg

Askari wa Mgodi wa Mwadui akilinda eneo lenye uzio,lililojengwa kuzuia uwizi wa almasi

=============================================================================
Kuna mengi tunaweza tusikubaliane na JPM,lakini kuna mengine baadhi tunaweza kumuunga mkono na kumtia moyo.Hili tunafanya si kwa sababu yoyote ile,bali kwa sababu nia na kusudio lake inakuwa ni kulinyanyua Taifa kufikia kule ambapo wengine walisita kufika.

Tumesikia uamuzi wa Rais,tumesikia nia ya Amiri Jeshi Mkuu,kuagiza JWTZ kujenga UKUTA kuuzunguka eneo lenye mrundikano wa madini ya Tanzanite huko Mererani-Manyara.Uamuzi ambao mimi kama raia,mdau wa historia ya uchimbaji madini Tanzania na raia wa kawaida,ninaunga mkono kwa asilimia zote.

Suala hili limepokelewa kwa mtazamo tofauti,wapo watu wanaoliponda na kumkosoa Rais,wapo wanaoona kuwa UKUTA si suluhisho,na maswali yao ni kuwa ujengaji wa UKUTA hauna tija katika kufikia lengo la kuzuia uwizi wa madini ya Tanzanite.

Wengi wanajisahaulisha kuwa hata huko Geita,eneo la madini lipo ndani ya uzio,huko North Mara-Nyamongo,dhahabu ipo ndani ya uzio.Ni lazima Tanzanite nayo,ambayo kwa miaka mingi ilikuwa nje ya uzio,nayo iwekwe ndani ya uzio.

Mwaka 1940 wakati Dr Williamson alipofungua mgodi wa Mwadui,eneo lenye kuchimbwa almasi lilikuwa wazi na bila kizuizi,baada ya wenyeji kujua thamani ya almasi na faida ya almasi,biashara ya magendo ilishamiri.Ikawa 50% ya almasi inayochimbwa ndani ya mgodi wa Mwadui ikawa inauzwa kwa magendo.Ilisafirishwa kwa magendo na kwenda kuingizwa katika mfumo wa almasi ya Kimberley kule Afrika ya Kusini.

Ikawa katika soko la dunia kule London,almasi ya Mwadui ikaanza kuuzwa kama ni almasi kutoka eneo la Kimberley kule Afrika ya Kusini.Dr Williamson akawa katika juhudi za kukabiliana na magendo haya na ilimuumiza kichwa kujua namna atakavyojilinda na biashara ya utoroshaji wa almasi kutoka katika eneo la uchimbaji.

Jambo la kwanza alilofanya Dr Williamson,ni kujenga uzio wenye kilomita za mraba 24 ili kuzuia eneo la uchimbaji,akaanzisha jeshi la askari wasaidizi(Auxuliary Police) 200 na akaajili askari mwenye cheo cha Chief Superintendent kutoka katika jeshi la polisi la jiji la Birmingham Uingereza ili kuwafunza askari wa kiafrika namna ya kulinda mgodi wake.

Dr Williamson akaagiza "specie" ya mbwa wakali toka kwao Canada,akaunda kikosi cha farasi na kwa mara ya kwanza "Electronic Eyes" zikafungwa katika mgodi wa Mwadui ili kuzuia wizi wa almasi.

Kama hii haikutosha,Dr Williamson aliweka geti moja tu,la kuingia na kutoka ndani ya mgodi wa Mwadui.Wakazi wote wa Mwadui na wasaidizi wao walikuwa na "Pass" maalumu zilizowatambulisha kama ni wakazi wa mgodi,ndugu au rafiki wa mkazi yoyote wa mgodi hakuwa na ruhusa ya kuingia eneo la Mwadui bila kibali maalumu.

Kwenye geti la kuingia na kutokea "Protection Area" ambapo almasi inachimbwa walikaa askari waafrika waliokuwa watiifu na wenye kulipwa mishahara mizuri ili kuwaepusha na tamaa za rushwa na magendo.Gari zilipekuliwa kwa umakini,na wale wachambua almasi walisimamiwa kwa ustadi mkubwa sana,ili wasichepuke hata na kipande cha almasi.

Licha ya ulinzi wote huo,bado wakazi wa pembezoni mwa mgodi wa Mwadui toka vijiji vya Utemini,Maganzo na Mwigumbi walivumbua mbinu mpya ya kuiba.Kama "Nyoka" wa Marerani,hawa wa Mwadui waliitwa "Wabeshi".Rais wetu anasema wataweka kamera,hata ukificha Tanzanite kwenye kiatu itaonekana,lakini kule Mwadui,licha ya kuwepo kwa "electronic eyes",mbwa,farasi na askari pamoja na wafanyakazi kuvuliwa nguo wakati wa kutoka eneo la mgodi,lakini bado magendo yalifanyika.UKUTA inaweza isiwe suluhisho,lakini unaweza kupunguza tatizo.

Licha ya uzio,hawa wabeshi huiingia mgodini kwa njia za panya,huua askari na mbwa na kuiba almasi,matajili wa almasi za magendo hupatikana katika mji mdogo wa Kahama,miaka hiyo,Waarabu wengi wa Maganzo walifadhili wabeshi walioenda kuiba almasi kwa kuvuka uzio wa mgodi.

Wabeshi wengi waliuwawa na mbwa wa mgodi pamoja na askari kwa silaha za moto,licha ya ujenzi wa "fence" na ulinzi wa doria ya mbwa na farasi,bado almasi iliibiwa,lakini si kwa kiwango kama kile cha kabla ya kuwa na uzio.

Kupunguza wizi zaidi na zaidi,Ikaamuliwa watu wote wanaotoka eneo la uchimbaji wa almasi,wavuliwe nguo na kukaguliwa wakiwa uchi wa mnyama,hii ni kwa sababu,licha ya uzio na ulinzi,bado kuna wafanyakazi walioficha almasi katikati ya upenyo na matundu ya miili yao.

Chief Security wa Mgodi wa Mwadui,polisi mstaafu,raia wa Uingereza,Mr Supt Burgess alihakikisha kunakuwa na uwiano wa askari mmoja na mfanyakazi mmoja.Wakati wa "sorting" ya almasi,wafanyakazi waliokuwa "sorting Area" walikuwa na askari mmoja mgongoni.Askari hawa walilipwa vizuri,walikuwa na nyumba nzuri na huduma nyingine za kijamii zilizo bora ili kuwaepusha na vishawishi.

Uzio wa UKUTA wa Tanzanite huko Mererani ambao ni mpango wa Rais JPM,uendane na uboreshaji wa maslahi ya walinzi wa eneo husika.Kujenga UKUTA bila kuwa na walinzi walioboreshewa maisha na mishahara yao,inaweza kuwa ni kazi bure.

Huwezi kumkabidhi mbwa duka la nyama lisilo na kufuri alilinde huku akiwa na njaa ya kutwa nzima.Mwisho wa siku ni kumuonea mbwa na kumuona ni mwizi na asiye na msaada.UKUTA wa Mererani bila walinzi walio na maslahi bora ni kazi bure.Hili aliliona Dr Williamson,na kushinikiza kuanzisha kikosi cha askari wake wa kisasa,waliolipwa,kutunzwa na kufunzwa kwa gharama za mgodi wa Williamson.

Hatimaye mwaka 1951,Dr Williamson akashawishi Bunge la Tanganyika(LEGCO) kutambua askari wa Mwadui wanaolinda mgodi chini ya sheria ya "Tanganyika Auxiliary Police Force",japo askari hao wakabaki kuwa chini ya mgodi wa Williamson.

Kikosi cha Askari wa Mwadui kikawa mfano wa askari wote wa Tanganyika,hata baada ya uhuru,askari wengi wa Mwadui waliasisi vikosi vya farasi,brass-band na mbwa katika chuo cha polisi Moshi.

Hii ni rai kwa Rais Magufuli,haitoshi tu kujenga ukuta kuzunguka Mererani,bali wawepo walinzi wenye uweledi na maslahi mazuri kulinda eneo la mgodi.Huko Mwadui,enzi za Williamson,licha ya kuwepo kwa uzio na ulinzi mkali,bado "wabeshi" wa kijiji cha Maganzo na kule Mwigumbi,walijipenyeza ndani ya mgodi na kuiba almasi za magendo.

Kwa "njaa" ya Polisi wa kamanda Sirro,hata UKUTA ukijengwa,si ajabu kuwakuta wakiwasaidia "nyoka" wa Mererani kupenyeza na madini nje ya eneo la uzio ili na wao wapate mgao kusukuma maisha yao.Uzalendo katikati ya njaa na dhiki,ni kama biskuti kukataa kuyeyuka ndani ya maji au bilauri ya sharubati.

[HASHTAG]#Mererani[/HASHTAG] [HASHTAG]#UKUTA[/HASHTAG] [HASHTAG]#KwabajetiIpi[/HASHTAG]?
 
Labda ataifishe maeneo ya wachimbaji wadogo,maana uwiano wa mchimbaji mdogo na askari pamoja na wana Apollo itakuwa kazi ngumu sana

Nadhani ukuta ukiisha sitashangaa nikisikia leseni za wachimbaji wadogo zikifutwa na eneo kuwa chini ya serikali au akapewa muwekezaji,na huo ndio itakuwa mwisho wa uchumi wa watu wa maeneo hayo

Ninavyoiona serikali hii inatamani sana kuhodhi maeneo ya madini,na sehemu rahisi ni eneo la wachimbaji wadogo mererani,sasa hivi wanadanganywa kwa muda kwamba wanawekewa ukuta wa bure

Nawashauri wana mererani wakae mkao wa kusikia tamko lolote wakati wowote
 
Upo sahihi...Mimi pia ningewaomba wale wapiga kura wa Ole Millya,wajiandae kisaikolojia
 
View attachment 596776
Supt Burgess akikagua kikosi chake cha kwanza cha askari wa mgodi wa Mwadui mwaka 1951.

View attachment 596777
Askari wa Mgodi wa Mwadui wakisimamia uchambuzi wa almasi "Sorting Area"

View attachment 596778
Wafanyakazi wa Mgodi wa Mwadui wakikaguliwa kama wamebeba almasi mara baada ya kumaliza kazi katika mgodi.

View attachment 596769
Lango la kuingia kwenye eneo linalochimbwa madini ya almasi,lango hili lililindwa masaa 24

View attachment 596765

Bendera hufuata upepo!
 
Upo sahihi...Mimi pia ningewaomba wale wapiga kura wa Ole Millya,wajiandae kisaikolojia
Kwa kweli,wabunge wa Manyara na Arusha waombe commitment ya serikali bungeni na waonyeshe wasiwasi, kwanza kujaziwa tu wanajeshi pale ni kama wanaandaliwa kisaikolojia,

Bahati mbaya serikali inataka kuwa tajiri wananchi wawe masikini
 
Mambo ya udhalilishaji huo kuvua nguo mmmh ahaaa bora siku hizi kuna haki za Mbwa mpaka binadamu, It was too much, Wazee walidhalilishwa sana kwenye mtiririko wako hicho kipengele cha kuvua nguo ni upuuzi mkuu wa hao wakoloni weupe waliwafanya watu wajinga
 
Hilo la kujenga sio wazo baya lakini ni kujaribu kuokoa chochote. Lakini nimeshauri ili tija ya hayo madini inatakiwa baada ya ukuta pachimbwe kwa mtindo wa open cast na sio hiyo ya watu kuchimba kama fuko. Ajira zitolewe kwa haohao wachimbaji wa sasa, watakaokosa ajira waandikwe majina yao, kijengwe kiwanda cha kuzalisha chochote kutokana mapato ya huo mgodi kisha ajira wapewe wale waliopoteza ajira zao kutokana na mabadiliko hayo.

Nje ya mada, pia napendekeza speed hiyo iliyoonyeshwa na jeshi kujenga ukuta, napendekeza jeshi lipewe matractors, combine harvesters, mbegu za kisasa wakalime, na chakula kitakachopatikana ndio kiwekwe kwenye maghala ya serekali ili kupambana na njaa na bei kupanda. Kisha sisi tunaolima kwa nguvu zetu tuachwe tuuze tunapotaka kwa faida.
 
Aya yako ya mwisho nimeielewa sana!!Umejadili vema
 
Nimependa hapo mwishoni ulipoweka [HASHTAG]#ukutakwabajetiipi[/HASHTAG]?
 
Labda ataifishe maeneo ya wachimbaji wadogo,maana uwiano wa mchimbaji mdogo na askari pamoja na wana Apollo itakuwa kazi ngumu sana

Nadhani ukuta ukiisha sitashangaa nikisikia leseni za wachimbaji wadogo zikifutwa na eneo kuwa chini ya serikali au akapewa muwekezaji,na huo ndio itakuwa mwisho wa uchumi wa watu wa maeneo hayo

Ninavyoiona serikali hii inatamani sana kuhodhi maeneo ya madini,na sehemu rahisi ni eneo la wachimbaji wadogo mererani,sasa hivi wanadanganywa kwa muda kwamba wanawekewa ukuta wa bure

Nawashauri wana mererani wakae mkao wa kusikia tamko lolote wakati wowote

Kweli, ,,pakipigwa ukuta wachimbaji wadogo wakae mkao wa safari
 
Duuuh!!Yaani jamaa wanakaguliwa uchi wa mnyama!!Kumbe wanaapolo walianza zamanj sana kabla ya mkoloni.Sasa hawa waliiba madini wakauza wapi?
 
Hayo mambo ya ukuta, matuta kwangu mimi nayaona kama vile ni physical measure, siyo mambo ya kutumia akili, kuna vitu unaweza kuzuia kwa physical measure lakini siyo madini ambayo mtu anaweka mfukoni anaondoka nayo
 
Hii ni katika kulinda rasilimali za nchi.
Kuna uvumi kuwa majiran huwa wanajitapa eti ule Mlima upo kwao, sasa naomba mh auzungushie ukuta tuone watafanaya nn.
Ni maoni tu ndugu zangu.
 
Utatuzi wa matatizo ya Tanzania umo mikononi mwa watanzania wenyewe. Rais ameonesha jinsi ya kuthubutu kukabili matatizo yetu wenyewe kwa mazingira yetu na uwezo wetu. Nimependa ile wanunuzi waje Mirerani na wanunue hapo hapo na Tanzanite isafishwe hapo hapo.
 
Back
Top Bottom