G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,591
- 36,004
Ni wazi kuwa CCM inataka CHADEMA kupeleka wagombea wengi bungeni ili kushindanishwa kwenye ubunge wa EALA kisha CCM wautawale mziki.
Kwa maana nyingine ni kuwa CCM wanataka kuichagulia CHADEMA wawakilishi na iwe rahisi zaidi kuwanunua kwenye kampeni. CHADEMA kwa hili wamewaweka CCM mfukoni.
CHADEMA inatakiwa kukaza hivyohivyo ili kuzuia vitendo vyovyote vile vya hujuma na kuzalisha upya umamluki ndani ya chama.
Hakuna mahali popote pale kanuni zinazoelekeza kuwa wapitishwe wagombea wanaozidi ili wakashindanishwe na pia kwa mujibu wa nafasi za CUF na CHADEMA kanuni ya uwiano wa moja ya tatu inavunjwa rasmi kwani haitekelezeki.
Tumeona yaliyotokea CUF kwa CCM kuamua nani awe muwakilishi wa CUF EALA kwa maslahi ya CCM! Kamwe CHADEMA tusiruhusu mchezo huo. Walipolala wao sisi tulishaamka siku nyingi! Mpasuko ndani ya CUF kwa sasa utufunze jinsi umamluki wa "fisi" CCM unavyoangaza na kupepesa huku na kule.
Kupeleka wagombea wengi ni mwanzo wa kukipasua chama kwa kuwa itawalazimu kuomba uungwaji mkono ndani ya CCM na hapo ndipo mwanzo wa kuanza upya kulea mamluki ndani ya chama.
Pia sasa bunge liangalie upya kanuni hii ya eti mgombea wa CHADEMA kupigiwa kura na mtu wa CCM au vyama vingine. Ni kanuni isiyo na maana na iliyokosa weledi kitaaluma. Ni kanuni chafu na inayozaa umamluki ndani ya vyama.