Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,698
- 4,693
Wazungu kuendelea kuzuia miradi yetu kwa sababu za ‘nature’ naona bado wamaamini Afrika ibaki kuwa bara la giza ili watoto wao wakijifunza maisha ya watu wa zamani, waje wayaone Afrika. Haikubaliki. Nasubili niungwe mkono na Wamarekani kama wa-TZ wanavyounga mkono Wamarekani kuzuia ujenzi wa hydro power ya Stigler. Ni aibu kwamba kuna wa-TZ wanaodhani US inafahamu sana matatizo yetu au inatutakia mema sana kuliko rais wetu. Walipokuja na Lighting Africa, walikuja na miradi yao ya mitambo ya gesi. Matumaini ilikuwa ni kuvuna toka TZ. Kuna dalili wanaziona kwamba sasa mitambo yao haitahitajika sana tukiwa na hydro kuliko hiyo mitambo ya gesi ambayo ni ya kwao.
Kwa Wa-TZ wenzangu naomba tujadili. Sisi hatuna nafasi ya kushauri yanayotokea US. Iwe ni ukuta wa Texas/Mexico au mitambo yao ya nuklia. Hebu tuelewesheni kuna madhara gani ya ujenzi wa hydro ambayo ni makubwa kiasi cha kupigiwa kelele dunia nzima? Au ni hizo ripoti za WWF ambazo nyingi zimeandikwa na wa-TZ wenzetu, wengine tukiwafahamu ni dhaifu kitaaluma na wengine ikiwa ni sehemu ya upigaji? Lakini pia turudi kwenye maoni ya Rais. Je, machimbo ya Uranium na hiyo hydro, nini kina madhara kuliko kingine? Mbona hawajasema stop uranium mining?
Naomba tujadili, kitaalamu. Tuondoe hisia za kisiasa.