Kwa hili la musoma mjini ufisadi unanukia kwenye sensa.

Aug 18, 2012
17
2
Ni siku ya ijumaa ambapo makarani wa sensa halmashauri ya manispaa ya Musoma walipokutana kupokea posho ya kazi ya sensa. Makaran kwa uvumilivu wao wamepewa pesa mida ya Saa kumi na moja wakikuta pesa imeongezeka tofauti na mkataba unavyoonyesha. Pesa hiyo ni shilingi 7000 kwa kila karani.

Makarani hao walipo jaribu kuhoji imetoka wapi hiyo pesa mara wanaambiwa ni pesa ya usafiri kipindi cha SEMINA wakiendelea kuhoji kama ni nauli ilikua wap kipindi cha semina na kwa nini watu wa DODOSO REFU na FUPI walipwe sawa huku siku za semina DODOSO REFU zilikua kumi na moja na DODOSO REFU siku saba, wakihoji kama ni pesa ya naul kwa hesabu zipi wamepata elfu sama.

Mara zikazuka tetesi kwamba ni Agizo kwa halmashauri ziwalipe makarani pesa hizo kwa ajili ya kujaza DODOSO LA JAMII. Kwa kua hii pesa haipo kwenye mikataba kuna walakini wa UCHAKACHUAJI na kama si hivyo basi muandaaji wa mkataba wa Taasisi ya takwimu hakua makini na kukosa umakini huo kama si kulindana afukuzwe kazi kwa kuchochea fujo nchini na kuwa kikwazo cha zoezi la sensa 2012.

Makarani wa sensa jana walisubiri pesa kuanzia saa tatu akhsubuhi na kuanza kulipwa saa 12 jioni bado kuna vifa vya kazi havijatolewa kwa taarifa kutoka kwa mratibu wa sensa manispaa ya musoma anasema jana ilikua ndege ija na hivyo vifaa kama uniform, vitambulisho, na mabegi maalumu ya kubebea madodoso. Naomba kuwasilisha.
 
Hakuna uniform bongo nzima. Bora nyie mmelipwa hata 7000 kujaza dodoso la jamii hapa kibaha ni sifuri ila baadhi ya vifaa hatujapewa. Hii sensa ni ya haijawai tokea tz.
 
Yaani ni aibu, huku manyara hata posho ya kuwapa viongoz huko vijijin hakunaga sasa nashndwa kuelewa kesho 2taanza vp kaz
 
Elfu 7000 haijulikani ni ya nn maana wanasema ya nauli kipindi cha semina mara wanasema ya dodoso la jamii haieleweki
 
Hakuna uniform bongo nzima. Bora nyie mmelipwa hata 7000 kujaza dodoso la jamii hapa kibaha ni sifuri ila baadhi ya vifaa hatujapewa. Hii sensa ni ya haijawai tokea tz.

suala la uniform na vitambulisho yanatangazwa kwenye vyombo vya habari hata juzi watu wa NBS walihojiwa karani atatambulikaje wakasema kuna uniform zipo. Kwa mtizamo sensa hii na mwendo huu haitafana.
 
Kwani Mawakala/karani wa sensa wanalipwa Shs ngapi kwa siku ili kazi hiyo ikamilike?Maake nasikia mara 7000 per day, wengine wanasema 35,000 per day.

Mwenye data anipe maake kuna mtu wangu namdai long time sasa kalamba hiyo kitu (ukarani).Kwa mwendo wa 35,000 nadhani ni siku 3 tu atarudisha hiyo fedha kwenye mzunguko na wengine wakope pia ili kukuza uchumi.
 
njiii hii kila mtu siku hzi akipata upenyo na yeye anataka kufisadi,

sijui viongozi malaika tutawatoa wapi kwenye jamii hii iliyopotea!
 
Kwani Mawakala/karani wa sensa wanalipwa Shs ngapi kwa siku ili kazi hiyo ikamilike?Maake nasikia mara 7000 per day, wengine wanasema 35,000 per day.

Mwenye data anipe maake kuna mtu wangu namdai long time sasa kalamba hiyo kitu (ukarani).Kwa mwendo wa 35,000 nadhani ni siku 3 tu atarudisha hiyo fedha kwenye mzunguko na wengine wakope pia ili kukuza uchumi.
DODOSO REFU kwa siku 11 za semina kila siku 35000, DODOSO FUPI kwa siku 7 za semina kwa siku 35000. Na zoezi la sensa 250000 na pesa ya nauli 35000 kwa siku saba ila usimdai kwa fujo nenda polepole
 
Back
Top Bottom