Kwa hili la Mtwara na Lindi, Je Chadema ni chama cha Kaskazini na Ukristo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili la Mtwara na Lindi, Je Chadema ni chama cha Kaskazini na Ukristo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mshikachuma, Jun 5, 2012.

 1. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wote tunashuhudia mambo yote yanayofanywa na Chadema huko kusini(Lindi na Mtwara) kupitia local Television, magazeti na kwenye mitandao ya kijamii.

  Ukweli ni kwamba Chadema imepokelewa na kukubarika vizuri sana huko kusini. Swali langu ni -:

  Kuna baadhi ya watu huwa wanasema Chadema ni chama cha kaskazini na ukristo, Je Mtwara na Lindi ni kaskazini? Je Mtwara na Lindi kuna wakristo wengi kushinda Mbeya na kaskazini?

  .....Nakaribisha mgongano wa kimawazo.
   
 2. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kwani magamba yakiishiwa cha kusema ulitaka yasemeje?
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu tumesha wamaliza hata huku Jamvini hawaongei tena!!! Chikawe anagawa sanda misikitini halafu mashehe wanaingia mitini kwani anawaletea mikosi
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Haya maneno ya ukaskazini, ukristo na upuuzi kama huo tumeshauchoka jamani. Wamagamba wayalete na mnaojiita cdm pia!? Aaagrh!
   
 5. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Daah! ene wei nimekuta umeandika kitofauti! ungekula tusi hilo
   
 6. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu,umeshasahau kuwa vijana wa Nape hii ndiyo kaulimbiu yao hapa jamvini? Sasa tunataka kusikia wanasemaje
  baada ya CDM kutikisa huko kusini.
   
 7. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  We ulifikiri nimeandika nini?
   
 8. Y

  Yabisi Member

  #8
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtwara na lindi ni kaskazini mwa msumbiji
   
 9. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kauli itabadilika na kuwa cdm inapeleka ukristo na ukaskazini huko kusini.
   
 10. B

  BULOLE BUKOMBE JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu wapelekee ujumbe wangu hapa chini watu wote wanaosema kaskazini, kusini Mashariki na Magharibi wanajitahidi kutufundisha jiografia ya darasa la nne

  HABARI KAMILI Wana cdm tukikaa kimya mtatuona wajinga kama mlivyo ninyi nyote mnaotaka kuiaminisha jamii upumbavu wenu Kama huna cha kusema ni bora kukaa kimya halafu wajinga wote mnaotaka kutuambia cdm ni ya kaskazini acheni upumbavu huo ni wajinga kama nyie ndiyo wanaweza kuamini ujinga huo hivi cdm mlitaka kianzie kwa baba zenu au vyumbani mwenu au wapi ndipo kiwe halali kwenu? Hizo dini zetu pia zilianzia ulaya na uarabuni mbona hakuna anayesema ni dini za weupe na badala yake waafrica ndiyo wengi zaidi kwenye hizo dini kuliko hata waliozileta?

  Kifupi naomba muelewe wajinga wote mliotumwa kuhadaa watu, kuwa kila kitu lazima kiwe na mwanzo bila kujali mwanzo huo ni kusini kaskazini mashariki au magharibi kama zilivyo dini zenu zilianzia ulaya na uarabuni ndipo zikafika africa na cdm ni hivyo kaeni kimya watu wapo kazini na siyo kijiweni kuandika majungu mmeshachelewa ndege iko angani.
   
 11. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Ukiwa Msumbiji, Mtwara na Lindi ipo kaskazini!
   
 12. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unamaanisha nini?
   
 13. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  chadema kwa sasa ni chama pekee cha kitanzania na watanzania,ili kuthibitisha hilo naomba m4c ivuke maji iende z'bar!watu hawataamini kinchotendeka!
   
 14. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Daima watu huzungumzia pande nne za dunia bila kujali wao wako wapi!Ukisema CHADEMA ni ya kaskazini mpaka wa kaskazini unaanza na kuishia wapi?
   
 15. The Magnificent

  The Magnificent JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 2,669
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160

  Mkuu,
  Japokuwa umetumia lugha kali kidogo,nakupongeza....
  Hata mimi nawashangaa sana anaoihusisha CDM na kaskazini au uchaga,,,,by the way hapa kingeanzia labda pwani...wangesema chama cha watu wa pwani au chama cha wazaramo....kingeanzia musoma....kingeitwa chama cha wakurya/wajaluo/wajita.....
  Sasa napata taabu kidogo...labda wangetuambia mahali sahihi ambapo kilipaswa kuanzia ili kisiwe cha kikanda au kikabila(ambapo hakuna kanda au kabila) vinginevyo nitaendelea kuwaona hao waeneza propaganda kama wahuni,wapuuzi tu....


  The Magnificient
   
 16. W

  Welu JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  HIVI huko kasikazini hakuna CCM? Kilango niwawapi,? Mkono wawapi? Tyson mzee wa kusinzia a.k.a Wasira wawpi? Kinana n.k ni wawapi?....1.......2.......3........nk ni wawapi? Mrema wa TLP ni wa kaskazini je tlp ni ya kaskazini? Mbatia ni wa Dar je NCCR ni ya DSM?
   
 17. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,122
  Likes Received: 1,209
  Trophy Points: 280

  Mgomba wa ndizi ukitokwa na magamba, nini kinafuatia? CCM itakufa tu kwani nimepata habari toka kwa yule fundi seremala wa taifa anayechongesha lile jeneza lao kunako 2015; kaniambia kuwa analimazia na kuniomba niwahakikishie watanzania wenzangu kuwa sasa analipiga randa ili wazikwe vizuri kunako 2015. Sitashangaa kusikia Makamba na unafiki wake anaomba kujiunga na Chadema kunako 2015, japo ni kikongwe lakini ataomba tu kujiunga huku akitumia kigezo cha Ngombare Mwiru (mze asiye na faida serikalini/taifa) ili naye apate kula na kuendeleza unafiki wake. Chadema mkataeni huyu Maganda (Makamba) na vikongwe vingine vitakavyokuja omba ulaji, najua hata Kikwete ataomba tu kujiunga. Mapinduzi lazima yaje tu kwa kishindo, 2015 oyeeeeee!
   
 18. S

  SINTO FAHAMU Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama mnasuburi ubwabwa wa hitima mtasubiri sana, na huyo mchonga majeneza mwambieni achonge mengi maana msafara utakuwa mrefu kwenda Moshi na Arusha kupeleka maiti.
   
 19. rugumisa

  rugumisa Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na kitu chochote lazima kianzia mahali fulani ili kisambae duniani.mfano mzuri ni ukristo vuguvugu lote lilianzishwa na WAGALILAYA.Na mgalilaya ndio alikuwa na majukumu ya kuipeleka dunia nzima kwa zaidi ya watu bilion mbili na nusu kwasasa.mbegu moja inabidi ife ili izae makumi,mamia na maelfu!
   
 20. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,775
  Likes Received: 6,108
  Trophy Points: 280
  Ndugu zanguni; ogopeni sana kiumbe kinachokaribia kukata roho kuingia mautini na hasa kama matendo yake wakati wa uhai wake yalikuwa ya mashaka. Kiumbe cha aina hiyo kiko tayari kufanya lolote ili kujinusuru lakini ndio hivyo tena siku "yenyewe" ikiwadia imewadia.

  Na ndipo ilipofikia CCM; matendo yake kwa taifa letu yamekuwa machafu ajabu; siku zake ilizoandikiwa kuishi ndio hivyo tena zimekwisha mtasikia na kuona kila kimbwanga. CCM walipofikia sasa hivi wako tayari kuropoka kila aina ya upuuzi ili kujinusuru. Suala la ukweli na amani ya nchi kwao sio issue tena; la muhimu watajiokoaje na kifo kinachowakabili!

  Narudia tena: AMANI YA TAIFA HILI ITAVURUGWA NA CCM wala sio na kabila, dini, au kanda fulani; kama ikitokea basi vitakuwa ni vichocheo tu vya CCM bali ibilisi halisi ni lichama lenyewe!
   
Loading...