Kwa hili la mgomo wa madaktari, JK hatutokusamehe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili la mgomo wa madaktari, JK hatutokusamehe!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Masakata, Feb 7, 2012.

 1. Masakata

  Masakata JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Nikiwa kama mtanzania wa kawaida,maana uwezo wa kwenda na kupelekwa India kwa matibabu sina,nimesikitishwa sana na Mh.Rais J.Kikweti alivyoshindwa kabisa kuutatua mgogoro huu wa madaktari,imenisikitisha na imenishangaza sana kwa mkuu wa nchi kushindwa kutatua mgogoro mdogo kama huu,mpaka hivi leo umeleta MAAFA MAKUBWA kwa jamii yote ya kitanzania,licha ya mamlaka makubwa ya kikatiba,na kwa hakikia wewe binafsi na chama chako tawala HATUTOWASEMEHE DAIMA kwani maafa uliyoyasababisha ni Makubwa Sana,..nawashauri watz wenzangu kwa unyonge wetu,tuipigie CCM kura ya chuki hapo mwaka 2014 na 2015,ili tuwatoe madaraka,.
   
 2. M

  MBU2G Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ndugu,Damu za watanzania waliopoteza uhai kwa kukosa huduma zitawalilia na upanga utakua juu yao.
   
 3. m

  moshingi JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo lililomo humu JF ni kila jambo linaangaliwa katika sura ya kisiasa, Mgomo wa ma-dr
  tusijaribu kuufanya kuwa ni siasa...kila jambo humu linajaribu kuhusishwa na siasa...nadhani
  huu ni UBATILI mtupu sawa na kujilisha upepo...Katika hali ilivyo serikalini kwa sasa(ukata mkubwa wa fedha)
  hata Mh. Slaa angepewa nchi asingeweza kuutatua mgogoro wa ma-dr kirahisi, halafu ukaepusha migomo
  mingine ya waalimu, mahakimu, mapolisi, zimamoto, magereza, na wengineo...kuendesha nchi siyo lelemama!!
  Ningetarajia kwa kuwa sote tupo kwenye jahazi moja tumshauri humu rais wetu kuhusu hatua muhimu za haraka
  na zenye busara ili azichukue kuokoa maisha ya wanadamu wenzetu yanayoteketea katika mgomo huu
  Halikadhalika tumshauri namna ambavyo mgomo kama huu hautaweza kutokea tena, na kuepusha watumishi
  wengine wasigome...Maana hakuna kazi iliyobora zaidi kuliko nyinginezo...kila kazi inao umuhimu wake
  katika maendeleo ya taifa...
   
 4. i

  iphoneman Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naomba tutazame kitu kimoja ktk utoaji wa hoja zetu, ktk thread nyng hasa znazohusu mgomo wa madaktar tunaanza kumlaumu rais, hv ikitokea waalimu, madereva, polisi, n.k. wamegoma kw wkt mmoja bdo lawama ztakua kwa rais? Wizara znafanya kaz gan au nini maana ya kuwa na wizara husika? Tunatakiwa tuanze kuhoji wizara na utendaj kaz wake ktk kutatua matatzo ikishndkana kbsa ndo rais ainglie kati, ila tusikimbilie kumlaumu rais tu 7bu yy hawez kuzunguka ktk kila idara na kutenda kaz othrwise there z no meaning of DELEGATION OF AUTHORITY/POWER.... c kwamb namtetea rais wala madaktar kwa mgomo ila tunatakiwa tufikiri kiumakini kbla ya kulaumu mtu moja kwa moja!
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sijui kama ushauri wako una mantiki kwa kila mtanzania, unapoandika kitu humu kumbuka kuwa tunatofautiana katika ushabiki wa kisiasa. Wengine ni CCM, CUF, NCCR Mageuzi na vyama vingine....ninavyoona mimi ushauri wako unamuelekeo wa kiitikadi zaidi na umeshindwa kukumbuka kuwa CCM unayodhamiria kuitoa ni nambari wani!
   
 6. s

  sugi JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo kazi ngumu ni kuiongoza Tanzania tu?tatizo viongozi wetu wananuka ufisadi na ndo walotufikisaha hapa
   
Loading...