Kwa hili la mdahalo wa wagombea Urais, Lissu unazidi kuchemka

T2020JPM

JF-Expert Member
Sep 8, 2020
635
263
Kitendo cha mgombea wa urais kupitia chadema kuomba mdahalo na jemedari wetu Magufuli kimezidi kumpoteza kwenye ramani. Najua yupo busy na kampeni naomba wafuasi wake mliopo hapa jamvini mnijibu maswali yangu.

1. Baada ya kuzunguka sehemu mbalimbali ndani ya nchi akifanya kampeni, je Lissu ameona watanzania hawajamuelewa mpaka aombe kufanya mdahalo?

2. Anaposema mdahalo ufanyike kwa lugha yoyote je hajui kama kiswahili ndio lugha ya taifa? Na mdahalo usipofanyika kwa kiswahili aoni kama atakua hawatendei haki wapiga kura wake ambao hawazungumzi iyo lugha itakayotumika?

3. Anaposema kama jemedari Magufuli akikataa kufanya mdahalo itabidi tujiulize usomi wake, tangu lini mdahalo umekua ndio kipimo cha usomi wa mtu?

Aya kazi kwenu wafuasi wa Lissu kunijibu baadhi ya maswali yangu.
Ila msishau kuwa Magufuli kashaonesha uwezo mkubwa kuendelea kuongoza nchi kama rais na kufanya kampeni kwa wakati mmoja.
 
Hahaha UVCC mnatokwa jasho nyie wakati mgombea yupo?!

Mdahalo Magufuli aweze vipi, kwa lugha gani?! Labda kisukuma.

Tutasikia takwimu za madaraja hata yaliyojengwa kabla ya uhuru.

Hivi nyie uvcc a.k.a JESHI LA AKIBA mnalipwa na Bashiru?!
Baada ya kuandika porojo zako za kufikirika, naomba majibu comrade ni maswali matatu tu
 
Hahaha Bashiru kasha waharibu vichwa, aliwaambia mjibu hoja nyie mnatangatanga tu, mtalipwa kweli?!
Usinitoe kwenye reli comrade nasubiri majibu, wafuasi wa Lissu mnakwama wapi? Mnataka Lissu ndio awajibie kampeni atafanya saa ngapi?
 
Siyo mara ya kwanza kufanyika mdahalo na hii siyo nchi ya kwanza mdahalo utatusaifia kufahamu maono ya wagombea wetu hatutaki mtu achaguliwa kuwa Rais kwa mazoea badala ya uwezo wa kufanya hiyo kazi. Na pia hatutaki Rais dikteta wa kuwaza namna ya kutunyamazisha badala namna ya kuimarisha mifumo ya utawala ili kuwatetea maendeleo watanzania
 
Usinitoe kwenye reli comrade nasubiri majibu, wafuasi wa Lissu mnakwama wapi? Mnataka Lissu ndio awajibie kampeni atafanya saa ngapi?

Kila mgombea anajibu maswali yake. Nashangaa magufuli anamtuma Bashiru kumjibia hoja, na bashiru anawahangaisha watoto wa watu huku hata hamjui mnafanya nini?

Aliwaambia "Nendeni mkajibu hoja" siyo kujaza maandishi na hamna hoja wala majibu ya hoja.
 
Siyo mara ya kwanza kufanyika mdahalo na hii siyo nchi ya kwanza mdahalo utatusaifia kufahamu maono ya wagombea wetu hatutaki mtu achaguliwa kuwa Rais kwa mazoea badala ya uwezo wa kufanya hiyo kazi. Na pia hatutaki Rais dikteta wa kuwaza namna ya kutunyamazisha badala namna ya kuimarisha mifumo ya utawala ili kuwatetea maendeleo watanzania
Sasa mkuu kama unaamini kupitia mdahalo utatusaidia kufahamu maono na uwezo wa kufanya kazi kwa wagombea nadhani performance ya Magufuli inaonekana kwa macho sasa kuna haja gani ya kuja tena kujieleza kwenye mdahalo?
 
Kila mgombea anajibu maswali yake. Nashangaa magufuli anamtima Bashiru kumjibia hoa, na bashiru anawahangaisha watoto wa watu huku hata hamjui mnafanya nini?
Aliwaambia "Nendeni mkajibu hoja" siyo kujaza maandishi na hamna hoja wala majibu ya hoja.
Kawaida huwa sijadili vitu vya kufikirika najua huna ushahidi wa Magufuli kumtuma Katibu wake kujibu hoja. Narudi usinitoe kwenye reli comrade nijibu maswali yangu
 
Mnaogopa sababu mnajua hajiwezi, sasa kama wewe ni mtu wa vitendo,unajenga madaraja,unanunua mandege..uko analytical unajua watanzania tunataka nini and how you deliver them, kwa nini uogope mdahalo?lol
Tupo busy kuwaelezea watanzania nini tutakifanya kwa miaka mitano ijayo na njia pekee ni kupitia kampeni , madaraja na ndege vitajiongelea vyenyewe.
 
Kila mgombea anajibu maswali yake. Nashangaa magufuli anamtima Bashiru kumjibia hoa, na bashiru anawahangaisha watoto wa watu huku hata hamjui mnafanya nini?
Aliwaambia "Nendeni mkajibu hoja" siyo kujaza maandishi na hamna hoja wala majibu ya hoja.

Hana uwezo wa kushinda mechi zake.

Hana ujuzi wala uwezo wa kujieleza.

Hana uwezo wala ujuzi wa kupanga hoja.

Huyu jamaa kwa ujumla hafai!
 
Ndio utasikia watu wakiamini huyo baghsgoshahogryo alidefend PhD na kufaulu!

Hizi ni zile za kupewa angekuwa ni mdada degree za hivyo huwa zina majina yake.

Wanatukosea sana wanaokimbia midahalo. Tanzania ni zaidi mno ya mtu mmoja mmoja. Tanzania inahitaji midahalo kufahamu mbivu na mbichi.
 
Kwamba mdahalo Ndio utatupatia rais bora kabisa.

Mie namtazamo tofauti kabisa, watanzania tunapenda kuongea tatizo liko kwenye vitendo.

Na uwezo wakuongea inawezekana Ukawa hauendani na vitendo.

Kama lengo nikujua mgombea anatupeleka wapi, Nadhani kila Chama kina ilani yake imeandaliwa tayari zisome vizuri Ilani za vyama vyote Utajua malengo ya kila Chama.

Mdahalo ni muhimu sana ila sio Lazima ila Kama ratiba haikuwepo kwasasa wagombea wako busy ilipaswa mapema kwenye ratiba kuwe na muda huo.

Mdahalo pia usingeombwa na mgombea urais wa chama kimojawapo labda ungeombwa na Watu wengine. Anapoomba mmoja wa wagombea maana yake anamanufaa na huo mdahalo na anauhitaji Sana hivyo mgombea mwingine hawezi kukubali kwani sio sehemu ya silaha yake ya kushinda uchaguzi.
 
Back
Top Bottom