Kwa hili la Mbowe Marekani na Umoja wa Ulaya wamejitia aibu, ni rasmi sasa kuna kitu wanakitafuta Tanzania

Tangu mwanzo walio wengi walianza kuwa na shaka juu ya haya mataifa ya nje namna yanavyoitazama Tanzania.

Tukio la kuumia kwa mh Mbowe kama inavyodaiwa kuwa alishambuliwa lilileta taharuki kubwa kiasi cha mataifa haya makubwa kuja na matamko mengi.

Jambo la kushangaza ni kitendo cha Marekani na Umoja wa Ulaya kupitia balozi zao kutoa matamko yaliyoashiria kuihusisha serikali na tukio hilo.

Jambo ambalo si sawa kidiplomasia. Taarifa ya polisi imekuja kuwatia aibu baada ya kuthibitisha kuwa mh Mbowe hakushambuliwa na mtu.

Kila Jambo linalofanyika hapa kwetu wamekuwa wepesi sana kutoa matamko haraka bila kuyafanyia utafiti wa kutosha hii inatia shaka kuwa Kuna agenda za siri wanazo dhidi yetu.

Tangu Magufuli aunde serikali yenye msimamo mikali na kujiamini katika mambo mbali mbali basi imekuwa kesi kubwa kwa hawa watu.

Mifano mizuri hii:

Walilazimisha tuna Ebora kwamba tunaficha wagonjwa.

Wakatangaza Tanzania kuna magaida yatashambulia masaki bila kushirikisha serikali.

Wakazuia mkuu wa mkoa eti ananyima watu haki ya kuishi.

Kwenye corona ndio kabisaa kila siku ni kuisema Tanzania tu wakati huko kwao wanakufa maelfu.

Leo tena wamekuja na matamko kibao kuhusu kuumia kwa Mh Mbowe, wakishutmu serikali.
Haya leo wameumbuka tena baada ya ukweli kuwekwa wazi.

Kila siku wamekuwa watu wa matamko tu kwetu swali la kujiuliza ni je wanatupenda sana au ni kipi hasa?
Wana nia gani na sisi?

Wananufaika na nini na huu uzushi wanao utangaza dhidi ya Tanzania?

Watanzania tusipokuwa makini Hawa watu watakuja kutuundia vikundi vya waasi hapa kwetu kama hizi propaganda zao zitafeli.

Hawana upendo wowote kwetu hawa ni maharamia tu.
Ofisi za balozi wanapata taarifa moja kwa moja toka kwa wananchi hawataki taarifa za vyombo vya ccm, balozi zote wanaujua Ukweli jinsi ccm inavyowafanyizia wapinzani hata ukija na uongo wa kuwachafua Balozi za nje ni kama unajisumbua tu
 
Unachekesha wewe mpuuzi hivi mpaka kulaani unadhani wanategemea taarifa za polisi fisiemu,ambao Lisu kapigwa risasi na hakuna mtuhumiwa mpaka sasa hivi,wanachongea wanamaanisha masifi maji nyie watoa roho za watu
Dawa yenu ni kuwapuuza, maana mshakuwa kama nguruwe kila mtakachotupiwa kwenu ni chakula,

Nakuona ulivyo na hasira umefula vibaya kama NYUMBU vile
 
Wewe unajua nini?
Wewe umekuja na hoja ambayo kwanza ni nje kabisa na mada kuwa meli imekamatwa huko Libya ikiwa na bendera ya Tanzania.

Sasa nikuuliza Tanzania tuna meli ya masafa marefu hata moja.?
Jibu ni kwamba Tanzania hatuna meli za masafa marefu, sasa hujiulizi hiyo bendera ya Tanzania imefikaje huko kwenye meli ya watu.?
Alafu ina shehena ya silaha, Tanzania tunazalisha silaha sisi tangu lini?

Hao ni wahuni tu walio amua kutumia bendera yatu kwa makusudi yao binafsi.
 
Dawa yenu ni kuwapuuza, maana mshakuwa kama nguruwe kila mtakachotupiwa kwenu ni chakula,

Nakuona ulivyo na hasira umefula vibaya kama NYUMBU vile
ccm atampuuza nani? ccm angekuwa wa kupuuza asingekuwa anahangaika kuwafanyizia wapinzani angeacha kila mmoja aendelee na siasa zake
 
Wacha kutoa majibu mepesi kwenye masuala nyeti yanayo hitaji kutumia akili kubwa.
Wewe umekuja na hoja ambayo kwanza ni nje kabisa na mada kuwa meli imekamatwa huko Libya ikiwa na bendera ya Tanzania.

Sasa nikuuliza Tanzania tuna meli ya masafa marefu hata moja.?
Jibu ni kwamba Tanzania hatuna meli za masafa marefu, sasa hujiulizi hiyo bendera ya Tanzania imefikaje huko kwenye meli ya watu.?
Alafu ina shehena ya silaha, Tanzania tunazalisha silaha sisi tangu lini?

Hao ni wahuni tu walio amua kutumia bendera yatu kwa makusudi yao binafsi.
 
Mbona tulishawang'amuwa siku nyingi na wataendelea kuumbuka kila siku!! Wanaingizwa chaka kila mara na wasaliti wanaowafadhiri.
uling’amua na nani? Kwa kipi uling’amua? Siku nyingi zipi? Nani ataendelea kuumbuka? nyie wachache waonevu ndiyo mtaumbuka wenyewe
 
Back
Top Bottom