Kwa hili la maliasili, Pius Msekwa ajivue gamba

President Elect

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
693
212
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, amekiaibisha chama tawala kwa kuhusishwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka, akiwa mwenyekiti wa bodi chini ya wizara ya maliasili na utalii.

Inabidi aachie ngazi ili kurudisha imani kwa wana-CCM, na imani ya wananchi kwa serikali yao.
 
Gamba halivuliki hakuna aliye msafi ukizunguka huku masaburi,jairo,mbangwa,luhanjo,iddy simba,...............................naomba mwingine aendeleze list.
 
Magufuli kauza nyumba za nchi, sita katumia hela mfuko wa jimbo vibaya, shamshi mwangonga, msekwa, na mukama kaapendelea kampuni ya kin'gunge na kin'gunge pia mwingine aongeze list
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, amekiaibisha chama tawala kwa kuhusishwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka, akiwa mwenyekiti wa bodi chini ya wizara ya maliasili na utalii.

Inabidi aachie ngazi ili kurudisha imani kwa wana-CCM, na imani ya wananchi kwa serikali yao.

Hao si ndiyo wasafi kiasi cha kuwa taka wenzao wajivue gamba? maana kashfa ilianza kwa nape, sita sasa ipo kwa msekwa na hawa ndiyo watu ambao chama kimeeleza kuwa ndiyo watu safi, huu ni uthibitisho kuwa samaki mmoja akioza wote wameoza. Haiingii akilili kama wataendelea kumshinikiza Mzee chenge na Lowasa wajivue gamba wakati wao wana maganda. hapana hii haikubaliki. kama ni vipi wote wasulubiwe. vionginevyo wapotezee ishu nzima.
 
Gamba halivuliki hakuna aliye msafi ukizunguka huku masaburi,jairo,mbangwa,luhanjo,iddy simba,...............................naomba mwingine aendeleze list.

Hivi huyu Iddy Simba, si aliwahi kuwa waziri wa viwanda na biashara, akajiuzulu kwa kashfa ya vibali vya sukari?

Pius Msekwa naye ajiuzulu umakamu wa mwenyekiti CCM, kwa kashfa ya maliasili. Pia JK atengue uenyekiti wake kwenye Bodi ya uhifadhi wa Ngorongoro. Naunga mkono hoja.
 
Kwa heshima na taadhima, mzee wetu Pius Msekwa achia ngazi.

Uking'ang'ania madaraka mzee, utajikuta muda si mrefu unaburuzwa mahakamani, kama ilivyokuwa kwa wenzako, Basil Mramba na Daniel Yona.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom