Kwa hili la leo ni wazi kuwa CCM wamejiua!.

Nakubaliana na wewe mkuu, kwa spidi hii ya akina Mchemba, Nape, Komba n.k. hawa jamaa wao hata KUUA ili mradi CCM ibaki madarakani si tatizo kwao. CCM is getting out of hands na hawa "wahuni" wana nguvu humo!

Mkuu umegundua jambo KUU!!

" WAHUNI WANA NGUVU MMNO" .... Be Blessed for this vision!!

Ni Kwa CCM wao wenyewe kwa wenyewe kugawanyika ..ili kuweza KU NEUTRALIZE THE WRONG IN THEM NA KU BALANCE NATIONAL POLITICAL FORCES!!!

Kama usalama wa Taifa unapenda ki ukweli USALAMA WA TAIFA HILI ... WAO NDO WARATIBU MAPASUKO HUU HARAKA SANA!!!
 
Nionavyo mimi ccm imeshadumbukia chooni,
sasa imebaki kuua raia wasioipenda ccm,
leo hii hata wafanyakazi wa serikali hawaipendi ccm!
 
Mkuu unachosema wewe ndio kigumu na hatari kuliko nilichopendekeza ...!!

Hawa Liberal CCM wasanii na Wa babaishaji ... Ndio wenye DOLA , VYOMBO VYA USALAMA ...Mkuu watatuchinja watatumaliza ..hawa !! Hawafikiri na kuona katika hali timamu ...!!

Wanahitajika Watu wenye UTU na EXPIRIENCE KUBWA kuwakabili Hawa Wasanii na kuwanyanganya Zana za usalama wa Taifa kwa Busara ... Kwani sasa ... wamechanganyikiwa na malichoamua? NA LIWALO NA LIWE...Mkuu kuwachia hawa watu hata wiki mbili madarakani ... na Jeshi zima la Nchi likiwa mikononi mwao ...HUONI SYRIA IKINYEMELEA TANZANIA?

NAKUAPIENI WANAHITAJIKA WAKONGWE KUOKOA TAIFA HILI TOKA MIKONONI MWA " LIWALO NA LIWE" wataitosa Nchi Mtoni ... Hatimaye watasema ...LILE LIWALO LIMESHAKUWA..

Hima Watanzania wenye UTU, HEKIMA, BUSARA ...GAWANYANENI HIYO CCM MAPANDE MAWILI ...HARAKA SANA!!!!

Ni kweli kuwa CCM haiwezi kuachia madaraka kwa kura kirahisi. Japo wapo tayari kwa lolote, yaani liwalo na liwe, kuwaacha waendelee kupotezea nchi muda wa maendeleo ni mbaya na hatari zaidi. Hawa jamaa wana choice kuu mbili. Moja ni kukubali kushindwa uchaguzi wa 2015 kwa amani na ku-transfer power bila kuchubua mtu, wakifanya hivi watakumbukwa vizazi na vizazi na watastahili kusamehewa kwa missmanagement yoyote ile ili tuanze upya provided watakuwa tayari kurudisha hela walizoficha Uswisi.

Option ya pili ni kutumia mapinduzi ya kidola (Hapa sisemi kijeshi, maana wanaotawala ni raia wa CCM) kwa kuchakachua, kupiga watu na kujitangaza wameshinda, wakifanya hivi kuna mawili wanaweza kutawala watu ambao hawaongozeki, yaani hawakusikilizi zaidi ya wewe kuwalazimisha kama mtawala. Au watapambana na public pressure itakayowafanya watumie nguvu kubwa kuizima na hatimaye kuipeleka nchi kwenye fikra na mawazo ya avenge kwa wale watakaopoteza nduguzo. Hili likifanyika basi wajue kuwa The Hague inawanyemelea na itakuwa sasa ni nchi ya kipolisi zaidi ya kiraia. Athari zake ni kupungua kwa uzalishaji, uchumi kushuka, watalii kuikimbia nchi na hata wahisani kujitoa. likifanyika hili watatawala kwa kubangaiza na pale watakaposhindwa kulipa mishahara ya majeshi basi watakuwa wanajihakikishia maisha ya pressure zaidi.

I hope 2015 Akina Salim watawaashauri wakubali kushindwa na warudi kujipanga upya.
 
Kwa umbali kidogo naweza kuelewa unachomaanisha japokuwa hilo la 'CCM AA' ni Part II ya Movie ya 'Liwalo na Liwe'

No Mkuu, Hata ndani ya usalama wa Taifa, JWTZ, POLISI, Nk Bado Kuna Watanzania kwa Maana ya Watanzania WA KWELI KABISA ...!! Walikuwa wamebanwa tu!! Ni kama walikuwa maekufa ganzi na kuchanganyikiwa ...Lakini Sasa?

Ninaamini wanaweza kuamaka kwa dhati ya Miyo yao, Utu na Uzalendo na Kuchukua hataamu ... kwani wanjua kuw ahatuna miezi sita au tisa mbeleni kabala Taifa Halijaingia Mtoni!! Likayoyoma huku wao wamejikunyata na huku wana uzoefu na UJUZI Tele ya kuwanyangaya hawa Liberal CCM Silaha waisije kujiumiza wenyewe na wanachi wote.

Nikumabie nini?

Leo Liberal CCM wanakimbiza na kudaka watu na kuwaamuza ...soon wataanza kujirudia wenyewe na kujiumiza kabisa ... Nani haoni hilo!!

Wazazi wagongwe ...amkeni GAWANYA CCM MAAPNDE MAWILI ... Na vikosi vya usalama ..viratibu hilo ...!!! Vingine ni Majuto mazito hapo mbeleni ... Picha kamili angalienei Mzaha pale bungeni, Pale Ndago singda, Kwa Dr Uli na tamidhilia yote inayomuhusu nk

Hima CCM ipunguziwe uharibifu inayoweza kuufanya ... Kwa ... KUGAWANYWA MAPANDE MAWILI .. Nani afanye hilo ...sio CHADEMA ... ni CCM wenyewe!!!!
 
Mpaka saa inaonekana bunge halina linachokifanya bajeti mbovu zinapitishwa, mijada ya msingi kama hatima ya madaktari hawawezi kujadiri.
 
Wala sishangai yanayotokea! CCM wanajipanga kua chama pinzani hapo 2015.. tunayoyaona sasa ni rehersal tu sema rehrsal yenyewe wanaifanya kwa hasira
 
Kwanini wapinzani wasisusie vikao vya bunge?yani kilichotokea leo ni aibu sana,hivi hatuwezi kuitoa hii serikali ya ccm kabla ya 2015 maana naona kwa mwendo huu tutaangamia kabla ya 2015
 
Ccm washapoteza dira siasa imewashinda hawaiwezi tena nawashauri wabadilishe usajili wao kutoka chama cha siasa kuwa NGO labda huko wataweza
 
Mpaka saa inaonekana bunge halina linachokifanya bajeti mbovu zinapitishwa, mijada ya msingi kama hatima ya madaktari hawawezi kujadiri.

Bunge la maajabu
Bunge lisilo na Meno
Bunge la Spika anayesema waziri ajibu kwa ufupi
Bunge la Spika 'asiyesikia la mkuu'
Bunge la Kibabe
Bunge Kama ngao ya Serikali
Bunge la Tanzania
Bunge la Kuunda tume
Bunge la 'Hovyo hovyo'
Bunge 'Dhaifu'
Bunge 'Legelege'
Bungeeeeeeeeee...
 
wamebuni njia ya kukwepa na kuzuia aibu kwa kuwatumia polisi kukamata watu then wanawafunga mdomo watu wasijadili eti iko mahakamani, mi naona kama wanajimaliza zaidi

Polisi hawa cjui lini watakuja jitambua binafsi nawashangaa sana watu wanaongea mambo nyeti ya kuwanasua lkn wapi wameng'ang'ana kutumiwa tu wachache kutoka chama tawala
 
Muda mrefu sana kabla sijajiunga na wazo la Mageuzi na kuingia Chadema binafis yangu niliamini zaidi kwamba inawezekana CCM Asilia ambao ni Conservative wangeweza kujitenga na hawa vijana ambao wengi wao sii wanasiasa wala hawana fikra pevu pinzani ya Azimio la Arusha bali ni watu waliotungiwa itikadi na IMF wakajaa tele kama pishi la mchele.

Lakini haikuwa rahisi hata kidogo kwa sababu salim mwenyewe aliingia pasipo kuwa na Mtandano mkubwa nyuma yake, alikuwa na nadhani watu kaa Butiku na Warioba ambao sidhani kama walkikuwa na nguvu yoyote ndani ya CCM wakati huo. Inasikitisha hata Kingunge na Kawawa hawakuwa na nguvu tena isipokuwa kutazama sinema inavyochezwa maana hawakuhitajika tena isipokuwa heshima tu..

Huu ndio ulikuwa mwisho wa matumaini toka chama tawala na ndio maana sisi wengine tukajiunga na Chadema kwa sababu hapakuwepo na uwezekano tena toka ndani ya Chama cha Mapinduzi infact sasa hivi jina hilo linakifaa zaidi chama hiki maana haawa ndio - Liberal wa Azimio la Arusha! na kukubali kurudi ktk Utumwa..

Ukweli ni kwamba Mkapa na Kikwete ni marais wazuri sana wa kutetea mfumo huu uliopo isipokuwa ninmakosa ya wananchi kufikiria wangeweza kufanya tofauti kwa sababu huwezi kuweka maazimio ya Zanzibar halafu ukatetea maskini, uikatetea wakulima na wafanyakazi hii haiwezekani! Hivyo, ni sisi wananchi tuloshindwa kusoma alama za wakati.

Kuna wakati namwelewa vizuri sana W.J. Malecela kwa sababu yeye anajiunga na CCM kwa kutofautiana na misingi ilojengwa na chama hiki, ni muumini wa CCM hii mpya yenye kuthamini Matajiri na uwekezaji toka nje ndio wataweza kutuletea maendeleo. Sasa tunapomchukia JK kwa kuelta wawekezaji nchini wanaoiba rasilimali zetu, yeye hatuelewi. WanaCCM wa leo hawatuelewi kwa sababu kwao hizi ni mbegu zinapandwa leo na pengine in 20 years tutaona matunda yake..

Wewe na mimi tunayaona mahandaki na caves tu zikiachwa na machimbaji migodi, tunaona toxic zikimwagwa na kuharibu mazingira lakini wao wanaitazama fedha. Fikra za madhumuni ya CCM Asilia hayapo tena ila kumetokea Chama cha mapinduzi kinacho turudisha ktk Ukoloni Mamboleo na kwao hawaoni ubaya wake ikiwa sisi wenyewe tulishindwa na Siasa za Ujamaa na Kujitegemea..

Was there a better way? Ndio tuliyazungumza hapa sana tu mwaka 2001 hadi ujio wa JK mwaka 2005 tukitoa mfano wa China, Malaysia na kadhalika lakini enzi hizo kuiuza nchi ndio ilikuwa mbiu ya Kitaifa. Tukauza viwanda na Mashirika yote bila hata moja wapo kuingia soko letu la DSE na kuuza share kwa wananchi. wakaletwa wageni ambao hawakupewa mashatri yaliyoachwa na mwalimu ya kwamba hakuna shirika la nje litakalo weza kuwekeza nchini bila mwananchi kuwa share holder tena kwa asilimia kubwa ikawekwa..Yote haya yalipotea - Liberals wakaja na mfumo wa kugawana Umaskini ktk kutandaza sinia kubwa la biriani yetu mkekani..Kufumba na kufumbua sinia tupu nyama zote zimeshaondoka - TUmeliwa sisi..

Nilisema mwaka 2010 Kbala ya uchaguzi kwamba Chaema wangeweza tu kushinda kama watatafuta kiti kikubwa, na tukawapa pendekezo la Dr.Slaa wakajaribu na hakiika waliweza kuitetemesha CCM lakini bahati mbaya nitasema tena Dr.Slaa na Chadema hawawezi kurudia na kuupata Ushindi maana CCM wamejiandaa kama kawaida yao na mwongozo wao kwamba watafanya kila hila washinde Uchaguzi..

Na trust me Dr.Slaa hawezi kushinda kwa ukupitia sanduku la kura hilo tusijidanganye. Hawezi, ushindi ulikuwa wake mwaka 2010, kama Seif Sharrif Hamad mwaka 2000 baada ya hapo ni mchezo ule ule. Ila nafahamu kwa uhakika Chadema wanaweza tena kuizumbua CCM mwaka 2015 kama wataondoa kasoro zilizopo baina yao na viongozi wengine nje ya Chadema ambao wanajulikana ktk misimamo yao kitikadi, ni Wazalendo wenye kuunga mkono miiko na maadili ya viongozi sii hawa kina Shibuda ambao wanapigania nafasi zao bungeni..

Niliongea na kiongozi mmoja wa Chadema ambaye alinieleza mpango mzito sana waliouandaa mwaka 2010 kwa mazungumzo na CUF Bara lakini ilitokea mushkheri na Unafiki kiasi kwamba Uhasama mkubwa ukazushwa baina ya CUF na Chadema.. Lakini nadhani bado tunayo nafasi hiyo ya kuunganisha CUF bara na baadhi ya viongozi wanachama wa CCM Asilia wenye umaarufu mkubwa ktk system yetu inavyofanya kazi kuunda UMOJA wao dhidi ya Hawa Chama cha Mapinduzi...

Hili linaweza kuleta Uhsindi lakini bado sina imani na sanduku la kura, hivyo yawezekana tu kutokea mageuzi nchini kaa wananchi wataondoa Tofauti zao na kuwa wamoja kama ilivyotokea Misri au Tunisia kisha kuunda Baraza la Mapinduzi ambalo ndilo litasimamia uchaguzi utao fuata. Nje ya hapo jamani hakuna kitu, hakuna tena Conservative ndani ya CCM - Hakuna na kama wapo hawana nguvu tena ya ushawishi kwa sababu hata wao wanashindwa kujua watasema nini kuhusu Azimio la Arusha ilihali Azimio lile lilishindwa?.

Wasichofahamu ni kwamba lilishindwa ktk kufikia MALENGO lakini halikushindwa ktk MADHUMUNI yake..Na ndivyo itikadi zote hupwaya kufikia malengo kutokana na mazingira ya kiuchumi, wakati na mahitaji lakini haina maana kabisa kwamba madhumuni ya itikadi pia hupoteza umuhimu wake kwa walengwa...
 
Vyama vya upinzani vipo tayari,
CCM wanazidiwa kila dakika inayopita,
Kujigawa si solution,
Kufa ni solution,
Zanzibar kuna donda bichi,
Ubabe ndani ya CCM
Huku CDM inawanyima usingizi,
na kuungwa mkono na wananchi,
CCM itakufa kikahaba,
Ikiwa imelala na wawekezaji,
kitanda kimoja
 
....Pamoja na uandishi wako wa Riwaya ndefu (Nakubali kutofautiana nawe)
Nadhani kuna point nyingi ambazo umeziacha.. Umesahau kuwa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015 watanzania tunaweza kuwa na Katiba mpya itakayoweka utaratibu mzuri wa kupiga kura na Tume huru ya Uchaguzi hivyo kuondoa mizengwe.
....Pia umesahau kuwa Serikali ya Tanzania imegewanyika vipande viwili vikubwa (Kuna mawaziri na wabunge kadhaa tayari wameomba kujiunga na CHADEMA).
...Mwisho ili Tanzania itoke hapa ilipo inahitaji mtu mwenye uwezo wa kupanga na kuamua bila kukuna kichwa. Inahitaji KIONGOZI na siyo MTAWALA.
 
Vyama vya upinzani vipo tayari,
CCM wanazidiwa kila dakika inayopita,
Kujigawa si solution,
Kufa ni solution,
Zanzibar kuna donda bichi,
Ubabe ndani ya CCM
Huku CDM inawanyima usingizi,
na kuungwa mkono na wananchi,
CCM itakufa kikahaba,
Ikiwa imelala na wawekezaji,
kitanda kimoja

Mkuu nimeipenda hii
"CCM itakufa kikahaba ikiwa imelala na wawekezaji kitanda kimoja"
 
Huoni vibopa wa dunia,
Wakipishana ofisi za CCM,
CCM achanua chanu,
Wamtia rupia penyeza.

Eti mgeni wa CCM,
Tangu lini mwekezaji,
kawa mgeni wa chama?
ukahaba huu wa mchana,
CCM mtazaa Ibilisi.

CCM yauza mwili wake,
Yatoa uloda kwa vibopa,
Kupata mtaji wa 2015,
Ili kununua ushindi.

CCM kahaba tamania pochi,
hachagui wa kumdondokea,
Hunde na Ibilisi,
Wote washa mfanya.

Nahakika wala sibuni,
CCM itakufa kikahaba,
Ikiwa imelala na wawekezaji,
kwa pamoja kitanda kimoja
.

Mkuu nimeipenda hii
"CCM itakufa kikahaba ikiwa imelala na wawekezaji kitanda kimoja"
 
naombeni kuuliza...hivi wabunge wasipokua na imani na spika ni njia zipi wanaweza kuchukua kumg'oa madarakani? coz huyu mama ni one of the weakest speakers in the history ya bunge letu ni mbaguzi na anapendelea upande mmoja both yeye naibu wake na wenyeviti...
 
polis tz bado wana mbinu za kikolon na kuandaa maisha ya ukuu wa wilaya wakistaafu jesh so lazima waibebe ccm but time..
 
Mliozaliwa juzijuzi mna tabu ya kuielewa CCM ,CCM haitaondoka kwa mizozano ya kishoga pale bungeni,kuiondoa CCM ni kuhakikisha kunafanywa kwenye mikutano ya hadhara,mkoa kwa mkoa ,wilaya kwa wilaya kijiji kwa kijiji na nyumba kwa nyumba ,ni ile operation sangara ikiwa itafanyiwa kazi vilivyo basi CCM itakuwa haina maisha marefu sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom