Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 7,909
- 13,368
Salaam wakuu.
Wengi mtakuwa mmezipata habari za kimbunga kilichozua taharuki mjini Arusha. Binafsi nimekishuhudia na kujifunza mengi hasa juu ya umuhimu wa elimu ya majanga nchini.
Ilikuwa ni mida ya saa tisa kimbunga hichi ana sijui nikiite upepo wa vumbi, kilipovutuga mji mzima wa Arusha. Nilishuhudia watu wakikimbia huku na kule wengine wakijiuliza ni nini hiki huku baadhi wakikaza mwendo kisiwafikie. Ila ghafla kikatapakaa mji mzima (kila nilipopita nilikikuta)
Jambo moja lililonishangaza ni watu kukimbilia kujikinga kwenye miti na majengo/vibanda nikajiuliza hivi haya ni maeneo salama kweli kwao?, mara eneo moja nilipopita kile kimbuka kikaivaa miti wacha kianze vurugu watu huku na huku nusura wagongwe na magari taliyowasha full light kusaidia muono kwenye vumbi lile.
Kwa uelewa wangu sidhani kama kujificha kwenye miti na majengo/vibanda ni sahihi kwa hali hii ya kimbunga kwani inaweza kuvunjwa au kung'olewa na ukapata athari zilizoweza epukika. Pia swala la kupiga picha kiholela kwenye majanga kama haya si zuri.
Nitoe rai kwa jeshi letu la zima moto na wokozi tafadhali toweni elimu ya majanga hasa haya majanga ya asili kwani sasa dunia inakumbana na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.