sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Mbunge ni nani?
Mbunge ni mwakilishi wa walipa kodi ambaye anawajibika kwa wananchi na kwa Bunge kwa kuwa ndicho chombo cha uwakilishi wa wananchi.
Unapomtishia Mbunge wa wananchi usalama wa maisha yake, unawatishia wananchi waliomtuma pale. Hakujipeleka pale kama walivyo wabunge wa “Jimbo la Ikulu”, alikwenda kwa matakwa ya wananchi kusimamia maslahi ya umma.
Bunge letu ni la mfumo wa vyama vingi, hata iweje litapinga hoja za upinzani bungeni kwa hoja na si vinginevyo. Ndiyo maana kwa kupitia wingi wao(majority) Bunge limekuwa likipitisha maamuzi mengi yasiyo na tija kwa kuwa kiti cha Spika kinaongozwa na MNEC wa CCM na mwanachama wa chama hicho aliyeshindwa kuzuia mihemuko ya kichama.
Tumeona mara nyingi wakosoaji wa mifumo ya kiuongozi ndani ya bunge wamekuwa wahanga wakubwa wa mfumo huo kwa kudhalilishwa mara kwa mara na kutishiwa maisha yao hasa pale wanapo pambania maslahi mapana ya wananchi.
Hakuna asiyejua umuhimu wa kambi ya upinzani bungeni, umuhimu wake ndiyo unao lirudisha bunge kwenye mstari kwa kulikumbusha majukumu yake ya kibunge kwani ndicho chombo cha uwakilishi wa wananchi.
Ukitazama Bunge letu, huwezi amini kama ni chombo cha uwakilishi wa wananchi chenye majukumu ya kuisimamia serikali na kuishauri. Mijadala iliyoko pale, wabunge wa upinzani wanaikosoa serikali na kuielekeza na wabunge wa chama kinachotawala wanapinga na kuitetea serikali ya chama chao iliyoko madarakani, ndiyo maana kwa dhana hii Bunge letu linaonekana dhaifu.
Kwa udhaifu huu, chombo hiki kimeshindwa kwa makusudi kuwasimamia wabunge wake hususani wa upinzani pale wanapotishwa na watendaji wa mhimili wa serikali kutoka kitengo maalumu (intelligence special unit).
Kwa kitendo cha kumtishia mwakilishi wa wananchi bungeni kama alivyothibitisha mh. Zitto Zuberi Kabwe, ni kinyume na haki na kinga za mamlaka ya bunge kwa wabunge. Ikiwa Mbunge anatishwa sisi tuliomtuma ajatuwakilishe tupo salama kwa kiwango gani!!!!
Ni wakati wa kiti kulitazama jambo hili kwa upana wake, huenda maadui wa bunge wakatumia fursa hii kulichafua bunge zaidi wakidhani wanalisaidia.
Hoja za wabunge hujibiwa kwa hoja na si vitisho, tukiruhusu hawa wasiojulikana kuliingilia bunge letu tutaharibu afya ya mjadala.
Kwa kuwa Bunge si idara ya serikali bali ni mhimili unaojitegemea, halina budi kurudi kwenye majukumu yake ya kiutendaji kwa mujibu wa katiba, sheria na kanuni, kwa kuachana na ubabe usio na tija kwa maslahi ya taifa.
Tunamtaka Mh. Spika aunde Kamati ya kuchunguza matukio yanayotishia uhai wa wabunge wake ili kurudisha imani na Bunge letu kuwa salama kwa wabunge wake wote bila kujali itikadi, vinginevyo ukimya huu wa bunge tafsiri yake ni kubariki vitendo hivi vya vitisho.