Uchaguzi 2020 Kwa hili la kuenguliwa Wagombea wa Upinzani, tuna la kujifunza

fenestra rotunda

JF-Expert Member
Jun 18, 2015
608
614
Wakuu salaam,

Baada tu ya wagombea ubunge na Udiwani wa CHADEMA kuchukua fomu maeneo mbalimbali Tanzania watu walitoa ushauri jinsi ya kuepuka makosa kama yale ya 2019.

Katika majimbo yote ya Uchaguzi ni majimbo machache saana ambayo niliona wagombea wa ngazi mbalimbali wakiongozwa na wagombea ubunge wakifanya vikao vyakujifunza jinsi ya kujaza fomu kwa usanii. Mathalan John Heche alifanya vizuri sana katika hili, ingawa wengi humu jamvini walimbeza na kumsimanga.

Lakini cha ajabu kwenye haya majimbo ambayo vikao vya kujaza fomu vilifanyika, sijawahi sikia wagombea wa ngazi yoyote wakienguliwa wala kuwekewa pingamizi. Hili linanifanya nifikirie kuwa kuna uzembe wa wazi ulifanyika kwenye majimbo yeye matatizo na hawakuwa serious kuwafunda wagombea wao namba nzuri ya kujaza hizo fomu kwa usahihi na wala hakukuwa na msisitizo wa kutosha kwa viongozi wa ngazi zote kuhusu hili.

Mara nyingi maelekezo yaliyo mazuri yalikuwa yanatolewa twitter na Martin Maranja. Ila cha kujiuliza ni kuwa je, wagombea wa ngazi zote wapo twitter useme kwamba labda wangefuata maelekezo murua ya yule kada? Je, kina nani walikuwa responsible kuhakikisha hamna kosa katika ujazaji fomu ukiacha mambo ya wakurugenzi? Kwa nini hawakuamua wote kwa pamoja kufanya kama alivyofanya Heche kule Tarime vijijini?

Jambo lingine ni kama walifanya vetting ya kutosha kwa wagombea wao kuhakikisha hawana makandokando mathalan mgombea ubunge Jimbo la karagwe aliyeenguliwa kwa kukwepa kulipa kodi na yeye kutokuwepo kutoa utetezi.

Niwakumbushe wana CHADEMA kuwa the playing field is tilted and and the game is not fair, otherwise tutaishia kulalamika kila uchaguzi with no action to take. Ukishajua kuwa mfumo unaopambana nao hauko upande wako wala haukujali basi jaribu kabisa hata yale maeneo madogo kama kujaza fomu uzifanyie perfection. Nionavyo kwa sasa we are too late katika hilo.
 
Back
Top Bottom