Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Succession plan - ule uwezo wa kuandaa kesho kwa kutumia uzoefu uliopatikana leo na jana. Hiyo ni tafsiri yangu ambayo inaweza kupingwa na mtu yoyote yule.
Kisiasa succession plan ni ule uwezo wa kuandaa wanasiasa wa kesho kwa kutumia namna mbalimbali za kuwapa uzoefu wakiwa katika umri mdogo.
Jakaya Kikwete, Edward Lowassa na makada wengine wa umri wao walikuwa wakipewa uzoefu wa siasa kwa kuwa karibu na Mwalimu Nyerere pamoja na wakongwe wengine wa siasa. Kizazi cha kina Nyerere kilipoondoka kina Kikwete wakawa wameshaiva kuwa viongozi.
Ally Hapi, Paul Makonda na wenzao wa umri wao walikuwa wakipata uzoefu wa mambo ya siasa kwa kuwa karibu na Jakaya Kikwete na wengine ambao ni wakongwe kwao. Yale ambayo kina Kikwete waliyapata toka kwa kina Nyerere yanarithishwa kwa kina Makonda. Hiyo ndio maana ya succession plan, hiyo pia ni sifa ya chama makini cha siasa.
Inapokosekana succession plan chama cha siasa kinakuwa kama kundi fulani la wapigaji, kunakuwa na ubinafsi wa hali ya juu.
Lakini succession plan haiondoi madhara ya ufisadi ambao umekuwa ukiitesa CCM kwa muda mrefu. Urithishwaji wa uzoefu wa kisiasa huzalisha wanasiasa wa baadae, na hili ni jambo jema sana kutiliwa mkazo na vyama vyote vya siasa, kwa faida ya uhai mrefu wa vyama.