Kwa hili la DCI Manumba unapata fikra gani kichwani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili la DCI Manumba unapata fikra gani kichwani??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KakaKiiza, Feb 20, 2012.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  • DCI Manumba juzi alitoa Repoti juu ya ugonjwa wa Dr Mwakyembe ambayo inaelezea kwa wao kama polisi wanachokiamini na ndiyo kauli ya Jeshi la Polisi.
  • Wizara ya Afya na kutokana na maelezo ya Waziri mwenye dhamana amepinga kwakutojua hiyo riporti ilikotoka akaongezea labda polisi wanambinu nyingi za kupata habari.
  • Dr Mwakyembe yeye amekanusha kwakusema yeye ana riporti mwenyewe nakama manumba anareporti na anachokieleza kwa waandishi basi nitofauti na reporti yake!!
  • Waziri wa Afrika Masharika Mh Sitta yeye anasisitiza kwamba Dr Mwakyembe alilishwa sumu sasa ninani yuko sahihi??Kwa mkanganyiko huu wewe unapata fkira gani kwa hizi Taasisi nne kwa kuvuruga watu??


  Je DCI Manumba alikuwa anasababu gani ya kusema hii ndiyo riporti ya ugonjwa wa Mwakyembe??Niwapi alipata vipimo je mkemia waserikali anaemaje mbona yeye yupo kimya??
   
 2. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Manumba anatumiwa ni watu wanaopewa vyeo wakiwa hawana uwzo wa kutosheleza. Hajui alifanyalo maskini ya Mungu, kwenda shule kuna mtu kasema hivi hufuati shule unafuata elimu maana shule utaiacha elimu utaondoka nayo. dhiki tu
   
 3. m

  mchambakwao Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu,Manumba amenukuliwa jana mamesema kuwa "Suala hili sasa litashughulikiwa kisheria" Sijui hapo mwanzo lilikuwa likishughulikwaje?
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KAULI TATA ZA DCI MANUMBA:
  MIKANGANYIKO YOTE HII YA SERIKALI YA CCM NA MAUAJI YA 'KI-JASUSI' KWA DR MWAKYEMBE JE MHESHIMIWA ASINGALIKWEPO BADO DUNIANI WATU TUNGESIKIA NINI TOKA KWA HII SERIKALI YA LOWASSA NA KIKWETE?


  Nafuu Dr Mwakyembe mwenyewe yupo akasikie kwa masikio yake mwenyewe hii serikali ya CCM alioitumikia kwa miaka mingi sana na katika mambo mazito zaidi jinsi gani kinavyomnango na tatizo la ki-afya ambalo mbegu yake ilipandwa vipi, na nani, lini na kwa malengo gani yote wanayafahamu yote.

  Ugua pole Dr Mwakyembe, Mungu yupo na anao uwezo wa jabu usiofahamika undani wake kwa binadamu wa kawaida.

  Amini utaishi, na wale wote waliohusika katika haya kamwe malengo yao kukutumia wewe kama jiwe la kupandia kuelekea kuutwaa urais wa JMT bora wakasahau kabisa hizo ndoto!!!!!!!!!


   
 5. K

  KIMU Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli ni dhahiri kabisa ya kuwa tulipofikia ni pabaya watu hawana hofu ya Mungu kabisa, lakini ikumbukwe ya kuwa hakuna masika........... Pole sana Dr. Mwakyembe hata wananchi tunaamini maneno ya kinywa chako ndio yenye ukweli
   
 6. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,833
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Huyu Manumba hafanyi kazi kama mtaalamu aliyetaalamikiwa na taaluma ya ukachelo, bali anafanya kazi kisiasa zaidi. Ndio maana comment zake nyingi ni kusaidia chama tawala, inafaa sana avuwe magwanda abebe kadi yake ya sisiemu basi apande majukwani aanze siasa huko aliko sijui gorafa ya tano Ghana/Ohayo rd ni kama ameingia choo cha kike.
   
 7. Mabwepande

  Mabwepande JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huyo Manumba kazi yake si ni Kubambikizia watu kesi.
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  we manumba,mwakyembe si classment wako pale udsm?

  kweli yuda aliacha wafuasi.
   
 9. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na wala si kutumikia magamba.. Ni kutumikia mafisadi papa!

  We Mwakyembe mwenyewe kasema amesoma UD na Manumba,na IGP Mwema ni mwanafunzi wake..

  Lakini bado anasisitiza haogopi kuitetea nchi yake.. Na kasema ataendelea kuipigania nchi yake,na akataja kuwa atakapopona,ataanza na Kagoda na EPA.

  Na akamalizia kwa kusema Mungu aibariki Tanzania...
   
 10. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  DCI is a satanic robot that works by being by remotely operated either by EL or AR. Richmond didn't deliver (deliberately by EL and AR conning tricks) so Dowans was invited as planned.


   
 11. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ni ukweli usiopingika kwamba wapo watanzania innocents walioko walioko magerezani kwa ajili ya utendaji mbovu wa viongozi kama hawa. Wapo wanaoteseka na wengine kupoteza maisha lakini rais wetu ametia pamba masikio yake na kufunga macho yake. Sielewi haya hayamhusu? Au kawaagiza waifanye kazi hiyo na ndiyo maana kakaa kimya kwani utendaji wa wasaidizi wake unaridhisha. Mungu iokoe Tanzania na viongozi wasiowajali watanzania.
   
 12. k

  kuzou JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  manumba hakikisha unamshtaki sita,ahaa kumbe jalada lipo kwa AG,sasa mshnikize ashtaki akiseama ushahidi hautoshi panda pipa mpaka appolo,leta ushahidi kwamba sumu hiyo ni ya ulanzi
   
 13. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...ufalme umefitinika, hayo hayana budi kutokea.
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Jamaa by profession ni Jambazi. Yeye na ripoti ya kitabibu wapi na wapi? On the other hand Sitta was right
   
 15. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,078
  Likes Received: 7,295
  Trophy Points: 280
  No,
  Nadhani anafanya kazi kama Mganga wa kienyeji kwa kutumia ramli
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mleta mada hujasema kweli hata moja.

  Hiyo ripoti ya Manumba ioneshe na mnukuu kasema nini.

  Mwakyembe pia hajaelezea kuwa kawekewa sumu. Ni wapi aliposema kawekewa sumu? Na aliyemuwekea nani?

  Sitta kasema kama unavyosema wewe au mimi, sio msemaji wa Serikali wala madaktari.

  Waziri wa afya hajakanusha chochote, kasema mkawaulize waliowapa hiyo habari.

  Nini uisichokielewa hapo? Kila mmoja kasema kwa wakati wake na kwa ujuzi wake.

  Msilazimishe ambayo hayajaandikwa.
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Majibu ya sokoni kwa mambo mazito kama haya tena yanayowauma sana WaTanzania wengi sana moyo juu ya Dr Mwakyembe na mkasa uliomtokea wakati AKITETEA MASLAHI YA UMMA dhidi ya mafisadi waliokubuhu!!!

  Nasema swala la Dr Mwakyembe ni nzito kuliko jinsi ambavyo watu wengine ndani ya serikali ya CCM wangependa lionekane kwetu sisi wananchi.

  Hakika tunawasikitikia sana wale wote wanaoufanyia utani mashaibu ya Dr Mwakyembe mjue mnachezea uhai wa mtu hapo.

   
 18. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huyu DCI MANUVA inatakiwa wapigwe mawe mpaka afe.
  kabla ya hapo inatakiwa atueleze
  BALALI YUKO WAPI mana hizi sarakasi zao hatuzielewi kabisaaaaa
   
 19. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkuu, Watanzania tunataka kujua ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya watuhumiwa waliotajwa katika taarifa ya Mwakyembe kwani taarifa ile kwa sehemu tuliyosoma kutoka gazeti la mwanahalisi iko wazi kabisa. Watanzania tunapata hasira tunapoona watuhumiwa hao wanapewa tuzo na kupandishwa vyeo na wengine kuhamishwa kutoka eneo moja kwenda eneo lingine. Lakini mbaya zaidi wanaotoa taarifa za njama hizo ndio wanaonekana wazushi na maadui hata viongozi kuwataka watanzania wawapuuze wakati tuna uwezo wa kujua nyeusi na nyeupe. Hizi enzi ni tofauti.
   
 20. M

  Mwanyava JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuna mtu alileta taarifa hapa JF akisema kuwa kulikuwa na njamaa ya kuipata taarifa ya ugonjwa unaomsumbua Dr. Mwakyembe na kwamba 40M zilitengwa au alipewa mtu wa hospitali ili kufanikisha uchakachuaji huo. Watu walichangia walivyoweza ...
  Labda hiyo taarifa baadala ya kupelekwa vyombo vya habari (magazeti) wameamua kumtumia DCI Manumba. Ingependeza Manumba atwambie amelipwa shs ngapi kuusema uongo uliyochakachuliwa na mafisadi !!!
  Inasikitisha shana watu wanaotakiwa kuwalinda raia wote bila kubagua wanakuwa walinda masilahi ya mafisadi kwa kuwa wanalipwa hela. Mungu awalaani.
  Kila jambo lina mwisho kwa kuwa hata mafisadi nao wataonja mauti hata kama wanajitaidi kuwatanguliza wengine wanaowapinga ktk ufisadi wao.

  Tumuombee Dr. Mwakyembe ili Mungu azidi kumpa uponyaji.
   
Loading...