Kwa hili la CHADEMA kuvunja uongozi wa majimbo Mkoa wa Dodoma

NZURI PESA

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
5,959
2,938
Habari wadau, nimesikia katika kipindi cha tuongee magazeti cha RFA kuwa CHADEMA imeuvunja uongozi wa majimbo ya mkoa wa Dodoma kwa kile kinachodaiwa kushindwa katika uchaguzi mkuu.

Niueleze tu kwa uongozi wa Dodoma mjini aliyepaswa kuondoka hapo labda Massawe lakini watu kama Fred na Ishengoma, mama Mbahuka nk ni kikosi kazi cha CHADEMA Dodoma mjini hao jamaa wanaipaisha CHADEMA Dodoma kwa nguvu zao, mlichopaswa kufanya ni kuwawezesha tu waweze kutenda zaidi.
 
Kwa Dodoma wanahitaji nguvu za ziada.Wasipokuwa makini wanaweza kuvunja uongozi kila baada ya uchaguzi mkuu.
 
Wananchi wa Dodoma huwa hawajuagi kama kuna vyama vingine wao wanakijua chama kimoja tu Chama cha mapinduzi tena sahiv ikulu inahamia Dodoma watachagua ccm kizazi hadi kizazi
 
Ni cham pekee kinachothubutu kuondoa viongozi wabovu, ccm kazi yao ni kutoa matamko tu lakini hawathubutu kufuta uongozi hata wa mlinzi wa majengo.
 
Chadema mara zote inabadilika. Tofauti na chama kama ccm ambacho kinasema kila siku, wiki, mwezi, mwaka, muongo na karne kuwa ni kile kile~ccm ni ile ile.

Dodoma wataamka tu.
 
Habari wadau, nimesikia katika kipindi cha tuongee magazeti cha RFA kuwa CHADEMA imeuvunja uongozi wa majimbo ya mkoa wa Dodoma kwa kile kinachodaiwa kushindwa katika uchaguzi mkuu.

Niueleze tu kwa uongozi wa Dodoma mjini aliyepaswa kuondoka hapo labda Massawe lakini watu kama Fred na Ishengoma, mama Mbahuka nk ni kikosi kazi cha CHADEMA Dodoma mjini hao jamaa wanaipaisha CHADEMA Dodoma kwa nguvu zao, mlichopaswa kufanya ni kuwawezesha tu waweze kutenda zaidi.
Wajinga hao. Utategemeaje wafanye vizuri wakati hawata kuwezeshwa hawawezeshwi. Wanawategemea wafanye siasa kwa pesa zao mfukoni ikija wakishinda na kupata ubunge, wanakuja moto kudai ruzuku na kuzipangia matumizi wao wenyewe. wanataka kupata mtaji kwa kupitia migongo ya wengine. Chama gani hiki. Et alafu leo wanakuja na matamko ya kusimamisha watu. Wanajua ni muda kiasi gani wamepoteza. Wanajua pesa zao kiasi gani zimetumika. Wanaweza kuwafidia? Tukihoji tu mapato na matumizi ya chama mnatuona wasaliti. Ziko wapi pesa tulizochanga kupitia mitandao mwaka jana. Mtasema mmetumia kufanya kampeni. Hahahah. Mtakua Mmetakatisha pesa kirahisi sana
 
Chadema mara zote inabadilika. Tofauti na chama kama ccm ambacho kinasema kila siku, wiki, mwezi, mwaka, muongo na karne kuwa ni kile kile~ccm ni ile ile.

Dodoma wataamka tu.
Dodoma wataamka kwenda wapi. Kwa kutumia ajenda gani. Labda tuhabarishe vizuri. Tunachojua chama kwa sasa hakina ajenda ya kusimamia. Sanasana ni ajenda za kuwatetea wanaotumbuliwa na Magufuli
 
Back
Top Bottom