Kwa hili la CDM jangwani kweli Dar ina wenyewe

Wakuja mwingine huyo, utujibu tu ulikuja kwa usafiri gani wa treni, fuso, basi au nn ? na ilikuwa wakati wa kampeni gani, za mwenge, uhuru au nn ?

walianza ooh wadini..wakaja ooh kaskazini iyo..imeingia jijini wanaanza ooh WAKUJA wale..mwisho wa siku mnasema cdm inawagawa watz lakini mnaweza kujipima kwa maneno yenu na kauli zenu..hata ivyo kwani wanaopiga kura za dar ni wakazi wa maneromango,vikindu, kimanzichana,mkuranga au ni wakazi wa jiji(wakuja)?..acha kujidanganya..kujifariji gani kumekaa hivyo..
 
Kampeni za ccm zakufunga wakati wa uchaguzi wa 2010 watu uwanja ule walijaa kuliko haw a wa cdm , nilishangaa kuona jangwani uwanja una gap kubwa sana japokuwa matangazo mliyafanya kwa nguvu sana. Duh kweli cdm Dar hamna lenu, napendekeza makao makuu ya cdm yahamie arusha

Ni kweli mafuso yalileta watu wengi si uliyaona? Mbaya zaidi gharama za kuwaleta watu zilitokana na kodi yetu tukiwemo tusio na chama cho chote. Ila niliona kama tarehe 26/5/2012 watu walitembea kwa mguu kuelekea jangwani. Sidhani kuwa wewe ulikwenda kwa miguu yako; nahisi ulitumia gari ya serikali yenye namba bandia.
 
Tathmini ya kisayansi ya mkutano wa cdm jangwani ni kama ifuatavyo :
  • Imedhihirika kweli DAR KUNA WENYEWE na si kama Arusha, kwani kwa idadi ya watu , Dar ina watu wengi kuliko Arusha , ila Arusha kwenye mikutano ya cdm watu wengi hujitokeza kuliko hata wale walioonekana jangwani pale kwenye kile ‘kijiumati’ japokuwa matangazo yalikuwa mengi. Hii yadhihirisha Dar ina wenyewe, na wengi wetu ni wakuja si wana Dar kindaki ndaki
  • Mbowe adhihirisha ni mgeni na historia ya Dar. Uwanja wa Jangwani anaujua historia yake? Ni jambo la kushangaza na kustaajabisha kuuita uwanja wa jangwani ni ‘cdm square’. Wenye hadhi hiyo ni wakazi wa Dar wenye kuujua asili ya uwanja ule, mtu km Mbowe wakuja hadhi hiyo ameipata wapi? Ni jambo la ajabu na kustaajabisha
  • Cdm kwa dar mambo ni magumu sana, tuliambiwa kwenye kwenye magazeti (na sijui km ni kweli) kuwa kwa arusha na yenye watu wachache kuzidi Dar watu 10,000 walirudisha kadi, ila kwa Dar na yenye watu wengi zaidi ya Arusha ni 3100 tu. Ndio narudia kusema Dar ina wenyewe sio mji wa kuvamia vamia tu
Kwa haya machache yaonyesha wazi cdm kwa Dar mna kazi ya ziada, Dar ina wenyewe sio km Arusha. Na wengi waliojitokeza kwenye ule mkutano 80% ni wakuja si wana Dar kindaki ndaki.

Ulichotumia kufikiri ungetumia kwa mambo mengine uchumi wako ungeimarika isue za DIDAS
 
cdm bana badala yakujibu hoja wanabaki wanalalamika km mwenyekiti wao pale jangwani, analia lia weeee polisi wamuonee huruma na tume ya katiba iwaonee huruma. Na ww tena hapa unamuiga na ww unalia , tukusaidiaje?

gamba wewe, hata ufanye nini limegoma kuvuka na unaswampa nalo tu, hamuwezi kusalimika tumeshawabamba.

M4c kama kawa kama dawa.
 
Huyu jamaa hata simsomi...hata hao anaowaita wakuja si ni Watanzania kama yeye anavyojiita wa Dar kindakindaki au naye ni mzanzibari mwingine huyu. Tuwekee thread yenye utashi watu wachangie na sii huu upuuzi.
 
jamani naomba huyu jamaa aelewe kuwa nchi hii kila mtu anaruhusiwa kuishi na kuweka makazi yake popote kwa kufuata kanuni na taratibu zilizopo bila kuvunja sheria,,,,wakazi wa dar ni wengi sana ila na asilimia kubwa siyo wazaliwa wa pale lakini hao wanahaki ya kupiga kura kama wamejiandikishia huko,,,,, cdm hawakufanya mkutano wakiwatafuta wazawa wa dar kama ingekuwa hivyo ila walikutana na watu wote bila kuhoji huyu mtu ni mzaliwa wa wapi, tukiangalia hivyo hata arusha siyo wakazi wote ni wazawa wa arusha watu wametoka sehemu mbalimbali kutafuta maisha jambo ambalo haliwazuii kuhudhuria mikutano ya siasa kama mwandishi anavyotaka kutuaminisha.

Idadi ya watu waliojitokeza pale tunasema ni wakazi wa dar kwakuwa mkutano ule ulifanyikia mkoa huo naomba mwandishi kama uliumia sana usitake kuanzisha vijisababu visivyo na msingi,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,sikutegemea kama kuna mtu anaweza sema sehemu au mkoa fulani "una wenyewe" nchi hii ni mali ya kila mtu kama ni hivyo mbona watu wanaomiliki asilimia kubwa ya maeneo ya dar siyo wazawa??????? Tena inawezekana wewe huna hata hatua moja ya kijisehemu cha kukuzikia tu. Ndugu zangu tumpuuze huyu mtu sana

Wenye dar , nakupa assignment watafute wakina Mzee iddi simba, wakina mzee sykes nk watakupa habari za wenye dar. Ww ni wa kuja tu, na hakuna sehemu tanzania hii isiyokuwa na wenyewe, usijiaibishe kwa kutojua hilo.
 
Huyu jamaa hata simsomi...hata hao anaowaita wakuja si ni Watanzania kama yeye anavyojiita wa Dar kindakindaki au naye ni mzanzibari mwingine huyu. Tuwekee thread yenye utashi watu wachangie na sii huu upuuzi.

Na mkianzisha siasa za majimbo, itabidi mwende mliko tok a kwani hatutahitaji wakuja wa dar
 
gamba wewe, hata ufanye nini limegoma kuvuka na unaswampa nalo tu, hamuwezi kusalimika tumeshawabamba.

M4c kama kawa kama dawa.

Enheeeeeee na ww nae umekuja kuimba taarabu km wenzako badala yakujibu cha maana, hv man matatizo gani nyie watu , au ndio hali ngumu ya maisha inafanya mpaka uwezo wenu wakufikiri mdogo kiasi hiki ?
 
Ulichotumia kufikiri ungetumia kwa mambo mengine uchumi wako ungeimarika isue za DIDAS

Wale wale km wengine, kweli cdm ni chama cha wahuni, wote ngonjera tu ngonjera tu hakuna hata anae jibu kwa hoja zenye mashiko
 
walianza ooh wadini..wakaja ooh kaskazini iyo..imeingia jijini wanaanza ooh WAKUJA wale..mwisho wa siku mnasema cdm inawagawa watz lakini mnaweza kujipima kwa maneno yenu na kauli zenu..hata ivyo kwani wanaopiga kura za dar ni wakazi wa maneromango,vikindu, kimanzichana,mkuranga au ni wakazi wa jiji(wakuja)?..acha kujidanganya..kujifariji gani kumekaa hivyo..

Najua hii kitu inawauma sana kusemwa ni wakuja ila ni hali halisi , ww dar ulikujaje ?
 
Kweli huna unalolijua kama member mmoja alivyosema. Bila kumung'unya maneno, ingekuwa CCM haikuchakachua matokeo kule Segerea CDM ingekuwa na majimbo mangapi Dar na CCM ingebaki na mangapi?

Kampeni za ccm zakufunga wakati wa uchaguzi wa 2010 watu uwanja ule walijaa kuliko haw a wa cdm , nilishangaa kuona jangwani uwanja una gap kubwa sana japokuwa matangazo mliyafanya kwa nguvu sana. Duh kweli cdm Dar hamna lenu, napendekeza makao makuu ya cdm yahamie arusha
 
Tathmini ya kisayansi ya mkutano wa cdm jangwani ni kama ifuatavyo :
  • Imedhihirika kweli DAR KUNA WENYEWE na si kama Arusha, kwani kwa idadi ya watu , Dar ina watu wengi kuliko Arusha , ila Arusha kwenye mikutano ya cdm watu wengi hujitokeza kuliko hata wale walioonekana jangwani pale kwenye kile ‘kijiumati’ japokuwa matangazo yalikuwa mengi. Hii yadhihirisha Dar ina wenyewe, na wengi wetu ni wakuja si wana Dar kindaki ndaki
  • Mbowe adhihirisha ni mgeni na historia ya Dar. Uwanja wa Jangwani anaujua historia yake? Ni jambo la kushangaza na kustaajabisha kuuita uwanja wa jangwani ni ‘cdm square’. Wenye hadhi hiyo ni wakazi wa Dar wenye kuujua asili ya uwanja ule, mtu km Mbowe wakuja hadhi hiyo ameipata wapi? Ni jambo la ajabu na kustaajabisha
  • Cdm kwa dar mambo ni magumu sana, tuliambiwa kwenye kwenye magazeti (na sijui km ni kweli) kuwa kwa arusha na yenye watu wachache kuzidi Dar watu 10,000 walirudisha kadi, ila kwa Dar na yenye watu wengi zaidi ya Arusha ni 3100 tu. Ndio narudia kusema Dar ina wenyewe sio mji wa kuvamia vamia tu
Kwa haya machache yaonyesha wazi cdm kwa Dar mna kazi ya ziada, Dar ina wenyewe sio km Arusha. Na wengi waliojitokeza kwenye ule mkutano 80% ni wakuja si wana Dar kindaki ndaki.

WASI KWA MANENO YAKO KAMA ULE UMATI WOTE NI WA WAHAMIAJI WA DAR, ELEWENI TAYARI MMESHAUPOTEZA MJI. wATU WENGI VILE WAWEZAJIGAMBA KUWA SIYO WATU WA DAR? AU KWAKUWA WALE WAZEE WA DAR WA KAHAWA HAWAKUWEPO? UMEWASAHAU WALE MKULU ANAOPENDA KUWAITA NA KUONGEA NAO?
 
wengine ni wadau wa ccm lakini huu ni upuuzi wa ajabu..mwana ccm halisi hana siasa za kibaguzi kama wewe.nyie ndio wale wana uamsho nini??
 
Basically hii ni Makala ya kujifariji!! Kwani watu wengi walivyosikia ni live coverage Hawakuweza kufika jangwani kutokana na Jiografia ya dsm!! Ila msg sent!! Usafiri wa public dar ni kero ndio maana hata baadhi ya watu Hawakufanikiwa kufika
 
Wenye dar , nakupa assignment watafute wakina Mzee iddi simba, wakina mzee sykes nk watakupa habari za wenye dar. Ww ni wa kuja tu, na hakuna sehemu tanzania hii isiyokuwa na wenyewe, usijiaibishe kwa kutojua hilo.

Asili ya DSM ni Wazaramo, sasa hawa wazee uliowataja ni Kabila ipi vile.

Mwenzio sijajuagaaa!!!!!

KIMBUNGA iNAKUJA!!!!!!!

MIZAMBWA
NABII MTARAJWIA
 
Basically hii ni Makala ya kujifariji!! Kwani watu wengi walivyosikia ni live coverage Hawakuweza kufika jangwani kutokana na Jiografia ya dsm!! Ila msg sent!! Usafiri wa public dar ni kero ndio maana hata baadhi ya watu Hawakufanikiwa kufika

Mtasema mengi tu, ila ukweli lazima tuuseme, hakuna sehemu nchi hii isiyo na wenyewe, sasa nyie tukiwaambia hilo mnasema ubaguzi
 
Mwaka huu mmeshikwa pabaya! Umekazania Dar kuna Wenyewe, sasa wenyewe ndo kina nani?!
Acha kuwa na mawazo magando wewe, nijuavyo mimi Dar ya sasa sio ya kipindi kile Taifa linapata uhuru kutoka kwa mkoloni, ambapo asilimia kubwa walikuwa Wazaramo and the likes. Dar ya sasa ina-mchanganyiko wa watu (makabila) kila aina na kutoka kila pembe ya nchi kuanzia Wazaramo, Wasukuma, wadengereko, waha, wachaga etc. Single yenu mliyotoa ya u-Kaskazini imeanza kuchuja nini?! mmekuja na Single nyingne ya 'Dar kuna Wenyewe'?!. Baada ya hii single ya sasa, mtakuja na single gani?! Mbona kipindi hiki tutasikia mengi.
Hii ni dalili ya kushikwa sehemu mbaya na magamba yamepata moto.
Hii single yao inadhihirisha kuwa sasa tumewaingiza uvunguni mwao. Kama Gaddafi alivyofikishwa kwao Sirte,
Subiri kifo cha aibu kama cha huyo huyo Muammar Gaddaf.
 
Asili ya DSM ni Wazaramo, sasa hawa wazee uliowataja ni Kabila ipi vile.

Mwenzio sijajuagaaa!!!!!

KIMBUNGA iNAKUJA!!!!!!!

MIZAMBWA
NABII MTARAJWIA

Hivi hata kusoma hujui mkuu ? nimekuambia nakupa assignment, au hujui maana ya neon hilo?
 
Wana bodi nashauri tujenge utamaduni wa kupima thread zinazoletwa hapa jukwaani,maana watu kama huyu anaejiita Geniusbrain,sioni alichopost zaidi ya utumbo tu,kuendelea kujibizana na mtu kama huyu anaeweza kukiogopa na kukikimbia kivuli chake ni kupoteza muda wetu wakuu,jitu kama hili ni la kuachana nalo,kama haoni kinachoendelea na wala hasikii,wala hasikii hata harufu basi asubiri kusimuliwa japo huenda napo asisikie.na kwa kauli za mtu kama huyu kamwe hazina athari kwetu zaidi ni athari kwake
 
Back
Top Bottom