Kwa hili la CDM jangwani kweli Dar ina wenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili la CDM jangwani kweli Dar ina wenyewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GeniusBrain, May 28, 2012.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tathmini ya kisayansi ya mkutano wa cdm jangwani ni kama ifuatavyo :
  • Imedhihirika kweli DAR KUNA WENYEWE na si kama Arusha, kwani kwa idadi ya watu , Dar ina watu wengi kuliko Arusha , ila Arusha kwenye mikutano ya cdm watu wengi hujitokeza kuliko hata wale walioonekana jangwani pale kwenye kile ‘kijiumati’ japokuwa matangazo yalikuwa mengi. Hii yadhihirisha Dar ina wenyewe, na wengi wetu ni wakuja si wana Dar kindaki ndaki
  • Mbowe adhihirisha ni mgeni na historia ya Dar. Uwanja wa Jangwani anaujua historia yake? Ni jambo la kushangaza na kustaajabisha kuuita uwanja wa jangwani ni ‘cdm square’. Wenye hadhi hiyo ni wakazi wa Dar wenye kuujua asili ya uwanja ule, mtu km Mbowe wakuja hadhi hiyo ameipata wapi? Ni jambo la ajabu na kustaajabisha
  • Cdm kwa dar mambo ni magumu sana, tuliambiwa kwenye kwenye magazeti (na sijui km ni kweli) kuwa kwa arusha na yenye watu wachache kuzidi Dar watu 10,000 walirudisha kadi, ila kwa Dar na yenye watu wengi zaidi ya Arusha ni 3100 tu. Ndio narudia kusema Dar ina wenyewe sio mji wa kuvamia vamia tu
  Kwa haya machache yaonyesha wazi cdm kwa Dar mna kazi ya ziada, Dar ina wenyewe sio km Arusha. Na wengi waliojitokeza kwenye ule mkutano 80% ni wakuja si wana Dar kindaki ndaki.
   
 2. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nimefurahi kuona kuwa na wewe ulifuatilia yaliyojiri pale CDM SQUARE.
  Kumbukumbu ya umati kama ule uliona lini hapo jangwani ya ZAMANI (CDM SQUARE) kama si enzi za Papa John wa II.
  Sijui lakini kama unalijua hili maana unaonekana huna lolote unalojua.
   
 3. S

  Senator p JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwambie gamba hlo,litajulia wap?linasubr lifatwe na mafuso ya magamba kama mzgo ili lipelekwe.
   
 4. Ishina

  Ishina Senior Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwaka huu mmeshikwa pabaya! Umekazania Dar kuna Wenyewe, sasa wenyewe ndo kina nani?!
  Acha kuwa na mawazo magando wewe, nijuavyo mimi Dar ya sasa sio ya kipindi kile Taifa linapata uhuru kutoka kwa mkoloni, ambapo asilimia kubwa walikuwa Wazaramo and the likes. Dar ya sasa ina-mchanganyiko wa watu (makabila) kila aina na kutoka kila pembe ya nchi kuanzia Wazaramo, Wasukuma, wadengereko, waha, wachaga etc. Single yenu mliyotoa ya u-Kaskazini imeanza kuchuja nini?! mmekuja na Single nyingne ya 'Dar kuna Wenyewe'?!. Baada ya hii single ya sasa, mtakuja na single gani?! Mbona kipindi hiki tutasikia mengi.
  Hii ni dalili ya kushikwa sehemu mbaya na magamba yamepata moto.
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kampeni za ccm zakufunga wakati wa uchaguzi wa 2010 watu uwanja ule walijaa kuliko haw a wa cdm , nilishangaa kuona jangwani uwanja una gap kubwa sana japokuwa matangazo mliyafanya kwa nguvu sana. Duh kweli cdm Dar hamna lenu, napendekeza makao makuu ya cdm yahamie arusha
   
 6. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Kuna mijitu bado ina mawazo kuwa Dar ni yao! Endeleeni na uzaramo wenu, wajanja wanakuja na kukamata viwanja na kuporomosha majengo, nyie mnakazana kusema hao ni wakuja huku mkiwa mmewauzia viwanja!
   
 7. B

  Benaire JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Utaendelea kujisifu wa dar kindaki ndaki....wenzio tunatoka mkoa tunapiga business dar..tunajenga mikocheni....tunatanua kwenye viwanja high classic....tunakuacha temeke,keko magurumbasi na bendera ya CCM....Nyumba zetu,unakuja kupigia picha......sanasana utauza nyumba na kusogea kongowe...mwana kindaki ndaki huyo...we mjanja kweli....kumbe unajua dar imejengwa na kindaki ndaki?
   
 8. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli umepungukiwa na Haya. Pamoja na kufaidika na CCM, lakini weka Akiba ndugu yangu. Watu zaidi ya Elfu tatu kurudisha kadi za CCM pale Chadema Square wewe kwako ni Poa tu! Wenzio Nape na nduguze toka Mkutano ule wa pale Chadema Square siku hizi kwenye Dinner yao, Vidonge vya Usingizi ni sehemu ya Diet, wewe unaona poa tu!
   
 9. E

  Eddie JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2012
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maneno yako twayyyib! kale kajiumati wengi wao ni mafundi gereji waliobebwa na malori ya wachaga kutoka kigogo dampo, tabata, mabaamedi wa Sinza, wauza kitimoto wa kimara, mbezi, na ubungo.

  Hawa Chadema kweli wageni mjini hawajawahi kuona jangwa linavyojazwa? ule ulikuwa mkutano wa Injili tu ndio maana kulikuwa na makapu ya sadaka Lema anakusanya, mkutano wa siasa sadaka za nini?
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mtaendelea kuliwa na kauli ya dar ina wenyewe.ccm mpaka wajaze uwanja huo wa chadema square mpaka wamlete 50cent
   
 12. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #12
  May 28, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  GeniusBrain, nafikiri hujatafakari haya;


  1. Kati ya wazawa na wakuja, akina nani wengi? Kama ni wakuja, basi CDM ina mtaji mkubwa lakini kama ni wazawa bac hoja yako ina mashiko.
  2. Jina la uwanja linaweza kubadilika muda wowote, kwa sababu jina la JANGWANI halina uhusiano na historia yeyote ya jiji hili. Hivyo, jina la "CDM square" linawezekana.
  3. Pia huwezi ku-conclude kwa kuangalia mkutano wa CDM pekee, subiri waandae CUF au CCM kwa matangazo kama yale yale, bila kubeba watu kwa magari kutoka sehemu mbali mbali afu uone watu wangapi watahudhuria na wangapi watarudisha kadi za vyama vingine afu ndo uje na conclusion sahihi.

  TAFAKARI UPYA
   
 13. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mtaendelea kuliwa na kauli ya dar ina wenyewe.ccm mpaka wajaze uwanja huo wa chadema square mpaka wamlete 50cent,mmezoea kuupotosha ukweli na magamba yenu
   
 14. v

  vangiling'ombe Senior Member

  #14
  May 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=6]SOMA HII AMEANDIKA GAMBA MWENZIO. LABDA ITAKUSAIDIA KIDOGO. KARNE YA 21 UNAONGELEA WATU???
  KOSA LA CCM:
  Ukiangalia vizuri, CCM haina uwezo wa kubaki madarakani miaka mitatu ijayo; ukiangalia vema CCM haiko madarakani hata sasa: Ukiangalia kwa umakini CCM haiko madarakani tangu miaka kadhaa iliyopita!!
  Hivi inakuwaje wanaCCM wamegeukia kuangalia tuvitu tudogo dogo na kudhani hiyo itakuwa style ya kujijenga? CCM ya sasa iantumia style ya kutafuta makosa yanayofanywa na CDM halafu kinacapitalize humo wakati hiyo ni style ilitumiwa na CDM miaka 10 au 15 iliyopita... Hiki ni kichekesho yaani "Dereva anakuwa Konda na Mpiga debe anakuwa dereva basi lile lile"
  CCM ya Nape ni mzigo kwa taifa; wanachama wanaotumika humu FB na janga la CCM na wafuatiliaji wa masuala ya siasa wanaweza kusema wazi CCM imekuwa kero kuanzia mtaani hadi mtandaoni.
  CCM haina pa kujirekebisha maana imeshafikia "point of no return" lazima "ibiringite"; imejiua yenyewe na kila anayejaribu kuiokoa ndo anaiua zaidi. Eti CCM ni ya kuangalia ruzuku ya CDM? CCM ya kuangalia eti watu wamebebwa kwenye mikutano wakati kila mtu kaona wamekwenda kwa miguu? Huu ni upuuzi ambao miaka 20 baadaye mtajuta kwa nini hamkutumia akili!
  Kuna wanaojiona wasafi ndani ya chama; ni kweli tunataka waadilifu; lakini uadilifu CCM ni msamiati tulioufuta kwa makusudi ili kubakiza misamiati michache. Kuna wanaojiona ndo wazalendo sana; wakati wameshindwa hata kulifanya gazeti la Mzalendo (sijui) kama bado lipo. Kama umeua gazeti la Mzalendo wewe unawezaje kuwa Mzalendo? CCM yangu inakufa huku bado naipenda, na nawaona wanoiua lakini hawagusiki maana wanaishi dunia nyingine ukiwagusa wewe si mzalendo.
  CDM wameanzisha "Opereshen Vua Gamba, Vaa Gwanda" ETi kuna operesheni "Vua Gamba na Gwanda, Vaa Uzalendo" Huu ni utoto ambao hata mwanangu XTINA hawezi thubutu kufanya. Nani atawaamini? Mna hela ngapi kukodi mafuso na kununua wali kwa ajili ya watu mtakaowaleta mkutanoni? Mna nini kipya cha kusema wakati mmeshindwa kutekeleza maagizo ya mikutano yenu, mtaweza ya mitaani? Kweli Nape una utani na Chama changu CCM!
  Mambo ya kulindana yatafika mwisho wake; lakini kuendelea kumlinda Nape ni kuua chama. Nape atupishe maana chuki yake dhidi ya CCM haijaisha na ameamua kuiua akiwa ndani baada ya kushindwa kutoka nje. Na Nape ukitoka CCM utakuwa ni mtu usiye na lolote na angalau CCM itasonga mbele hata kama si kwa mwendo mrefu. Ninakuambia haya kwa sababu siku zako za kukaa ndani ya CCM zinahesabika na huna ujanja wa kuzizuia. Muiache CCM ife natural death, msiiaccelate ufaji wake.
  [/h]
   
 15. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wewe na Mzee Akilimali wa Yanga inaonekana mawazo yenu na akili vinafanana, asante kwa kututuknana. Ndio maana wengine tueamua kubakia huku kwetu na M4C mkiikataa itashika kasi kutokea huku huku!

   
 16. ketwas

  ketwas JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 213
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wale wa kufunga kampeni walibebwa na malori hawa wa chadema hakuna hata mmoja aliyebebwa na malori,hata sisimizi wenyewe hakuna hata mmoja aliye kanyagwa kutokana na ule umati kutulia na kusikiliza mambo ya msingi wa taifa letu
   
 17. m

  mamajack JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  pole mwehu wa ccm.cdm hawana usafiri wa kukusanya watu kama wafanyavyo mafisadi.
  wele ulotuona pale ni wana dar tunajua tulifanyalo sio wewe kibaraka mkubwa wakati huna lolote ujualo.
  wajua wizi tu weye,jingine huna,na kama msimu huu hukupata shukurani yako kutoka kwa ******,basi imekula kwako,umesahauluka maana hatitatokea tena.
   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Dar in a wenyewe hili halina ubishi, hata mwalimu alipokuja dar alilitambua hili, na yeye mwalimu alijijua ni wakuja na si mkazi wa dar mwenye asili yake. wengine wapo ndio ila si wenye dar, ni wakuja wa dar
   
 19. K

  Kimbito nyama Senior Member

  #19
  May 28, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha kuchezea Sayansi wewe! unasema tathmini ya kisayansi wakati kila ulichoweka ni porojo? umesema Dar ina watu wengi kuliko Arusha. kisayansi ningetegemea uweke figures DSM...., Arusha.......

  Pia umesema wakazi wa Dar wanajua historia ya Uwanja, ungedokeza hata kidogo au 'quote' historia hiyo.

  Arusha Watu 10,000 walirudisha kadi, Dar 3100, una data za watu ambao bado wana kadi za CCM Arusha kabla ya hizo 10,000 kurudishwa na Dar kabla ya hizo 3100 kurudishwa? Hiyo ndiyo analysis ya kisayansi ambayo ungeweza kufanya.
   
 20. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Wewe waonyesha ni wale wale wakuja wa dar, km kin a Mbowe, Slaa, Mnyika nk asili yao ni kaskazini si Dar, na ww umo kwenye kundi hilo. Wote wa kuja mnajulikana tu, inawauma sana kusikia Dar in a wenyewe na ndicho mlicho kipata pale jangwani
   
Loading...