Kwa hili la bunge live natamani lifanyiwe marekebisho

machila

Member
Jan 4, 2017
52
20
Kwa kipind kirefu sasa nimemis bunge live, wakubwa wakasema bunge litarushwa usiku ili mchana tufanye kazi, ok ni mawazo mazuri maana watanzania ni wasikivu mno.

Kinachonishangaza wale waliosema tuangalie bunge usiku il mchana tufanye kazi wanazunguka huku na huko tena mchana kweupeee wakirusha hutuba zao mubashara tena sikitumia muda kuliko ule wa bunge cha ajabu hutuba hizo hazina marudio usiku ili sisi tuliotii agizo kufanya kazi tuwezekuona ukikosa mchana ndo basi tena, nikawa najiuliza kunani hapaa nikapata jibu kumbe hii mubashara ni kwa ajiri ya baba tu!

Mhm , nikajiuliza sasa kama mubashara ni kwa baba tu na yeye ni sehemu ya bunge kwa nn katiba yetu isiboreshwe ili kumuwezesha baba kuhutubia vikao vyote vya bunge maana kwa kufanya hivyo naamini bunge live litarudi tuuu. Hapa baba tu.

Watoto ukonga,!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu kibaya kama double standard na mbaya zaidi itumike kwenye kuminya suala muhimu kama demokrasia..

Rais yeye anafungua miradi toka saa 4 asub na anakuwa live na anahutubia hotuba ambazo zimejaa kila namna ya Kampeni..

Huu ni uonevu mkubwa kwa vyama vya upinzani..

Watu wakilalamika kuna ubaguzi ndio huu jamani.

Yana mwisho haya.
 
Back
Top Bottom