Kwa Hili la BBC Halikubaliki na ni Ubaguzi Mkubwa

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,029
2,000
Nashindwa kuelewa kwa nini BBC Swahili tawi la Tanzania wamekuwa namna hii, hii tabia yao ya kubagua wanafunzi wa field kutoka vyuo vingine na kukubali wa UDSM tu si sahihi,

Mnaua ndoto za vijana wengi wenye nia na hamu ya kufanya kazi BBC kama si kuongeza ujuzi zaidi kupitia shirika hilo, Mnafaa mjua si kila anayesoma UDSM basi ana quality za ziada za kujifua na idhaa yenu,

Wapo vijana wengi kwenye fani ya uandishi wa habari katika vyuo vingine vya kati na vikubwa lakini kwa kuwa mna utaratibu wa 'kibaguzi' unawafanya vijana hao wajikute wasifikie njozi zao,
Badilikeni bana
 

Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,081
2,000
Pole sana Mkuu kwa kadhia hiyo.

Huenda wana vigezo vyao vya kutoa field kwa wahitaji, na pengine wa vyuo vingine hawakidhi vigezo elekezi. Hivyo kutopata nafasi ya kufanya 'pt' hapo katika ofisi yao.

Cha msingi, wewe tafuta pengine. Jitume, piga msuli vema na kuwa mbunifu. Baada ya kumaliza chuo, utawapiga gepu hao wa UDSM. Na pengine hao hao BBC watakutafuta wakupe Ajira, nawe utawadengulia.

Wakikukataa, walazimishe kukutafuta.
 

SDG

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
7,638
2,000
Nashindwa kuelewa kwa nini BBC Swahili tawi la Tanzania wamekuwa namna hii, hii tabia yao ya kubagua wanafunzi wa field kutoka vyuo vingine na kukubali wa UDSM tu si sahihi,mnaua ndoto za vijana wengi wenye nia na hamu ya kufanya kazi BBC kama si kuongeza ujuzi zaidi kupitia shirika hilo,mnafaa mjua si kila anayesoma UDSM basi anaquality za ziada za kujifua na idhaa yenu,wapo vijana wengi kwenye fani ya uandishi wa habari katika vyuo vingine vya kati na vikubwa lakini kwa kuwa mnautaratibu wa 'kizwazwa' unawafanya vijana hao wajikute wasifikie njozi zao,badilikeni bana
Nenda TBC mkuu
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,197
2,000
Pale mtafuta Kazi anapompangia muajiri nini azingatie kwenye kuajiri!! BBC ni yao sisi tuna TBC nenda TBC
 

masare

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
442
500
UDSM is the best University in East and Central Africa.Kwa Africa inashika nafasi ya 13 ikizidiwa na vyuo vya Afrika Kusini na kimoja cha Misri tu. International wise UDSM ndio inajulikana hivyo hata mashirika makubwa ya kimataifa kama BBC yanatambua ubora wa UDSM tu na sio vyuo vingine vya Kata
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom