Kwa hili la Afya toto kadi(NHIF)Waziri tusaidie

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Mwanzoni mheshimiwa waziri Ummy ameiongelea vizuri na kutuhamasisha wazazi tuwakatie bima ya afya watoto chini ya umri wa miaka 18 kwa gharama nafuu...wananchi tulipokea hamasa hiyo kwa furaha kubwa tukijua sasa tumepata mkombozi upande wa tiba na kwa hilo tukupongeze mh waziri

Nadhani ni mwaka wapili sasa tokea wananchi tuanze kupata huduma hiyo lakini wiki hizi NHIF wameanza kuleta sintofahamu kwenye mpango Huu,ni kwamba kwa miaka michache iliopita baada ya kujaza documents zote na kukamilisha malipo yao ya mwaka walikua wakitoa kadi baada ya siku 21,japo ilikua ni ka hatua watu tulivumilia hizo wiki tatu,lakini kama vile haitoshi wamebadilika tena,hivi sasa ukishawalipa huipati kadi ya mtoto mpaka siku 90 zipite !!

Hii maana yake nini ? Huku sio kucheza na afya za watu ? Huku si kutesana ? Ni nini kinapelekea kadi kutengenezwa kwa miezi mitatu tena na pesa mnachukua ? Mbona benki taasisi nyeti kabisa lakini wiki haifiki wanakupa kadi yako ?

Tunaomba waziri husika hebu tusaidie uliulizie jambo hili na kuliweka sawa
Nhif kwanini mmetufanyia hivi ? Au mpaka siku mheshimiwa Rais azuke ghafla ofisini kwenu na kuwauliza hili....mtamjibu nini ?

Tunaomba siku 90 ziondolewe zibaki walau wiki mbili.twatumai wahusika mmesikia au mtaambiwa kwa swala hili.
 
Sio kweli,kama ni siku 90 maana yake kadi utakua nayo kwa kipindi cha validity yake kwa miezi 9 tu.
 
Back
Top Bottom