Kwa hili Kikwete hatutakusamehe, umeuza nchi yetu mchana kweupe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili Kikwete hatutakusamehe, umeuza nchi yetu mchana kweupe?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by babuwaloliondo, Aug 25, 2011.

 1. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Bibi Mawazia Kibwana , mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, akitoa malalamiko kuhusu kubomolewa choo chake na kuwekwa kwa uzio wa seng'enge na kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa Raia wa kigeni aliyeuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia yakwenda mtaa wa Mwanga kama walivyokutwa juzi Kijijiji hapo.
  [​IMG]


  Moja ya nyumba ambazo uzio umepita na kuziba vyoo vyao.


  [​IMG]  Wananchi wakitahamaki na kutokuamini wanachokiona.  [​IMG]
  [​IMG]


  Wananchi wakipita jirani na Jumba ambalo awali watoto walikuwa wakilitumia kama darasa la chekechea ambalo sasa linamilikiwa na mzungu huyo.
  [​IMG]


  1. Kikwete naomba nikuulize, ni kitu gani watanzania wamekukosea?, mpaka umeamua kuwauza katika nchi yao wenyewe?

  2. Hivi ni kweli kuwa watanzania wameshindwa kufuga hata kuku mpaka waje wawekezaji kutoka nje?.

  3. Hivi wewe ni mtanzania kweli, au unauraia wa nchi nyingine?  Source: Wananchi wa mchachamalia Mzungu aliyeziba njia na kuchukua mashamba Kinyenze, mkoani Morogoro ~ Father Kidevu
   
 2. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Hao wana nchi wa vjijni ndo wanang'ang'aniaga magamba waacheni yawatokee puani ukija uchaguzi huwaambii kitu wakisha pewa vilemba na kofia wanakua wehu kabisa na kutupa maneno ya kejeli sisi tunaopigania uhuru.
   
 3. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mhmmmmmm, mama yangu tanganyika shughuli ipo. Mpaka miaka hiyo iliyobaki ikiisha tutajikuta wote ni watumwa huko ughaibuni... Ee Mungu tuepushie janga hili, ccm ni janga la kitaifa
   
 4. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  zubaa ili uzikwe!
   
 5. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ati nini?!?
   
 6. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kama kweli sisyemu imekuwa janga la kitaifa, mturuhusu sisi walokole tufunge na kuikemea isambaratike kesho tu! Freedom is coming tomorrow.
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Serikali isilazimishe wananchi kuchukua sheria mikononi mwao.

  Mzungu mmoja....wananchi wako wangapi?

  Ukipiga mahesabu ya haraka, utaelewa tatizo liko wapi.

  Kwa nini Tanzania tunatega bomu la wakati? Nini kilitokea Zimbabwe?

  Kuna viashiria vingi vinavyoonesha kuwa Tanzania itaripuka siku za mbele.

  Baadhi ya viashiria, mwananchi wa kawaida ni zulia. ufisadi, 10% mentality kwa jamii yetu, maisha bora kwa kila mtanzania, usanii wa katiba mpya, 3% kutoka katika dhahabu yetu, umeme wa dharura, polisi kuua raia kinyemela, uchumi kupaa na kukua kwenye makaratasi tu huku mlalahoi mfuko unatoboka, elimu fasta fasta, taarifa za kiintelijensia inapokuja maandamano au mikutano ya vyama vya upinzani , rushwa na wingi wa malalamiko ya wananchi bila ya kuchukua hatua za kuwawajibisha wasiotimiza wajibu na majukumu yao nk.
   
 8. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaani migogoro ya ardhi inazidi kuongezeka kila kukicha. Hawa wanaoitwa wawekezaji hawana lolote jipya.
  Eti kisingizio ni kuongeza ajira, mimi nashindwa kuelewa hizo ajira zinaongezwa kivipi?

  Ikiwa wanavijiji wamejiajiri wenyewe kwa kilimo chao cha kila siku, leo eti wanaletewa mfugaji kuku ambaye anachukua ardhi yao, na kisha anawaajiri katika shamba alilowanyanganya?

  Yaani , Kikwete hatutakusamehe, kweli hatutakusamehe labda uame nchi 2015
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Tanzania nchi ya kufikirika.

  Huyu ulitegemea aseme hivi? mtendaji ni nani? Kila mtu anategemea mwenzake kuwa ndio atakayetenda, tunaishia kuwa hakuna kinachotendeka cha maana na wala hakuna anayeadhibiwa.

  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amezitaka mamlaka za dola kuwafukuza kazi, viongozi wakiwamo mawaziri wenzake waliojilimbikizia mali kwenye biashara kupitia nafasi zao.

  "Nchi imebaki mifupa mitupu huku wananchi wake wakiteseka kwa kushindia mlo mmoja na wengine wakiishi kwa kuokota vyakula majalalani, wakati huo baadhi ya watu wachafu wakiwamo viongozi wao wanaendelea kuneemeka bila kujali maisha duni ya mwananchi," alisema mjini hapa katika ufunguzi wa Kongamano Vijana wa Kikristo kutoka nchi za Afrika Mashariki.

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/166892-sitta-nchi-imebaki-mifupa.html
   
 10. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  Dah hadi kichwa kinauma ukifikiria madudu ya nji hii,ngoja nikapoze akili lah!
   
Loading...