Kwa hili, JK awaombe radhi Watanzania kisha athibitishe kuwa ni Muongo. Hatutaamini asemacho tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili, JK awaombe radhi Watanzania kisha athibitishe kuwa ni Muongo. Hatutaamini asemacho tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Dec 29, 2011.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Wanajamvi nimejaribu kumpima Mkuu wangu wa Kaya nimeshindwa kabisa kupata link na baadae nikawaza nikasema labda mie ndo mjinga. Hebu someni kauli hii ya Jk pale CCM ilipotimiza miaka 34 kule DODOMA.

  "Ukweli siwajui wenye Dowans na wala kampuni hiyo siijui...wapo wanaosema
  sijasema kuhusu Dowans kwa sababu wanaohusika ni rafiki zangu....sijasema kwa
  sababu Chiligati na Pinda wamesema, waliyosema yametokana na kikao changu cha
  kamati kuu...." Hii ni kauli ya Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 34 ya
  kuzaliwa CCM.JK ameeleza kuwa Wakati waziri wa Nishati na Madini Salum Msabaha
  alipomfuata kudai kuwa wizara ya fedha imegoma kuwalipa Dowans, lakini yeye
  alimtahadharisha kuwa hii inaweza kuwa kampuni feki.....

  Haya aliyasema na niliona mwenyewe na watanzania wengine waliona na kusikia.
  Vide hii hapa

  <font size="3"><font color="#ff0000"><span style="font-family: Cambria"><span style="font-family: Cambria">


  Baadae kidogo kwenye Mkutano wa NEC mwaka huu pale Lowassa alipopewa nafasi ya kuongea Akasema maneno haya kwa Kikwete ambaye hajayakanusha hadi leo kwa sababu alitikisa kichwa kuyakubali.


  Lowassa amkumbusha Rais Kikwete

  "Lakini Mwenyekiti, naamini utakumbuka jinsi nilivyotaka kuvunja mkataba wa Richmond, nilikupigia simu ukiwa nje ya nchi, lakini ukasikiliza ushauri wa kamati ya makatibu wakuu (Kikwete akatikisa kichwa kukubaliana naye) , mheshimiwa ushauri wa kamati ya makatibu wakuu ndiyo uliopelekea mkataba usivunjwe.

  "Pia naomba nikumbushe, nikiwa Waziri wa Maji niliwahi kutuhumiwa kuhusiana na kampuni ya City Water, tena nashukuru Mzee Nimrod Mkono yupo hapa, tukaenda kwenye kesi tukashinda. Sasa katika hili la Richmond kosa langu ni lipi? Je kuwajibika kwa maslahi ya chama changu na ya serikali yangu, utakumbuka ripoti ya Dk. Harrison Mwakyembe wakati anahitimisha Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, alisema kuna aina mbili ya uajibikaji, kwa makosa ya kiongozi mwenyewe na watendaji walioko chini ya kiongozi,

  "Dk.Mwakyembe akasema Waziri Mkuu aliyejiuzulu amejiuzulu si kwa makosa yake, bali ni makosa ya watu waliokuwa chini yake (huku akiwa ameshikilia Hansard ya Bunge),"

  "Mwenyekiti naomba nikukumbushe kuhusu kashfa zinazohusiana na &#8216;political perception', kama si busara za kina Mzee Mkapa mwaka 1997 kule Zanzibar, leo hii usingekuwapo hapo ulipo na ulisema urais ni mipango ya Mungu.

  "Unakumbuka kina Mzee Sozigwa jinsi walivyokuja na mafaili kwenye mkutano huo wa NEC kwa ajili ya kukumaliza.


  "Hata nilipokutana na Mzee Msekwa pale Dar es Salaam, aliniambia kuna watu wananoa mapanga kwa ajili ya urais wa Lowassa.

  "Kibaya zaidi, wanaonitukana ni wana-CCM (Nape, Chilligati na wenzao), lakini hata CHADEMA na wapinzani wengine hawanitukani," alisema Lowassa.


  MY TAKE
  Sasa ninachojiuliza na kushangaa ni kuwa Lowassa alipompigia simu JK si kwamba alikuwa anaitambulisha Richmond kwa JK bali alikuwa anataka kuvunja mkataba na Richmond ambayo JK alikuwa akiifahamu!!!!!!!!!!!^$%#* 100%. Kwa nini Watanzania tudanganywe kiasi hiki alafu tuendelee kuchekacheka???? Sasa Jk atuambie vipi tene tuamini anachokisema. Kama ulikuwa huijui Richmond kwa nini Ulikataa mkataba usivunjwe. Hii ni aibu kama pale baba awadanganyavyo wanae kisha wakajua kuwa baba yao muongo. Tuombe radhi vinginevyo hata utakayemrithisha kijiti ni dizaini hiyo hatutamchagua. Nina hasira vibaya sana ninavyoongea hivi ungeniona sura usingeamini.


  Usingeamni kama mimi ndiye nilibeba T- Shirt za CCM mwka 2005 na kuwagawia wanafunzi wa Chuo Kikuu Mlimani na kuwasombelea kwenda Diamond Jubilee kukushangilia tukiwa na matumaini makubwa na wewe. Kumbe loo... hadi aibu sasa hivi... kila aliyesema kuwa wewe hutafanya kama ulivyovuma nikambishia sasa hivi namuomba radhi. Na jamaa yangu aliyekuwa akisherekea kunywa soda za wanaharakati wakati anamsaidia Mnyika kuomba kura pale Mabibo Hostel chumaba hadi chumba ili Mnyika ashinde jimbo la Ubungo kisha kura akawapa magamba wote lazima awaombe radhi wanaharakati na zitapike hizo soda. Huyu mzee Jk yaaani...... basi ngoje nilie na kutubu kwa Mungu wangu ninayemjua. Najua waliofanya makosa kama mimi 2005 wako wengi kubalini kisha tusonge mbele. CHADEMA tekelezeni myasemayo kwa wananchi ili na wao wananchi waone tofauti. Baada ya hapa Nilihama rasmi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kumbe ulikuwa unamwamini j.k?!
   
 3. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Hamna jipya!
  JAKAYA KIKWETE ni mwongo asubuhi,ni mwongo mchana ni mwongo hata jioni.
  Ninyi ambao bado mnasubiri aombe radhi ili mumchague chaguo lake ndio magamba wa hii nchi.
  Hamna haja ya kuomba radhi,labda a-step down,au asubiri kuondolewa kwa chama chake 2015!
   
 4. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Mkuu enzi hizo tulipotea vibaya sana. Sio mimi tu walikuwa wengi....kwani alishinda je kwa kishindo???
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mkuu,funika kombe tu

  umekosea njia jana leo hutokesea tena,kupanga ni kuchagua,anza sasa kupanga iliuweze kuchagua kilicho bora
   
 6. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Mkuu kustep down ndo inakuwa ngumu hebu shauri iweje
   
 7. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Asante mkuu tukikiri kuwa tulikosea tena mbele ya jamiii kuliko kukiri kimya kimya hatutafanya mambo ya Shayo wa Sumbawanga.
   
 8. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  kAMA NI VIGUMU,BASI AENDELEE KUBORONGA ILI HASIRA ZA WATZ ZIENDELEE KUPANDA!
  Zitakapofika maximum limit,tutamiminika mitaani kuleta ukombozi wa pili!
   
 9. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unamwongelea nani huyu jk ,rais wa NEC?
   
 10. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  aisee mlinikera kipindi kile mimi nipo UCLAS nikiangalia raia na akili zao wanapewa tshirt na kofia kisha wanasombwa kwenye mabasi kwenda kumlaki fisadi, niliwashangaa sana aisee, nasiki kitendo cha kushika ile nguo yao ya kijani tu ndo umeshajiloga, pole sana, siku nyingine usikurupuke. vyema umetubu.
   
 11. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Asante sana mkuu
   
 12. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo common sense inakataa kabisa kwamba hayo maneno yalitolewa na mtu mmoja ahakuvunja mkataba wa watu ambao hanataarifa nazo sasa huo mkataba haukuwa na details za pande mbili? Kama taarifa za pande mbili zipo basi aliongea kwa namna ya kujisafisha tu.
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,139
  Trophy Points: 280
  unayoyajua na unayoyasikia kuhusu kikwete ni machache tu kati ya mengi yaliyokaribu kutokea subiri uone picha kamili ya kikwete wako aliyefanikiwa kuingia ikulu kwa kukupa pilau na pombe za kienyeji..
   
 14. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kama ulikuwa unamwamini kikwete ulitumia kigezo gani? Mbona huyo jamaa hakuwa na rekodi yoyote iliyotukuka.
   
 15. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Siku zote tukimjadili JK mods wanafuta haraka sana thread hizo, sina hakika kama na hii wataiacha hadi kesho, inafikia wakati we beg to believe hii JF ina walakini aisee. JK ni rafiki yangu sana tena sana, kukweli hata mimi nishaacha kumwamini kitambo sana.

  Ipo namna ya kwa nini JK anaonekana ni president aliyeshindwa kwa lolote na ambaye ni kama robota la misumari kwa watanzania maskini kama mie.

  JK ni ndumilakuwili ambaye anapenda kujionesha kuwa yuko kila upande simply to offload blame to a concerned folk, na hao folks wanajua maovu kibao ya JK ndio maana anashindwa hata ku'act' kama
  baba wa kaya badala yake yeye kawa business as usual, hebu ona haya tu machache, mosi, kwa nini alisaini makabrasha ya utaratibu wa katiba mpya masaa tu toka aonane na chadema je alipanga kuwaaibisha? Pili
  hebu ona NEC sasa inavyoongozwa na wachovu wapya waloteuliwa indeed they are full of blames huyu mara madaraka mabovu, mara mlungula, halafu JK anakurupuka na kuwapa madaraka makubwa kabisa hivi do you real suppose that right will be seen as executed? Ona mabalozi wetu waloteuliwa , hivi Batilda, Dr kweli watu wa Arusha wamuone hafai halafu JK aone anapaswa kuwakilisha nchi na sio jimbo, hivi wajameni rais ana akili na bisara kuliko wananchi wake!

  Ona cabinet yake, kila mtu na lwake, yeye wala anadunda tu, hivi rais yuko bize hadi hajui whats happening on the ground?

  Ila una haki JK, niliona wakati wa kampeni zako za urais kila mtu alikususa, watanzania wakawa wanataka chadema badala yako, ukafanya kampeni kubwa kana kwamba hatukujui, mabango ya matangazo yakajazana picha zako utadhani na wewe bidhaa sasa, ukafanya kampeni wewe, mama Salma na Watoto wenu bila kupumzika, sasa urais ni wako usimsikilize hata Mihambo aliposema 'nchi iko auto pilot', usijali mkuu chapa mwendo tu, na ukiondoka baba tunakuomba ututeulie na lowassa akurithi ili tushike adabu vizuri.

  Mwisho, mtamlaum bure JK, ujue katiba inasema sio lazima rais akubali maushauri yenu, hata mkianzisha gazeti liitwalo 'udhaifu wa JK' halafu mkaligawa burw msidhani yeye atajali sanasana mtaishia kuswenkwa magereza muache watoto wenu wakihangaika, JK baba yetu chapa mwendo tu, kama kuna ambaye anataka urais basi afuate utaratibu sio kubwabwaja kila siku.

  Hata kama ulisema huijui Dowans ulikuwa sawa tu mkuu wangu, sio lazima ujue kila kitu, ndio maana baba ukaweka wasaidizi wako, mawaziri husika na makatibi wakuu, wao ni lazima wajue na ndio maana baba lazima tulipe mabilioni.

  Mwisho baba, nakuomba usihangaike na wapayukaji, kama mleta thread ni makini basi angetoa na suluhu yaani mawazo yake sio kulalama kama alivyofanya.

   
 16. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Mwana alikuwa akiahidi na kuongea kwa confidence.
   
 17. only83

  only83 JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mkuu wewe ndio unamuona JK muongo leo? Mimi uwa namwangalia tuu anapokuwa anaongea bila hata kuona aibu anaendelea kuwadanganya watanzania kwa mengi tu...kwa kawaida Mungu uwa hamfichi mnafiki..na hii ndio zao la unafiki...
   
 18. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Hapa bado haujamtia JK hatiani kwa ushahidi huu labda kivingine, ndio tunajua kama JK mchezo mzima anaufahamu.

  JK alisema haijui Dowans
  EL anaaongolea alivyotaka kuvunja mkataba wa Richmond.
   
 19. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #19
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Hivi ungekuwa wewe ungekuwa unajisikiaje?
   
 20. T

  Thanksgiving Member

  #20
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, wenge mnashindwa kumuelewa vema JK, ni kawaida yake kujinukuu vibaya yeye mwenyewe, sembuse watu wengine?
   
Loading...